Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Thursday, 15 May 2014

Unknown / / 0

         Mamia ya watu wakisikiliza neno la Mungu katika moja ya huduma JEM

 Mwimbaji wa nyimbo za injili Tumaini Mbembela akimtukuza Mungu katika mojawapo ya huduma za JEM
 Dada huyu anayeitwa Happy Aggrey kutoka wilaya ya Mbalali mkoani Mbeya ,mnamo tarehe 13/04/2014 alihudhuria semina ya neno la Mungu iliyokuwa ikiendeshwa na Apostle Jeremiah Mwakanyelenge ndani ya kanisa la Moravian Isanga Mbeya akiwa na maumivu makali ya tumbo yaliyokuwa yakisababishwa na kupata uchungu na kupotea baada ya kupitiliza zaidi ya wiki 1 ya makadilio ya daktari ya siku ya kujifungua...dada huyo alipita mbele wakati wa kuombea watu wenye shida mbalimbali...usiku huohuo saa 7 za usiku dada huyo alijifungua mtoto wa kiume anayeitwa Jackson Daudi...Hakika Mungu anaweza kufanya mambo yote....Kwa habari zaidi tembelea http://www.jemministry.or.tz/

 Mtoto Jackson Daudi akiwa amepumzika ...

JAJI AMUHUKUMU KIFO MWANAMKE ALIYEBADILI DINI KUWA MKRISTO NCHINI SUDAN


Mwanamke wa kisudani aitwaye Meriam Yahia Ibrahim Ishag (27) jina ambalo analitumia baada ya kubadili dini na kuwa mkristo, amehukumiwa kunyongwa mpaka kifo na mahakama moja nchini huko Khartoum Sudan baada ya kukataa kata kata kuikana dini yake mpya na kurudi kwenye uislamu.

Mwanamke huyo alikuwa akifahamika kwa jina la Adraf Al-Hadi Mohammed Abdullah alipewa siku tatu kama nafasi kwake kurudi katika dini yake ya kiislamu lakini akabaki na msimamo wake kitendo kilichomfanya jaji Abbas Mohammed Al-Khalifa aliyekuwa akimuita mwanamke huyo kwakutumia jina lake la zamani la kislamu kwamba amemuhukumu kunyongwa mpaka kifo kwa kuukataa uislamu na kuwa mkristo ikiwa pamoja na kuchapwa viboko 100 kwa kosa la uzinzi kutokana na mwanamke huyo kuwa mjamzito.

Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo siku ya leo, mmoja kati ya viongozi wa kiislamu alienda
Baadhi ya wakristo wakiwa kanisani nchini Sudan.
kuzungumza na mwanamke huyo kwa dakika 30 akimsisitiza kubadili uamuzi wake bila mafanikio na kusikika akimwambia jaji Abbas kwamba yeye ni mkristo na hajawahi kushiriki uislamu na ndipo jaji huyo kutoka katika wilaya ya Haj Yousef alipoamua kumhukumu kifo huku mwanamke huyo akionekana kutostushwa na hukumu hiyo.

Baada ya hukumu hiyo watu wapatao 50 waliandamana kupinga hukumu hiyo wakisema si haki kwakuwa suala la dini ni haki kikatiba huku pia kundi lingine linalounga mkono hukumu hiyo liliwasili kuonyesha kuunga mkono jambo hilo huku ikielezwa hakutokea hali ya uvunjifu wa amani.

Mdau wa GK omba kwa ajili ya Meriam na taifa lake kwa ujumla, bila kusahau wakristo wanaopitia hali ya mateso kwasababu ya imani yao, lakini pia ombea wanaowatesa kwamba wakakutane na nguvu za Mungu. AMEN

Chanzo Yahoo

Unknown


Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit. Ut odio. Nam sed est. Nam a risus et est iaculis adipiscing. Vestibulum ante ipsum faucibus luctus et ultrices.
Follow me @Bloggertheme9

0 comments:

Recent News