KWA TAARIFA YAKO : HII NDIO SIRI YA SOLO MAARUFU WA KINONDONI REVIVAL CHOIR
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO''
ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la
kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia
yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au
kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka
comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
"Kwaniniii wataka kujiua wewe? kwaninii huna hamu ya kuishi? elimu unayo lakini huna amani, dini yako nzuriii lakini huna amani" haya ni baadhi ya maneno ya moja ya wimbo maarufu wa kwaya ya Kinondoni Revival kutoka Assemblies of God Kinondoni kwa Askofu Rogathe Swai. KWA TAARIFA YAKO hii leo ni kukujuza kuhusu mwimbaji solo wa muda mrefu wa kwaya hiyo ambaye uimbaji wake umekuwa kama kitambulisho cha kwaya hiyo popote aendapo. Huyu si mwingine bali ni mwanadada Rebecca Nzelwa Lukule ambaye kwasasa ni mke wa mtu.
KWA TAARIFA YAKO Rebecca ameimba nyimbo nyingi sana na kwaya ya Revival kati ya nyimbo hizo ni pamoja, Twaililia Tanzania ambao ndio uliomtambulisha vyema kwenye huduma ya uimbaji na ndio wimbo wake wa kwanza kuutengenezea solo (walipewa ruhusa na mwalimu wao kila mwimbaji atengeneze solo ya kujazia wimbo huo ) ambayo ilipitishwa na mwalimu wa kwaya kwamba aimbe kama alivyotengeneza. KWA TAARIFA YAKO Rebecca ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa kwaya ya Revival toka amejiunga nayo mwaka 1993 wakati huo kwaya nyingine ya kanisani hapo iitwayo Victory Singers walikuwa wakivuma haswa katika muziki wa injili.
KWA TAARIFA YAKO Rebecca aliendelea kuvumisha injili kupitia nyimbo zilizopata umaarufu kama 'Vumilia Samweli atazaliwa' na Mtu wa nne nyimbo ambazo Mungu ametenda makuu kwa watu wake na shuhuda nyingi kuwafikia wanakwaya hao "wako watu ambao hawakuwa na watoto lakini Mungu amewapa watoto, Wako ambao wamekuwa wakipitia mambo magumu lakini Mungu amewatetea na mambo mengi zaidi ya hayo" Rebecca ameiambia GK. KWA TAARIFA YAKO kujishusha kwake na uimbaji wake hodari Rebecca alichaguliwa na waimbaji wenzake kuwa mwalimu msaidizi wa kwaya akishirikiana na kupewa msaada na mwalimu mkuu wa kwaya kutengeneza nyimbo.
KWA TAARIFA YAKO kama hujui Rebecca ameichukulia umakini huduma
ya uimbaji kwakuhakikisha anasimama imara katika maombi kuiombea huduma
ya kwaya yake na yeye binafsi KWA TAARIFA YAKO kama hujui Rebecca
kwasasa amehama kimakazi yupo jijini Arusha na mumewe ambaye Rebecca
anasema anampa sapoti kubwa katika huduma yake ya uimbaji hata sasa
wanaabudu katika kanisa la Assemblies Bethel Christian Centre kwa askofu
Oral Sossy "Bado naendelea kumtumikia Mungu, na mwaka huu nimeamua
kumtumikia Mungu na kwaya ya inayoitwa Bethany ambapo nimeweza kuimba
nao wimbo unaoitwa "Mungu wetu hachoki" na tayari kwaya imetoa DVD yao
inayoitwa "Wewe ni Mungu wa kweli"
kila asimamapo kuhudumu ili Mungu akapate kusema na watu wake, na
matokeo yake yameonekana kupitia shuhuda hizo ambazo zimekuwa
zikiwafikia kutoka kwa watu ambao wamepata nafasi ya kuhudumiwa na kwaya
hiyo.
KWA TAARIFA YAKO Mimi binafsi pia bado naendelea kufanya huduma
mbalimbali nimeendelea kupata mialiko ya kuimba ndani na nje ya nchi na
nina watu ambao tumeamua kujiunga pamoja ili kufanya huduma hii.
Tunatembelea watoto yatima kuwafariji na kuwahudumia, tunatembelea
watoto wa mitaani na kubadilisha mwelekeo wa maisha yao na tunaendelea
kujifunza kuimba na kutembea na Mungu na kumcha Mungu" Wiki ya pasaka
nilialikwa Nairobi Easleigh kuhudumu kwenye kongamano la wachungaji na
watumishi mbalimbali wa Mungu. Hii inanipa kusonga mbele kwenye utumishi
na hata maisha ya kiroho kuwa bora zaidi" Rebecca ameiambia GK.
KWA TAARIFA YAKO kama hujui siri ya mafanikio ya Rebecca kupendwa
na wengi katika huduma yake ya uimbaji, ni kwamba kuna mengi ayafanyayo
ukiacha mazoezi ya uimbaji lakini pia ametabanaisha siri yake kupitia
GK kwamba "Naendelea kujifunza kutoka kwa Mungu, nataka uimbaji KWA TAARIFA YAKO hiyo ndiyo siri inayomfanya Rebecca kuwabariki wengi kila asimamapo madhabahuni kumtumikia Kristo.
unaobadilisha maisha ya watu, nataka uimbaji wenye mguso, hii
inawezekana hivyo nimeamua kuishi na kutembea na Mungu ili nimsikie
kiumakini anataka nini kwenye maisha yangu na kwenye utumishi huu.
Ninachokiimba nimaanishe, maisha ninayoishi nje ya madhabahu yawe ni
kama ninaposimama madhabahuni".
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo….



%2B(1).png)
0 comments: