Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Monday, 19 May 2014

Unknown / / 0

JAJI AMUHUKUMU KIFO MWANAMKE ALIYEBADILI DINI KUWA MKRISTO NCHINI SUDAN


Mwanamke wa kisudani aitwaye Meriam Yahia Ibrahim Ishag (27) jina ambalo analitumia baada ya kubadili dini na kuwa mkristo, amehukumiwa kunyongwa mpaka kifo na mahakama moja nchini huko Khartoum Sudan baada ya kukataa kata kata kuikana dini yake mpya na kurudi kwenye uislamu.

Mwanamke huyo alikuwa akifahamika kwa jina la Adraf Al-Hadi Mohammed Abdullah alipewa siku tatu kama nafasi kwake kurudi katika dini yake ya kiislamu lakini akabaki na msimamo wake kitendo kilichomfanya jaji Abbas Mohammed Al-Khalifa aliyekuwa akimuita mwanamke huyo kwakutumia jina lake la zamani la kislamu kwamba amemuhukumu kunyongwa mpaka kifo kwa kuukataa uislamu na kuwa mkristo ikiwa pamoja na kuchapwa viboko 100 kwa kosa la uzinzi kutokana na mwanamke huyo kuwa mjamzito.

Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo siku ya leo, mmoja kati ya viongozi wa kiislamu alienda
Baadhi ya wakristo wakiwa kanisani nchini Sudan.
kuzungumza na mwanamke huyo kwa dakika 30 akimsisitiza kubadili uamuzi wake bila mafanikio na kusikika akimwambia jaji Abbas kwamba yeye ni mkristo na hajawahi kushiriki uislamu na ndipo jaji huyo kutoka katika wilaya ya Haj Yousef alipoamua kumhukumu kifo huku mwanamke huyo akionekana kutostushwa na hukumu hiyo.

Baada ya hukumu hiyo watu wapatao 50 waliandamana kupinga hukumu hiyo wakisema si haki kwakuwa suala la dini ni haki kikatiba huku pia kundi lingine linalounga mkono hukumu hiyo liliwasili kuonyesha kuunga mkono jambo hilo huku ikielezwa hakutokea hali ya uvunjifu wa amani.

Mdau wa GK omba kwa ajili ya Meriam na taifa lake kwa ujumla, bila kusahau wakristo wanaopitia hali ya mateso kwasababu ya imani yao, lakini pia ombea wanaowatesa kwamba wakakutane na nguvu za Mungu. AMEN

Chanzo Yahoo

  Bonyeza hapa kusikiliza JP Radio FM...Nyote mnakaribishwa

VODACOM YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KYELA.

Mkuu wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule na Mwenyekiti wa chama cha msaraba mwekundu mkoa wa Mbeya Ulimboka Mwakilili wakimkabidhi mkuu wa wilaya Kyela Margareth Esther Malenga  Msaada waliotoa



Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Margareth Esther Malenga, akitoa shukrani kwa kampuni ya Vodacom na Chama cha Msalaba mwekundu kwa msaada walioutoa  kwa wananchi wake.

Mkuu wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule, alisema baada ya kupata taarifa za mafuriko wilayani Kyela Kampuni ilikaa na kujadiliana namna ya kutoa msaada kwa waathirika hao.



Ziara ya kwenda maeneo yaliokumbwa na mafuriko hali halisi ndiyo hii barabara zimeharibika

Jitihada zinaendelea kutengeneza miundo mbinu ya barabara



Wanafunzi wa shule ya msingi Kajunjumele wakiwa nje ya darasa lao

Mkuu wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule,akiongea na wanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi kajunjumele darasa hilo paa halina baadaya ya kukumbwa na kimbunga kilichoambatana na mafuriko yaliotokea hivi karibuni wilayani Kyela


Mwalimu akiwa nje ya darasa akisahihisha masomo ya wanafunzi wake 

Hii ni nyumba ya mwalimu tope limejaa ndani ya numba hiyo


Hali sasa imetulia na maji yanaenda kwa kasi ya kawaida



KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetoa msaada kwa Wananchi wa Wilaya ya Kyela kufuatia mafuriko yaliyoikumba Wilaya hiyo hivi karibuni na kutoa athari kubwa kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Margareth Ester Malenga, Mkuu wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule, alisema baada ya kupata taarifa za mafuriko wilayani Kyela Kampuni ilikaa na kujadiliana namna ya kutoa msaada kwa waathirika hao.
Alisema baada ya kuchangishana na kupata shilingi Milioni 10, walikubaliana na kitengo cha Msalaba Mwekundu juu ya vitu vinavyohitajika kwa haraka kwa ajili ya kuwapa msaada waathirika na ndipo walipowakabidhi fedha hizo.
Alisema Msalaba mwekundu walinunua Magodoro 500, Vyandarua 500 na mablanketi 500 vyote vyente thamani ya shilingi Milioni 10 ambavyo viliwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela juzi.
Aidha Mwakifulefule alitoa wito kwa mashirika mengine kujitolea kwa hali na mali misaada mbali mbali kwa wakazi wa Wilaya ya Kyela kutokana na kuwa bado na mahitaji muhimu.
Alisema hali badi ni tete na maeneo mengi yaliyoathirika bado hayajafikiwa hivyo ni vema taasisi zingine zikajitokeza kusaidia wananchi walioathirika na mafurika hayo.
Kwa upande waku Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Margareth Esther Malenga, akipokea msaada huo kwa niaba ya wananchi alitoa shukrani kwa kampuni ya Vodacom na Chama cha Msalaba mwekundu kwa msaada walioutoa wananchi wake.
Alisema Kampuni ya Vodacom inaubia na Serikali lakini ndani yake imekuwa ikiitumikia jamii na wananchi ambao ndiyo wateja wao na watumiaji wa bidhaa zao lakini wanaguswa na kutoa misaada mbali mbali kwa jamii inapokuwa inahitajika.
Mwisho.

 

 

Unknown


Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit. Ut odio. Nam sed est. Nam a risus et est iaculis adipiscing. Vestibulum ante ipsum faucibus luctus et ultrices.
Follow me @Bloggertheme9

0 comments:

Recent News