Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Wednesday, 28 May 2014

Unknown / / 0

MREMBO ANASWA NA NGUO ZA KUAMBIANA

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
AMA kweli duniani kuna sarakasi! Takribani siku kumi tangu alipofariki dunia aliyekuwa ‘kichwa’ kwenye filamu za Kibongo, Adam Phillip Kuambiana (38), mrembo aliyejitambulisha kwa jina Mary Njombe amenaswa na nguo za staa huyo wakati mali za marehemu hazijagawanywa.
Mary Njombe aliyenaswa akiwa amevaa nguo za marehemu Adam Phillip Kuambiana.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Mary ambaye ni mkazi wa Magomeni Hospitali, Dar amekuwa akipigilia pamba za marehemu hasa baada ya jamaa huyo kutangulia mbele ya haki.
“Jamani njooni huku Magomeni Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga nguo za marehemu Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walifanya msako eneo hilo hadi wakamnasa Mary.
Katika mahojiano na gazeti hili, Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa Kuambiana na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara ya mwisho amfulie (zinaonekana pichani).
Mary alisema kuwa yeye na Kuambiana walifahamiana tangu mwaka 2006 ambapo alikuwa akimbembeleza kuwa naye.
“Mwaka 2008 ndiyo tulianza rasmi uhusiano kwani mimi nilikuwa sina mwanaume na yeye hakuwa na mtu hivyo tulikubaliana na alikuwa akijulikana nyumbani kwetu,” alifunguka Mary.
Mwanadada huyo alisema kuwa yeye na Kuambiana walikuwa wakikutana kwenye Hoteli ya Grand iliyopo Magomeni, Dar na mara nyingi alikuwa akimpikia chakula na kumpelekea ‘lokesheni’.
“Nimeumia sana na sijielewi, Kuambiana ameniachia donda kubwa, nakumbuka neno la mwisho aliniambia nimpende sana kwani ipo siku nitamkubuka,” alisema Mary huku akiangua kilio.
Adam Phillip Kuambiana enzi za uhai wake akiwa amevaa shati alilonaswa nalo mrembo.
Alipoulizwa kama kweli nguo hizo ni za marehemu Kuambiana, alizama ndani akatoka akiwa amevaa pensi na shati la ‘drafti’ alilokuwa anapendelea kulivaa staa huyo ambalo ni maarufu sana.
Kuambiana alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 17, mwaka huu baada ya kuanguka chooni kutokana na kusumbuliwa vidonda vya tumbo.
Chanzo cha Habari: www.globalpublishers.info

 

BABA AMUUA KWA MAWE BINTIYE MJAMZITO KWA KOSA LA KUOLEWA NA ASIYEMTAKA

Mwili wa marehemu Farzana ukiwa chini pembeni yakiwa matofali yaliyotumika kumshambulia.

Wakati Meriam anasubiri kutekelezwa kwa adhabu yake kifungoni huko nchini Sudan, habari nyingine kutoka nchini Pakistan zinasema polisi nchini humo wamemkamata baba mmoja kwa kosa la kumuua binti yake wa kumzaa kwa mawe akishirikiana na familia nzima yenye jumla ya watu takribani 20 kwa kosa la binti yake kuolewa na mwanaume asiyetakiwa na familia.

Marehemu ametambulika kwa jina la Farzana Parveen (25) inadaiwa alikuwa mjamzito wa miezi mitatu wakati ambao kaka zake, baba yake na ndugu wengine walipowashambulia kwa mawe yeye na mumewe aitwaye Mohammad Iqbal (45) majira ya mchana mbele ya mahakama kuu ya mjini Lahore nchini humo.

Kwa mujibu wa mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu mkazi wa Pakistani aitwaye Zia Awan amesema hajawahi kusikia aina ya kesi kama ya Farzana kupigwa mawe hadi kifo, mbaya zaidi tukio hilo limefanyika mbele ya mahakama amesema Zia akizungumza na The Associated Press. Naye kwa upande wa baba mzazi wa marehemu Mohammad Azeem ambaye amemfungulia kesi mwanaume aliyefunga ndoa na binti yake bila ridhaa yake licha ya kwamba walikuwa wachumba kwa miaka kadhaa, ameonyesha kutojutia kitendo alichokifanya "Nimemuua binti yangu kwakuwa ameidhalilisha familia nzima kwakuolewa na mwanaume ambaye hakuwa na ridhaa yetu, sijutii kitendo nilichokifanya" amesema mzee Azeem.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa shirika la habari la AP linasema kumekuwa na vitendo vya adhabu za
Mume wa marehemu akiwa na mwili wa mkewe kwenye gari la wagonjwa.
kupigwa mawe katika taifa hilo la kiislamu la Pakistan kwasehemu kubwa kutokana na wanawake kutaka kuolewa kutokana na upendo ama mapenzi kwa ampendaye bali kwa kuchaguliwa mtu wa kuolewa naye jambo ambalo baadhi ya wanawake hawalitaki na kujikuta wakipoteza maisha namna hiyo.
Na katika kuonyesha kwamba vitendo hivyo haviwezi kuisha ni kutokana na adhabu nyepesi wanazopewa watu wanaokamatwa kwa kosa la kuua wenzao kwa kuwarushia mawe. Aidha Awan amesema linapotokea jambo kama hilo polisi hawafanyi uchunguzi kwa makini na kusababisha mahakama kutoa adhabu nyepesi kwa watuhumiwa.

Mapema mwezi wa April, wanandoa wa Kikristo nchini humo walihukumiwa kifo kwakosa la kuukashifu uislamu kwakupitia ujumbe wa simu za mkononi. Licha ya mwanasheria aliyekuwa akiwatetea wanandoa hao kwamba ujumbe huo haukutoka kwao kwakuwa hawajui kusoma wala kuandika lakini utetezi wake haukusikilizwa. Wakristo huishi katika matatizo mazito nchini Pakistani kwakufuatiliwa na polisi, kupelekwa vifungoni na wengine kuhukumiwa kifo.

 

MWANAMKE ALIYEHUKUMIWA KIFO SUDAN AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE GEREZANI

Meriam na mumewe Daniel siku ya ndoa yao.

Habari kutoka Khartoum nchini Sudan zinasema mwanadada Meriam Ibrahimu ambaye amehukumiwa kuchapwa bakora 100 na adhabu ya kifo kwa kosa la kubadili dini na kuwa Mkristo, amejifungua mtoto wa kike jana asubuhi, akiwa jela anakosubiria kutekelezwa kwa adhabu yake.

Meriam ambaye pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye miaka takribani miwili, wako pamoja jela toka mwezi february mwaka huu toka amekamatwa akidaiwa kuikana imani yake ya kiislamu na kuwa Mkristo, jambo ambalo Meriam analipinga kwakuwa licha ya baba yake kuwa mwislamu lakini amelelewa katika mazingira ya Kikristo toka akiwa mdogo na kwamba hakubadili dini alipoolewa na Dkt Daniel bali alikuwa Mkristo toka udogoni.

Licha ya utetezi wake huo, mahakama nchini humo imemtia hatiani mwanadada huyo mwenye miaka 27 kwakuwa ndoa yake haitambuliki kwa mujibu wa sheria za kiislamu na kwamba ameshiriki uzinzi katika kupata watoto wake hao. Meriam alipewa mda wa kujifikiria na kurudi kuwa mwislamu ili kuondolewa adhabu ya kifo, lakini hakufanya hivyo na kushikilia msimamo wake wa kuwa Mkristo, jambo ambalo lilipelekea hakimu Abbas kumuhukumu kifo na bakora 100, adhabu ambazo atazitumikia mara baada ya kujifungua.

Kwa mujibu wa mumewa dkt Daniel amesema mkewe amefungwa kwa mnyororo miguuni na hali yake imedhoofika huko gerezani. Hata hivyo tayari mashirika na mataifa mbalimbali wameitaka Sudan kumwachilia mwanamke huyo na kuwapa watu uhuru wa kuabudu wanachokipenda. Endelea kumuombea Meriam.
Bonyeza hapa kuona taarifa ya habari ikielezea tukio hilo

Unknown


Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit. Ut odio. Nam sed est. Nam a risus et est iaculis adipiscing. Vestibulum ante ipsum faucibus luctus et ultrices.
Follow me @Bloggertheme9

0 comments:

Recent News