Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Tuesday, 20 May 2014

MTOTO ALIYEIBIWA APATIKANA NA KUKABIDHIWA KWA WAZAZI WAKE

Unknown / / 0

  Bonyeza hapa kusikiliza JP Radio FM...Nyote mnakaribishwa

 MTOTO ALIYEIBIWA APATIKANA NA KUKABIDHIWA KWA WAZAZI WAKE

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi akimkabidhi mtoto Yosia Jerome kwa mama yake Orester Shabani 


Mume na mke baada ya kukabidhiwa mtoto wao wakitoka katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya


Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limemtia nguvuni mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Esther Amos(23) mkazi wa Nzovwe Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga  jinsi ya kiume mwenye umri wa miezi miwili.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema mtoto huyo Yosia Jerome aliibwa Mei 14 mwaka huu alipokuwa na mama yake aitwaye Orester Shaban(24) aliyekuwa akiuza mbogamboga katika soko la Ikuti Kata ya Iyunga Jijini Mbeya majira ya saa tatu asubuhi.

Mbinu aliyoitumia Esther ni kumrubuni mama wa mtoto kwenda kununua samaki huku akimkabidhi shilingi elfu kumi kuwa mbali ya njegere alizonunua kwa Orester pia angehitaji kupata samaki hivyo kumwachia mtoto ndipo alipotokomea naye kusiko julikana.

Kamanda ameongeza kuwa mama wa mtoto alitoa taarifa Polisi kituo cha Iyunga na Kati ambapo juhudi za kumtafuta mwanamke huyo zilianza na kufanikiwa kumpata Kijiji cha Mahenje Wilaya ya Mbozi nyumbani kwa Dada yake Esther.

Baada ya wasamaria wema kusikia taarifa za kuibiwa kwa mtoto wakazi wa Nzovwe walianza kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walianza kufuatilia taarifa za Esther aliyedaiwa kujifungua na yupo kwenye mapumziko ya uzazi kwa Dada yake wilayani Mbozi.

Askari walifuatilia mwenendo wa Esther na kufanikiwa kumkamata Mei 18 mwaka huu majira ya saa saba akiwa na mtoto na alipotakiwa kutoa maelezo alionekana kujikanyaga na hata alipotakiwa kumnyonyesha alishindwa kufanya hivyo badala yake alitoa chupa ya maziwa kwa ajili ya kumnyonyesha.

Baada ya Askari kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa waliitwa wazazi wa mtoto kwa ajili ya utambuzi wa mtoto na baada ya kumtambua Orester alizirai kutokana na kutoamini kile kilichotokea machoni pake kupatikana mwanae akiwa hai.

Mtuhumiwa alisafirishwa hadi Jijini Mbeya kwa mahojiano zaidi na Esther ambapo uchunguzi umebaini kuwa katika maisha yake kabla ya kuolewa amejaliwa kupata mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa na alipoolewa hakujaliwa kupata mtoto ndipo alipodanganya mume wake kuwa ana ujauzito ambapo amekwenda kwa Dada yake kujitazamia.

Mtoto Yosia alifikishwa Hospitali ya Wazazi ya Meta na kwamba Afya yake inaendelea vema.

Kamanda wa Polisi alimkabidhi mtoto kwa wazazi wake Ofisini kwake mbele ya Waandishi wa Habari na Maafisa wa Polisi ambapo alitoa wito kwa wazazi kuwa makini na watoto wao na kutowakabidhi watu wasiowafahamu pia waendelee kushirikiana na Polisi ili kukomesha uhalifu Mkoani Mbeya na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Kwa upande wake Baba wa Mtoto Jerome Nzowa amelishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano mkubwa hata kufanikisha kupatikana kwa mwanae akiwa hai na salama.

 

HATIMAE MTOTO ALIYEFUNGIWA NDANI MIEZI TISA KWA ULEMAVU WA MDOMO SUNGURA ATIBIWA NA KUREJEA SALAMA CHUNYA

Mtoto Selemani Kolineli Mushi(Miezi kumi)kutoka Kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Baada ya kufanyiwa upasuaji wa mdomo sungura

Mtoto Selemani Kolineli Mushi(Miezi kumi) Kabla ya kufanyiwa upasuaji

Yohana Kolineli  mama mzazi wa mtoto huyo akiongea na mwandishi wetu ambae hayupo pichani

Baba mzazi Kolinel Mushin kushoto akimsikiliza mkewe kwa makini baada ya mama huyo kufika kijijini kwao



Mtoto Selemani Kolineli Mushin(Miezi kumi)kutoka Kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya amerejea salama Kijijini baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na kuzaliwa na matatizo ya mdomo sungura.

Mtoto huyo alifichwa ndani baada ya kuzaliwa na kutakiwa kurudi Hospitali ya Wilaya ya Chunya miezi sita baadaye lakini Baba Mzazi wa mtoto huyo aitwae Kolineli Mushin akikataa kumpeleka Hospitali akidai huo ni mpango wa Mungu.

Mwanzoni mwa mwezi Mei baada ya mtoto huyo kukutwa na mwandishi wa Mbeya yetu na kuwashauri wazazi wa mtoto ndipo walipokubali kumpeleka Hospitali ambapo dhamana hiyo ilichukuliwa na Afisa Ustawi wa jamii Anna Geleta la kusafirishwa hadi Hospitali ya CCBRT.

Selemani baada ya kupokelewa katika Hospitali ya CCBRT alifanyiwa upasuaji na kurekebishwa mdomo ambao ulikuwa ukimpa shida wakati wa kula na kupumua kwa shida na aliruhusiwa kutoka Hospitali Mei 15 Mwaka huu na kurejea Mbeya Mei 17 ambapo gharama za safari ya kwenda na kurudi na matibabu kugharamiwa na CCBRT.

Kwa upande wake Baba mzazi Kolinel Mushin na Mkewe Yohana Kolineli wameishukuru Mbeya yetu blog,  Serikali na Asasi ya CCBRT kwa kufanikisha matibabu ya mtoto wao ambapo wao walidhani kuwa ugonjwa huo usingetibika.

Aidha walimshukuru msamaria mwema Osward Mwailomo aliyetoa taarifa kwa mwanahabari na Mwenyekiti wa Kijiji cha Igundu kwa ushirikiano wake hata kufanikisha upasuaji wa mtoto na hali yake inaendelea vema.

Selemani atafanyiwa upasuaji wa pili mwezi Mei mwakani katika Hospitali hiyo ya CCBRT ambapo gharama zote hutolewa na Hospitali hiyo.

Unknown


Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit. Ut odio. Nam sed est. Nam a risus et est iaculis adipiscing. Vestibulum ante ipsum faucibus luctus et ultrices.
Follow me @Bloggertheme9

0 comments:

Recent News