Mtumishi wa mungu na mkurugenzi JP & E Company Jeremiah Mwakanyelenge amewataka watu wote kutembea na kuishi katika kweli ya Kristo hasa wakati wa kipindi hiki cha christmas na mwaka mpya. Maneno hayo ameyasema jana katika semina ya wanahuduma wa JEM GOSPEL MINISTRY yenye makao makuu jijini Mbeya na watenda kazi wa Jp & E Company.
Mtumishi huyu ambaye anamtumikia Mungu katika kufundisha na kuhubiri duniani kote amenukuliwa akiwaasa wanahuduma ya JEM na jamii kwa ujumla wasifanye maandalizi yaliyotofauti na mapenzi ya Mungu katika kusherekea sikukuu za mwaka mpya na krismas, bali wawezefanya mambo yanayo ugusa moyo wa Kristo kwa kuyaenzi matendo mema ya kumpendeza Kristo na jamii kwa ujumla.
Alisisitiza kwa
kusema dunia ni ileile ya tangu uumbaji,
lakini matendo ya wanadamu wanaobadirika fahamu zao kila siku yanasababisha
dunia ya leo ionekene ni mpya na iliyojaa maovu mengi kuliko mema maana siku za
skukuu kama hizi wengi hupoteza maisha na wengine hupoteza baadhi ya viungo
vyao kwa kupigwa ambapo tayari amani na raha ya kuazimisha kuzaliwa kwa Yesu
inapotea.
Alihitimisha
kwa kuwakaribisha watu wote katika ibada za ya JEM GOSPEL MINISTRY kila siku ya
jumatano na jumapili jioni eneo la Soweto block Q .Pia aliwakaribisha watu waje
JP PRODUCTION kwa kurekod audio,video,kudurufu CD,kukodi vyombo vya mziki na
gari ya matangazo kwa gharama nafuu.

%2B(1).png)
0 comments: