Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Monday, 18 August 2014

Unknown / / 0


Mmoja wa wanaume waliovamia kituo hicho na kumbeba mgonjwa
Waziri wa habari wa Liberia Lewis Brown amesema kuwa wagonjwa 17 kati ya 37 waliokuwa katika zahanati iliyokuwa ikitumika kama kituo cha kuwatenga wagonjwa wa Ebola hawajulikani waliko.
Waasiriwa hao wa Ebola walikuwa wametengwa katika kituo hicho kilichoko karibu na kitongoji cha WestPoint Viungani mwa mji mkuu wa Monrovia kabla ya wenyeji kukivamia na kuwaachilia huru wagonjwa waliokuwemo na kukipora.
'' tukio hilo la WestPoint ni la kuvunja moyo sana maanake inahujumu juhudi zetu zote za kuzuia kuenea kwa homa hii ya Ebola,natumai tutarekebisha hali hii'' alisema bwana Brown.
20 waliosalia wako katika zahanati mbalimbali karibu na mji mkuu Monrovia .
Zahanati moja inaendeshwa na Hospitali kuu ya John F. Kennedy ilihali wengine wako katika zahanati ya ELWA nje ya mji huo.
Wote hao watachunguzwa kabla ya hatua madhubuti kuchukuliwa kwa maslahi ya Umma.
Katika hatua ya kushtua sana wakaazi wa vitongoji vya mji wa Monrovia walivamia zahanati hiyo iliyokuwa ikitumika kama kituo cha kuwatenga wagonjwa wa homa ya Ebola wakaipora na kuwaruhusu wagonjwa kutoroka.
''Kwa sasa tunashughulikia hali hii ilivyo kwani watu sasa wamerejea miongoni mwa jamii na hivyo kueneza maambukizi zaidi''
Zaidi ya watu 17 bado hawajulikani waliko baada ya kutoroka kutoka kituo cha kuwatenga wagonjwa wa Ebola.
''Kufuatia uvamizi huo tumejifunza mengi ''
Ajabu ni kuwa watu walikuja ndani ya kituo hicho walijileta huko wenyewe kwa hivyo sisi tunachukulia kuwa labda wagonjwa hao walitaka kusalia huko lakini wakalazimishwa kutoroka kukimbilia maisha yao kwa sababu wavamizi walikuwa wanapora mali ya Westpoint.
Brown alisema kuwa kwa sasa zahanati hiyo ya Westpoint Imefungwa lakini kuna mipango ya kuifungua tena.
''Tunafahamu kuwa kuna watu ambao bado wanashauku iwapo Ebola ipo ama hakuna lakini ukitizama takwimu kutoka jimbo la Lofa utaona kuwa idadi ya wahasiriwa imeanza kupungua.''
Lofa ndiyo iliyokuwa kitovu cha mlipuko ulioko sasa wa homa hii ya Ebola.
Zaidi ya watu 17 bado hawajulikani waliko baada ya kutoroka kutoka kituo cha kuwatenga wagonjwa wa Ebola.
Taharuki ilitanda kote nchini humo ,baada ya kituo kilichotengwa na kuwekewa kwa sababu ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola, kilishambuliwa na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu 37 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za Ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku.
Washambuliaji walipora magodoro na vitu vingine.
Mwandishi wa BBC katika kanda hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.
Mafisa wakuu nchini Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.

 

MWANAFUNZI WA TANZANIA ATWAA TUZO YA INSHA NCHI ZA SADC

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha nne Neema Steven Mtwanga (16) anayesoma katika Shule ya Sekondari Naboti Makambako, Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa insha katika shindano lililoandaliwa na Jumuiya ya uchumi ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC).…
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha nne Neema Steven Mtwanga (16) anayesoma katika Shule ya Sekondari Naboti Makambako, Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa insha katika shindano lililoandaliwa na Jumuiya ya uchumi ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC). Rais Kikwete alimpongeza mwanafunzi huyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe ambapo mwanafunzi huyo aliandika insha inayohusu mabadiliko ya tabia nchi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa jumuiya hiyo uliofanyika katika hoteli ya Elephant Hills mjini Victoria Falls Zimbabwe leo. Katikati ni mwenyeji wa Mkutano huo Rais Robert Mugabe na Dkt Stergomena Tax (katibu mkuu wa SADC) na kwa upande wake wa kushoto ni Nkosazana Dlamini-Zuma (Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika)
MTOTO wa Kitanzania, msichana Neema Steven Mtwanga, ameibuka kinara katika Mashindano ya Utunzi wa Insha katika nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa kushika nafasi ya kwanza miongoni mwa washindani 39 waliowania Tuzo ya Utunzi wa Insha hiyo kwa Mwaka 2014.
Msichana Neema Steven Mtwanga, 16, kutoka Shule ya Sekondari ya Naboti, Mkoa wa Njombe, ametunukiwa Tuzo ya ushindi huo katika Mkutano wa 34 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC ulioanza leo katika Hoteli ya Elephant Hills Resort, Victoria Falls, Zimbabwe.
Nafasi ya pili imeshikwa na Kudzai Ncube kutoka Shule ya Sekondari ya Mazowe nchini Zimbabwe na nafasi ya tatu imeshikwa na Manxoba Msibi kutoka Shule ya Sekondari ya Etjendlovu katika Swaziland.
Kwa ushindi huo, Neema Steven Mtwanga ambaye yuko kidato cha nne, amezawadiwa hundi ya dola za Marekani 1500 ambayo ni sawa na shilingi milioni 2.3 na amelipiwa gharama zote za kumwezesha kushiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC na kukabidhiwa zawadi hiyo. Aidha, Neema amepewa zawadi ya ipad kwa ajili ya matumizi yake ya teknolojia ya mawasiliano na habari.
Mashindano hayo ya Insha ya Mwaka 2014 yalianzishwa rasmi Oktoba, 2013 ambako washindani walitakiwa kuandika Insha kuhusu mada: “Climate Change is having adverse effect on the socio-economic development in the Region. What should the Education Sector do to mitigate the impact on the youth” – Mabadiliko ya Tabia Nchi yanaathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Kanda ya SADC. Nini Sekta ya Elimu ifanye kupunguza athari hizo kwa vijana?
Insha 39 zilipokelewa kutoka nchi 13 kati ya nchi 15 wanachama wa SADC ikiwa ni Insha tatu kwa kila nchi. Insha zilipokelewa kutoka Tanzania, Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Lesotho, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
Majaji wa kupitia na kuamua washindi wa Insha hizo walitoka Tanzania, Zambia na Zimbabwe na walikutana mjini Gaborone, Botswana, Julai, mwaka huu kupitia Insha zote na kutoa uamuzi wa nani washindi.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo wa SADC umepokea kwa furaha ushindi wa msichana Neema ukieleza kuwa ushindi huo umeiletea Tanzania heshima kubwa katika eneo la SADC na nje ya eneo hilo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
17 Agosti,2014

Unknown


Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit. Ut odio. Nam sed est. Nam a risus et est iaculis adipiscing. Vestibulum ante ipsum faucibus luctus et ultrices.
Follow me @Bloggertheme9

0 comments:

Recent News