Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Tuesday, 19 August 2014

Unknown / / 0
Stori: Haruni Sanchawa
“Mwanangu ana kichwa kikubwa lakini simtupi,” yalikuwa ni maneno ya kuhuzunisha ya mama wa mtoto Laurent Marykion ambaye amezaliwa miezi saba iliyopita katika mji mdogo wa  Mikumi mkoani Morogoro na   anateseka kutokana na tatizo la kuvimba kichwa.
Mtoto Laurent Marykion akiwa amelala.
“Baada ya kuzaliwa na kufikisha miezi mitatu, alipatwa  na tatizo hili la kuvimba kichwa  ambacho kinajaa maji,” alisema mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Devota Bogasti.
MAMA AIITA HALI HIYO NI JANGA
Alisema mtoto huyo ni wa  nne kuzaliwa, kati ya watoto wake huyo ameonyesha hali ya tofauti ya kukumbwa na kitu alichokiita kuwa ni janga.
Aliongeza kusema kuwa, Laurent alizaliwa katika Hospitali ya Mikumi mjini Morogoro akiwa na afya nzuri  lakini baada ya miezi mitatu  alianza kuvimba kichwa bila  kujua chanzo chake kilikuwa nini!
“Baada ya kujitokeza hali hiyo, hatukuwa na namna ya kufanya kutokana mimi na mume wangu kuwa na hali  mbaya kiuchumi, tulidhani mtoto wetu angeweza kupona mwenyewe.”
Devota akimwinua mwanaye Laurent aliyekuwa akilia.
Akifafanua zaidi mbele ya mwandishi wetu katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi), Muhimbili Wodi A alikolazwa na mwanaye huku akitokwa machozi, Devota alisema hajui hatima ya mtoto wake kuhusu kupona kwake.”
HALI ILIPOKUWA MBAYA
“Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya tulianza kutafuta namna ya kufanya ikiwa ni pamoja na kwenda katika Hospitali ya Mikumi iliyopo mkoani Morogoro kwa ajili ya kutafuta tiba lakini hakukuwa na matumaini ya kupata matibabu kama tulivyotarajia.
“Uongozi wa Hospitali ya Mikumi ulituambia kwa kuwa tatizo la mtoto  wetu lilikuwa kubwa ni lazima tumlete hapa Moi kwa uchunguzi zaidi.”
WAKIWA MOI MAMBO YALIKUWAJE?
 “Juni 4, mwaka huu tulifika Moi,  pamoja na kupokelewa vizuri na uongozi lakini bado tunahitaji msaada wa pesa kwa ajili ya kumsaidia mwanangu ikiwa ni pamoja na kupata lishe bora.
Devota akiwa amempakata mwanaye Laurent.
“Mimi na mume wangu hatuna uwezo wa kifedha. Sisi ni wakulima tunaotumia jembe la mkono na mwaka huu sikuweza kulima kutokana na kuhangaikia matibabu ya mwanangu.
“Ninawaomba Watanzania, yeyote mwenye moyo wa huruma anisadie ili niweze kunusuru maisha ya mwanangu anayeteseka kutokana na tatizo linalomkabili,” alisema Devota huku akifuta machozi kwa kutumia khanga yake.
MOI WANENA JAMBO
Kwa upande wake Msemaji wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa  ya Fahamu, Almasi Jumaa alisema taratibu za kumtibu  mtoto huyo zinafanyika.
“Mtoto huyu anafanyiwa utaratibu wa matibabu na Mungu akijaalia wiki ijayo (wiki hii), madaktari wanaweza kumfanyia upasuaji wa kichwa,” alisema Almasi.
Aidha, aliongeza kuwa hali kama  hiyo huwakumba baadhi ya watoto  na ni tatizo la kisayansi zaidi lakini akifanyiwa upasuaji hali yake itarudi kuwa ya kawaida maana kuna waliomtangulia walikuwa kama yeye lakini sasa hali zao zimekuwa nzuri.
Kwa yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kuwasiliana na mama  huyo kupitia namba ya simu 0713 643601 au 0757 843155 ambazo ni za ndugu yake wa karibu au kwa kwenda kumuona Muhimbili.
CHANZO CHA HABARI www.globalpublishers.info

Unknown


Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit. Ut odio. Nam sed est. Nam a risus et est iaculis adipiscing. Vestibulum ante ipsum faucibus luctus et ultrices.
Follow me @Bloggertheme9

0 comments:

Recent News