CHUO
cha Mlimani School of Profession Students cha Mbezi kwa Msuguri, jijini
Dar es Salaam, kimetoa hati za udhamini kwa wanafunzi wasiojiweza
wapatao 20, kutoka taasisi za kidini za Kiislam na Kikristo kwa makanisa
ya kata tano zinazozunguka chuo hicho.
Kata hizo ni Msigani, Kimara, Saranga, Mbezi na Kwembe zilizopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wetu mkuu wa chuo Hassan Ngoma, ameitaka jamii kujitokeza ili kutumia fursa waliyotoa kwa watu waliofeli na wale wenye kipato kidogo kuweza kuwasomesha watoto wao kwa kulipa kiwango kidogo cha fedha kulingana na uwezo wa wazazi ama mlezi wao.

‘’Tumejikita
katika kutoa huduma kwa jamii kwa kutoa udhamini wa wanafunzi 20
wasiojiweza, lengo likiwa ni kurudisha fadhila za chuo chetu kuwepo eneo
la Mbezi kwa miaka 5,” alisema mkuu wa Chuo hicho.
%2B(1).png)
0 comments: