Kushoto
ni Padri Kassase akiwa na mkuu wa chuo cha Mlimani School of
Professional Students, Hassani Ngoma katika makabidhiano ya hati ya
udhamini wa wanafunzi .
Viongozi na wawakilishi wa dini ya Kikristo na Kislamu wakiwa katika majadiliano kabla ya mkutano kuanza.
Mkuu wa chuo cha Mlimani Hassani Ngoma akisikiliza maswali kutoka kwa viongozi wa dini (hawapo pichani).
Mkuu
wa chuo cha Mlimani School of Profession Students, Hassan Ngoma
akikabidhi hati ya udhamini kwa wanafunzi 20 kutoka taasisi za dini ya
Kiislam na Kikristo.
Viongozi
na wawakilishi wa dini ya Kiislam wakiwa na bahasha zenye fomu ya
udhamini walizopewa na chuo cha mlimani School of Profession Students.
Wanafunzi wakiwa wanajisomea eneo la chuo.
Wawakilishi
wa dini ya Kikristo na Kiislam zinazozunguka chuo cha Mlimani School of
Profession Students, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo
hicho.
Baadhi ya waumini na viongozi wa dini ya Kiislamu wakibadilishana mawazo nje ya jengo la chuo cha Mlimani, Mbezi kwa Msuguri.
CHUO
cha Mlimani School of Profession Students cha Mbezi kwa Msuguri, jijini
Dar es Salaam, kimetoa hati za udhamini kwa wanafunzi wasiojiweza
wapatao 20, kutoka taasisi za kidini za Kiislam na Kikristo kwa makanisa
ya kata tano zinazozunguka chuo hicho.
Kata hizo ni Msigani, Kimara, Saranga, Mbezi na Kwembe zilizopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wetu mkuu wa chuo Hassan Ngoma, ameitaka jamii kujitokeza ili kutumia fursa waliyotoa kwa watu waliofeli na wale wenye kipato kidogo kuweza kuwasomesha watoto wao kwa kulipa kiwango kidogo cha fedha kulingana na uwezo wa wazazi ama mlezi wao.
Akizungumza na mwandishi wetu mkuu wa chuo Hassan Ngoma, ameitaka jamii kujitokeza ili kutumia fursa waliyotoa kwa watu waliofeli na wale wenye kipato kidogo kuweza kuwasomesha watoto wao kwa kulipa kiwango kidogo cha fedha kulingana na uwezo wa wazazi ama mlezi wao.
‘’Tumejikita
katika kutoa huduma kwa jamii kwa kutoa udhamini wa wanafunzi 20
wasiojiweza, lengo likiwa ni kurudisha fadhila za chuo chetu kuwepo eneo
la Mbezi kwa miaka 5,” alisema mkuu wa Chuo hicho.

%2B(1).png)
0 comments: