Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Tuesday, 30 December 2014


Mwanza
    katika Kijiji cha Ndami mkoa wa, tarafa ya Mwamashimba wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza watu wasiofahamika wamevunja nyumba na kumteka mtoto mwenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino na kutoweka naye.
    Watu hao walivamia nyumba ya wazazi wa mtoto Pendo Emmanuel, mwenye ulemavu wa ngozi wakiwa na mapanga na kisha kutoweka naye gizani baada ya kuwazidi nguvu wazazi wake.
Emmanuel Shilinde mzazi wa mtoto huyo ameieleza polisi kuwa majira ya saa nne usiku watu wawili waliuvunja mlango wa nyumba yake kwa jiwe wakamchukua mtoto kwa nguvu kisha wakakimbilia gizani kwa pikipiki.

    Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi mkoani mwanza Valentino Mlowola , ameitaarifu BBC kuwa leo ni siku ya tatu na polisi bado ina matumaini ya kumpata akiwa hai motto huyo, kwa kuwa bado hawajaupata mwili wake akiwa amepoteza uhai. Msako unaendelea na tayari kuna watu watano wanazuiliwa na polisi ili kusaidia kufahamu mtoto huyo yuko wapi.

    Takwimu za kuanzia mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wamepata ulemavu mwingine wa kudumu.

Read More

0 comments:

Jana ilinyesha mvua kubwa jijini Dar Es Salaam, ambapo mitaa kadhaa katikati ya jiji hilo imekuwa taabu kupitika, kwa wenda kwa miguu na pia magari. Mara kwa mara mvua kubwa zinaponyesha jiji la Dar Es Salaam hukabiliwa na matatizo hayo. Unadhani kipi kifanyike ili zinyeshapo mvua kama hizi wakazi wa jiji hilo wasikumbwe na matatizo hayo ya mara kwa mara?

Read More

0 comments:



    Shughuli ya kutafuta ndege AirAsia ambayo iliyopotea juzi usiku wa kuamkia imeendelea leo tena baada ya zoezi baada ya zoezi hilo kusitishwa kwa muda, ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Bornea ambapo ndege hiyo ilipotea

    Ndege ya indonesia imepotea ikiwa na abiria 162 ikitokea Surabaya nchini humo na kwenda singapore, habari za kupotea ndege hiyo QZ8501 zilianza kutolewa na mitandao mbalimbali ya kijamii mara baada ya kupata taarifa kutoka katika akaunti ya facebook ya Air indonesia.

    Kampuni ya kutengeneza ndege ya Airbus ya ufaransa ilisema ndege hiyo ilikabidhiwa kwa kampuni ya AirAsia ikiwa miongoni mwa ndege zilizozalishwa mwaka 2008 na hadi jumapili shirika hilo limedai kuwa ndege ilikuwa imesafiri safari 13,000 ambayo ni sawa na masaa 23,000

    Tarifa zilozo patikana katika vyanzo mbalimbali vya habari  za kimataifa zinasema marubani waliomba kuchepuka njia kutokana na hali ya hewa mbaya iliyokuwepo kwa wakati huo ni kwa mujibu wa shirika la usafirishaji wa  anga la indonesia (CAA).

    Uongozi wa kampuni hiyo ulithibitisha kupotea  kwa ndege aina ya Airbus320-200 yenye namba za usajili PK-AXC iliondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Surabaya saa 11:35(7:35 usiku) na kupoteza mawasiliano nawaongozaji wake saa 1:24(9:24usiku)

    Ndani ya ndege kulikuwa na abilia 155 ambao kati yao watu wazima walikuwa 138 na watoto 16 pamoja na mtoto mchanaga mmoja, pia walikuwamo marubani wawili,wahudumu wanne na muhandisi mmoja ambapo mingoni mwao kulikuwa na raia wa nchi mbalimbali wakiwemo raia 156 wa indonesia,wakorea watatu, na raia mmoja wa ufaransa,malaysia na singapore

Hadi sasa juhudi za kuisaka ndege hiyo zinaendelea kwa kushirikiana na shirika husika la CAA AirAsia
Read More

0 comments:



Read More

0 comments:

Tuesday, 16 December 2014



   

Mtumishi wa mungu  na mkurugenzi JP & E Company Jeremiah Mwakanyelenge amewataka watu wote kutembea na kuishi  katika kweli ya Kristo hasa wakati wa kipindi hiki cha christmas na mwaka mpya. Maneno hayo ameyasema jana katika semina ya wanahuduma wa JEM GOSPEL MINISTRY yenye makao makuu jijini Mbeya na watenda kazi wa Jp & E Company.

     Mtumishi huyu ambaye anamtumikia Mungu katika kufundisha na kuhubiri duniani kote amenukuliwa akiwaasa wanahuduma ya JEM na jamii kwa ujumla wasifanye maandalizi  yaliyotofauti na mapenzi ya Mungu katika kusherekea sikukuu za mwaka mpya na krismas, bali wawezefanya mambo yanayo ugusa moyo wa Kristo kwa kuyaenzi matendo mema ya kumpendeza Kristo na jamii kwa ujumla.
      Alisisitiza kwa kusema dunia ni ileile ya tangu  uumbaji, lakini matendo ya wanadamu wanaobadirika fahamu zao kila siku yanasababisha dunia ya leo ionekene ni mpya na iliyojaa maovu mengi kuliko mema maana siku za skukuu kama hizi wengi hupoteza maisha na wengine hupoteza baadhi ya viungo vyao kwa kupigwa ambapo tayari amani na raha ya kuazimisha kuzaliwa kwa Yesu inapotea.
    Alihitimisha kwa kuwakaribisha watu wote katika ibada za ya JEM GOSPEL MINISTRY kila siku ya jumatano na jumapili jioni eneo la Soweto block Q .Pia aliwakaribisha watu waje JP PRODUCTION kwa kurekod audio,video,kudurufu CD,kukodi vyombo vya mziki na gari ya matangazo kwa gharama nafuu. Read More

0 comments:





  Anaitwa Faridah Efesi Ambonisye ni mwimbaji wa nyimbo za injili na nyimbo na anatambulikana kwa jina la nyimbo yake - USIJIINUE na alizaliwa tarehe 31-july 1995  na alizaliwa mkoani Mbeya (chunya mjini-ujenzi) na kwa sasa unaishi  mkoa wa mbeya eneo la soweto na ni mwanafunzi  lakin pia anajishughulisha na huduma ya uimbaji wa nyimbo za injili.

Farida alianza kuimba kwaya akiwa na msukumo wa huduma ya uimbaji ndani yake, kwaya mbalimbali ameweza kuimba nazo kama vile vijana “A” Chunya,isanga,Ruanda katika makanisa ya Moravian Tanzania; lakini hali ilibadilika mnamo mwezi wa 12 mwaka jana alipo sikia wito wa kuhudumu binafsi kwani watu wengi walimshauri kuaza huduma hii na pili ni huduma aipendayo kwa siku nyingi.
 
 Katika  kila kitu kizuri hapawezi kosa changamoto na kwa Farida changamoto anzo zipitia katika huduma ya uimbaji ni kuvunjwa moyo na baadhi ya watu walio mtangulia kihuduma kwani wao hujiona kuwa wamefika na kuwadharau waimbaji wanao anza huduma hii ya uimbaji wa nyimbo za  injili lakini pia kukosa wadhamini wa huduma hiyo kwani anatamani kufanya huduma mahali pengi na kwa wakati muafaka lakini tatizo kubwa ni upatikanaji wa pesa za kurekodia nyimbo zengine ili kukamilisha albam yake

 Malengo yake makuu katika huduma yake ni kuimba na kumaliza abamu na kurekodi albamu yake,kutamani watu waokoke kupitia huduma hii ya uimbaji kwani ni kitu anachodhani kuwa ni agizo la mungu kwake, lakini pia kufahamika kwa huduma ndani na nje ya nchi

    “kiu ya kufika mahali ndiyo itakayo kuwezesha kufanikiwa katika kila kitu unacho kitamani kufanya”
 Ushauri wake kwa waimbaji wale wanaohitaji kuanza kuhudumu kwa namna ya uimbaji wasikate tamaa hata kama hali yao kifedha ,maisha na hata vita vya huduma wawe roho ya kusahau yale wanayo yaona bali kutazama mungu anasema nini kwako,na kuongeza kuwa huduma ya uimbaji waithamini kama huduma zingine pia kutofanya kama sehemu ya kupatia kipato.

Amependa kuwaarika watu kusikiliza kazi zake alizoanza nazo sasa kwani zina ujumbe mzuri kwa ajili ya watu wote “naipenda huduma yangu na naithamini lakini pia napenda  kuwa mfano mzuri katika huduma,kitabia,kusema lakini pia hata
kutembea kwangu”alisema  Farida… Read More

0 comments:

Sunday, 14 December 2014

MBEYA
 
Wadau mbali mbali wa Elimu Nchini wametakiwa kuwekeza zaidi katika Elimu ili kusaidia  kuboresha kiwango cha taaluma  nchini kwa kuchangia misaada mbalimbali katika secta hiyo
 
 
ndugu Steven Sikluzwe akizungumza katika harambee hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa bodi ya shule ya Amani Day care Steven Sikaluzwe  wakati akizungumza kwa niaba  ya  mgeni rasimi  Askofu wa kanisa la pentecoste victory mission Alex Fella  katika harambee ya kuchangi ujenzi wa shule  ya watoto  wa chekechea Amani Day Cear  iliyofanyika Nanenane kwenye jengo la tanapa.
 
   Amesema kuwa katika kuinu  kiwango cha elimu na taaluma  wadau wa elimu wanatakiwa kuwekeza zaidi  kwenye  Elimu kuliko kuwekeza kwenye vitu vingine ambavyo  havina manufaa yeyote katika jamii.
 
   Aidha ameongeza kuwa  jamii ikiwekeza kwenye Elimu  itasaidia kupata  wasomi na wataalamu mbalimbli ambao watakuwa msaada mkubwa  katika jamii na Taifa kwa ujumula.
 
   Hata hivyo  Sikaluzwe amedai kuwa serikali haina budi kutoa kipao mbele kwa shule za binafisi ya kwa kutoa usajilibila kipingamizi kwa shule zilizotimiza vigezo, kwani zimekuwa msaada mkubwa  wa kutoa  Elimu kwa jamii.
 
Kwa upande wake  Mkurugenzi wa  shule hiyo Amos Steward   amewataka wazazi kuwa makini  wanapowapeleka wa toto wao kuanza masomo kufuatia kuanzishwa kwa shule nyingi  zisizo sajiliwa ili kuepuka kutapeliwa.
Read More

0 comments:

Saturday, 13 December 2014

Turn off for: Swahili
Inline image 2
Mtumishi wa mungu calvin Nyorobi akiwaanaimba wakati wa uzinduzi wa albam yake mjini Tunduma    Muimbaji wa nyimbo za injili na mtangazaji wa mtangazaji wa kituo cha radio kiitwacho Ushind Fm  Radio, Calvin Nyorobi atikisa mji wa Tunduma mkoani mbeya Jumapili ya tarehe 7-12-2014 wakati alipokuwa akizindua albam yake ya kwanza ijulikanayo kwa jina la USIKATE TAMAA.

    Muimbaji huyo aliyefanya tamasha hilo katika ukumbi wa kanisa la Tanzania Asemblies of God(TAG)Tunduma kwa Askofu Kalinga  ambapo watu wengi walihudhulia tamasha hilo la aina yake katika mji  huo na kumuona mungu kwa namna ya ajabu

Inline image 1
Askofu Kalinga wa kanisa la TAG Tunduma akiwa katika tamasha hilo mara baada ya kuzindua rasmi

    waimbaji mbalimbali pamoja na kwaya mbalimbali walihudhuli tamasha hilo   na kutoa michango kwa ajili ya kumtia moyo muimbaji huyo akiwemo Tumaini Mbembela(mke wake),Sara Mwanginde,Hawa Lusekelo,Peter Mbuba, Gwakisa Mwakilema,Tedy na kwaya mbalimbali zilikuwepo kuhakikisha tamasha linapendeza na kuvutia.
    waimbaji mbalimbali pamoja na kwaya mbalimbali walihudhuli tamasha hilo   na kutoa michango kwa ajili ya kumtia moyo muimbaji huyo akiwemo Tumaini Mbembela(mke wake),Sara Mwanginde,Hawa Lusekelo,Peter Mbuba, Gwakisa Mwakilema,Tedy na kwaya mbalimbali zilikuwepo kuhakikisha tamasha linapendeza na kuvutia.
    Muimbaji huyo ambaye pia amekuwa akija kwa kasi katika tasnia ya habari amedai kuwa kumtumikia mungu kwa nanmna ya uimbaji ni tamaa ya  yake siku nyingi kwani anaamini katika kutumika pia ndiko ziko Baraka za mungu "kutumika ndko kunafanya mtu apokee mshahara wake hivyo katika kutumika kuna nguvu ya ajabu ndiyo sababu inayo nifanya niwe natamani kmtumikia mungu siku zote" alisema

    wageni waalikwa wote waliweza kuonesha uwezo wao kufanya kila linalowezekana kuhudhulia tamasha hilo pamoja na changamoto za hali ya hewa  lakini bado wali weza kuwa na subira ya kumuona mtumishi wa mungu huyo kwani walizoea kumsikia katika radio tu na siyo kuonana naye ana kwa ana na tamasha lijawa n nguvu ya mungu na watu walimuona mungu aliye hai katika mji wa tunduma
Read More

0 comments:

Saturday, 15 November 2014

JEM GOSPEL MINISTRY KIUWINJILIST ZAIDI TUNA MUONA MUNGU
Timu nzima ya Huduma ya Jem haikupata shida pindi kukiwa na mgawo wa maji kwa ukanda wa Tukuyu kwani bado vijana wa Yesu hawakujali umbali wa kuyafuata maji
 si hivyo tu fuatana nami
hao vijana wako kuchuma chai
Hata kwenye kilimo vijana hawakubaki nyuma katika kuiosaidia jamii
Baada ya kazi za kijamii muda wa ibada ulipofika tunarudi kumtukuza MUNGU
                      Habari ya ndiyo hiyo Tumwabudu Mungu katika Roho na kweli
Baada ya sifa Mtumishi wa Mungu Apostle Jeremiah alianza kufundisha Neno la Mungu lenye kuleta uponyaji kwa watu kuhusu kufunguliwa katika laana

Read More

0 comments:

THE WORD OF TO DAY


Read More

0 comments:

Thursday, 13 November 2014

MUNGU ALITENDA ANATENDA NA ATATENDA MVUA ZA BARAKA KWA WATU
Dalili za mvua ya baraka kunyesha ni kubwa sana.
Ni katiak semina kubwa ya Neno la Mungu inayaoendelea Kyimbila Tukuyu ambapo mkufunzi wa semina hiyo Apostle Jeremiah Mwakanyelenge anafundisha na kuombea watu wenye shida mbalimbali
Apostle Jeremiah Mwakanyelenge akifundisha mamia ya watu wanao hudhuria semiana inayoendelea Kyimbila Moravian
Fuatilia matukio haya katika picha
kwaya ya wenyeji wakimsifu Mungu
mama ambaye alikuwa hawezi kutembea bila kutukia fimbo lakini baada ya kufanyiwa maobezi mama akiwa na furaha iliyoje huku akionesha fimbo yake juu sasa mateso basi tena Mungu huyu
Semina hii imebeba kichwa cha somo Tengeneza madhabahu ili mvua ya baraka inyeshe. kadri semina inavyo zidi kuendelea na leo ikiwa ni siku 4 tangu semina kuanza hakika tunaona wingu zito la mvua za baraka limetanda kuashiria kunyesha kwa mvua za baraka hata kabla siku 8 hajaisha
hakika tuna muona Mungu akitenda mambo makubwa mmno miujiza inatendeka hakika Mungu ni mwema sana kwetu
Katika kufafanua somo hilo Apostle Jeremieah ameainisha maana saba za namna ya kuitengeneza madhabahu ambapo mamia ya watu wanaohudhuria semina hii wamejikuta wakifunguliwa macho yao na kuona kumbe wamejitengenezea madhabahu zingine nje ya madhabahu yenye uhusiano na Mungu na ndiyo maana watu hujikuta wakishindwa kubarikiwa  na kujikuta wakikalia laana
Waweza jiuliza maswali kuwa mvua za baraka ni zipi hizo tena. Ni mafanikio ya Rohoni na mwilini ambayo ni haki yetu kupata toka kwa Bwana maana tuwarithi wa ufalme wake. ikwa ni pamoja na amani, furaha, afya , mali
tutaendelea kukujuza kinachoendelea ama zaidi sana tafuta DVD za semina hii na nyingine nyingi
uliza hapa 0754637974 Read More

0 comments:

Wednesday, 12 November 2014

Wakati wa sifa watu hujitoa kumsifu Mungu waimbaji wakimsifu Mungu
Mtumishi wa Mungu Apostle Jeremiah Mwakanyelenge akiwa madhabahuni Kyimbila
waimbaji wakimshambulia ibilisi jukwaa toka kushoto Sara Mwanginde Scola Mwezimpya Rehema Noah Farida Efesi Neema Bukuku Moses Simkoko
Kwa Yesu ni raha upendo furaha amani kila mmoja alitumia kifaa chake kuchukua matukio
Huduma ya JEM GOSPEL MINISTRIES inayoongozwa na mtumishi wa Mungu Apostle Jeremiah Mwakanyelenge wanaendesha msako mkali wa kusambaratisha ngome ya shetani na malaika zake 
katika semina kubwa na yenye upako wa Mungu katika viwanja vya kanisa la Moravian ushirika wa Kyimbila 
Katika semina hiyo Mtumishi wa Mungu Apostle Jeremiah akifundisha soma Kutengeneza madhabahu akimaanisha eneo la kukutana na Mungu si mimbara bali eneo ambalo mtu atakutana na Mungu na kuwekeana agano na Mungu akifafanua zaidi kuwa sasa kuna marumbano na mafarakano hata nadani ya kanisa kwasababu madhabahu nyingi zimeharibika na zinatoa uvundo na uozo badala ya manukato mazuri ambayo nia m,aombi ya watakatifu 
jambio la msingi ni kwa waumini kujitambua kuwa wao ni hekaru la Mungu na kuwa watumishi wajenge utumishi wao kwa kumtegemea Roho Mtakatifu na si nguvu nyingine
Katika semina hii tunaona Mungu akiokoa na kuwafungua watu waliofungwa na shetani, kuna idadi kubwa ya watu walioamuakubadilisha maisha yao na kumpa Yesu maisha yao 
Read More

0 comments:

BONYEZA HAPA KUSIKIA MAHUBIRI YA APOSTLE JEREMIAH MWAKANYELENGE

Read More

0 comments:

Thursday, 6 November 2014

MATUKIO MBALI MBALI YANAYOTOKEA KATIKA MKUTANO WA INJILI YA NENO LA MUNGU UNAOENDELEA KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA FPTC- MWAKIBETE MBEYA UKIONGOZWA NA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU TEOFILO KISANJI(TEKU)
WATU WOTE MNAKARIBISHWA, WAGONJWA WATAOMBEWA BURE KABISA
MKUTANO UNAENDELEA  HADI TAREHE 09-11-2014 KUANZIA SAA 9:00 HADI SAA 12 :00 JIONI NA KUANZIA SAA 1:30 JIONI HADI SAA 3:30 USIKU Mchungaji mwenyeji ni S.KIAMBA

Wahubiri ni 
  1. ADAM MSIGWA (BAED)
  2. NEEMA ELISHA(BEDPSY)
  3. ELISHA KAZIMOTO
  4. ASIMESYE FADHILI(BAED)
    Watumishi waliosimama madhabahani hapo wote ni wanafunzi wa Chuo kikuu TEKU.
    WAKATI WA MAOMBEZI KWA WATU WENYE SHIDA MBALIMBALI.
Read More

0 comments:

Wednesday, 5 November 2014

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya darasa la Saba mwaka 2014 ambayo yameonyesha ongezeko la ufaulu wa asilimia 56.99 tofauti na ufaulu wa mwaka jana wa asilimia 51.6

Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es salaam leo Novemba 5, 2014 Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania, Dk.Charles Msonde, ametaja jumla ya wanafunzi waliojisajili kufanya mitihani kufikia 792,118 sawa na asilmia 98.2 na jumla ya watahiniwa 451 wamepata alama 100 au zaidi huku mkoa wa Dar es salaam ukiogoza.
Read More

0 comments:

Tuesday, 4 November 2014


Read More

0 comments:

WANAFUNZI WA SHULE MBALIMBALI WAKIWA KATIKA MAZINGIRA YA MTIHANI

baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye chumba cha mtihani


wanafunzi wakiwa katika kujisomea mara baada ya mitihani yao



SIKU YA KWANZA INAKUWA INAISHA KWA NAMNA HIYO ,OMBEA WANAFUNZI HAWA.


Read More

0 comments:

Recent News