Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Saturday, 15 November 2014

JEM GOSPEL MINISTRY KIUWINJILIST ZAIDI TUNA MUONA MUNGU
Timu nzima ya Huduma ya Jem haikupata shida pindi kukiwa na mgawo wa maji kwa ukanda wa Tukuyu kwani bado vijana wa Yesu hawakujali umbali wa kuyafuata maji
 si hivyo tu fuatana nami
hao vijana wako kuchuma chai
Hata kwenye kilimo vijana hawakubaki nyuma katika kuiosaidia jamii
Baada ya kazi za kijamii muda wa ibada ulipofika tunarudi kumtukuza MUNGU
                      Habari ya ndiyo hiyo Tumwabudu Mungu katika Roho na kweli
Baada ya sifa Mtumishi wa Mungu Apostle Jeremiah alianza kufundisha Neno la Mungu lenye kuleta uponyaji kwa watu kuhusu kufunguliwa katika laana

Read More

0 comments:

THE WORD OF TO DAY


Read More

0 comments:

Thursday, 13 November 2014

MUNGU ALITENDA ANATENDA NA ATATENDA MVUA ZA BARAKA KWA WATU
Dalili za mvua ya baraka kunyesha ni kubwa sana.
Ni katiak semina kubwa ya Neno la Mungu inayaoendelea Kyimbila Tukuyu ambapo mkufunzi wa semina hiyo Apostle Jeremiah Mwakanyelenge anafundisha na kuombea watu wenye shida mbalimbali
Apostle Jeremiah Mwakanyelenge akifundisha mamia ya watu wanao hudhuria semiana inayoendelea Kyimbila Moravian
Fuatilia matukio haya katika picha
kwaya ya wenyeji wakimsifu Mungu
mama ambaye alikuwa hawezi kutembea bila kutukia fimbo lakini baada ya kufanyiwa maobezi mama akiwa na furaha iliyoje huku akionesha fimbo yake juu sasa mateso basi tena Mungu huyu
Semina hii imebeba kichwa cha somo Tengeneza madhabahu ili mvua ya baraka inyeshe. kadri semina inavyo zidi kuendelea na leo ikiwa ni siku 4 tangu semina kuanza hakika tunaona wingu zito la mvua za baraka limetanda kuashiria kunyesha kwa mvua za baraka hata kabla siku 8 hajaisha
hakika tuna muona Mungu akitenda mambo makubwa mmno miujiza inatendeka hakika Mungu ni mwema sana kwetu
Katika kufafanua somo hilo Apostle Jeremieah ameainisha maana saba za namna ya kuitengeneza madhabahu ambapo mamia ya watu wanaohudhuria semina hii wamejikuta wakifunguliwa macho yao na kuona kumbe wamejitengenezea madhabahu zingine nje ya madhabahu yenye uhusiano na Mungu na ndiyo maana watu hujikuta wakishindwa kubarikiwa  na kujikuta wakikalia laana
Waweza jiuliza maswali kuwa mvua za baraka ni zipi hizo tena. Ni mafanikio ya Rohoni na mwilini ambayo ni haki yetu kupata toka kwa Bwana maana tuwarithi wa ufalme wake. ikwa ni pamoja na amani, furaha, afya , mali
tutaendelea kukujuza kinachoendelea ama zaidi sana tafuta DVD za semina hii na nyingine nyingi
uliza hapa 0754637974 Read More

0 comments:

Wednesday, 12 November 2014

Wakati wa sifa watu hujitoa kumsifu Mungu waimbaji wakimsifu Mungu
Mtumishi wa Mungu Apostle Jeremiah Mwakanyelenge akiwa madhabahuni Kyimbila
waimbaji wakimshambulia ibilisi jukwaa toka kushoto Sara Mwanginde Scola Mwezimpya Rehema Noah Farida Efesi Neema Bukuku Moses Simkoko
Kwa Yesu ni raha upendo furaha amani kila mmoja alitumia kifaa chake kuchukua matukio
Huduma ya JEM GOSPEL MINISTRIES inayoongozwa na mtumishi wa Mungu Apostle Jeremiah Mwakanyelenge wanaendesha msako mkali wa kusambaratisha ngome ya shetani na malaika zake 
katika semina kubwa na yenye upako wa Mungu katika viwanja vya kanisa la Moravian ushirika wa Kyimbila 
Katika semina hiyo Mtumishi wa Mungu Apostle Jeremiah akifundisha soma Kutengeneza madhabahu akimaanisha eneo la kukutana na Mungu si mimbara bali eneo ambalo mtu atakutana na Mungu na kuwekeana agano na Mungu akifafanua zaidi kuwa sasa kuna marumbano na mafarakano hata nadani ya kanisa kwasababu madhabahu nyingi zimeharibika na zinatoa uvundo na uozo badala ya manukato mazuri ambayo nia m,aombi ya watakatifu 
jambio la msingi ni kwa waumini kujitambua kuwa wao ni hekaru la Mungu na kuwa watumishi wajenge utumishi wao kwa kumtegemea Roho Mtakatifu na si nguvu nyingine
Katika semina hii tunaona Mungu akiokoa na kuwafungua watu waliofungwa na shetani, kuna idadi kubwa ya watu walioamuakubadilisha maisha yao na kumpa Yesu maisha yao 
Read More

0 comments:

BONYEZA HAPA KUSIKIA MAHUBIRI YA APOSTLE JEREMIAH MWAKANYELENGE

Read More

0 comments:

Thursday, 6 November 2014

MATUKIO MBALI MBALI YANAYOTOKEA KATIKA MKUTANO WA INJILI YA NENO LA MUNGU UNAOENDELEA KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA FPTC- MWAKIBETE MBEYA UKIONGOZWA NA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU TEOFILO KISANJI(TEKU)
WATU WOTE MNAKARIBISHWA, WAGONJWA WATAOMBEWA BURE KABISA
MKUTANO UNAENDELEA  HADI TAREHE 09-11-2014 KUANZIA SAA 9:00 HADI SAA 12 :00 JIONI NA KUANZIA SAA 1:30 JIONI HADI SAA 3:30 USIKU Mchungaji mwenyeji ni S.KIAMBA

Wahubiri ni 
  1. ADAM MSIGWA (BAED)
  2. NEEMA ELISHA(BEDPSY)
  3. ELISHA KAZIMOTO
  4. ASIMESYE FADHILI(BAED)
    Watumishi waliosimama madhabahani hapo wote ni wanafunzi wa Chuo kikuu TEKU.
    WAKATI WA MAOMBEZI KWA WATU WENYE SHIDA MBALIMBALI.
Read More

0 comments:

Wednesday, 5 November 2014

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya darasa la Saba mwaka 2014 ambayo yameonyesha ongezeko la ufaulu wa asilimia 56.99 tofauti na ufaulu wa mwaka jana wa asilimia 51.6

Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es salaam leo Novemba 5, 2014 Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania, Dk.Charles Msonde, ametaja jumla ya wanafunzi waliojisajili kufanya mitihani kufikia 792,118 sawa na asilmia 98.2 na jumla ya watahiniwa 451 wamepata alama 100 au zaidi huku mkoa wa Dar es salaam ukiogoza.
Read More

0 comments:

Tuesday, 4 November 2014


Read More

0 comments:

WANAFUNZI WA SHULE MBALIMBALI WAKIWA KATIKA MAZINGIRA YA MTIHANI

baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye chumba cha mtihani


wanafunzi wakiwa katika kujisomea mara baada ya mitihani yao



SIKU YA KWANZA INAKUWA INAISHA KWA NAMNA HIYO ,OMBEA WANAFUNZI HAWA.


Read More

0 comments:

Monday, 3 November 2014

 VURUGU zilizoambatana na ngumi kurushwa zimetokea jana katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba alipokuwa akitoa mada kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.
Vurugu hizo zimezuka baada ya watu waliokuwa na mabango kuvamia ukumbuni hapo na kusababisha baadhi ya watu waliokuwa wanafuatilia mdahalo huo kuwakabili na kuwapa kichapo.
Baada ya vurugu hizo, mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa moja kwa moja na ITV ulisimamishwa kwa muda. Read More

0 comments:

Sunday, 2 November 2014















Read More

0 comments:

Recent News