Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Wednesday, 27 August 2014





Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mtandao mmoja nchini Kenya unaoendesha shughuli zake nchini Kenya kuanzia Februari 23 mwaka jana, umetoa tangazo linalowataka watu kujiunga na dini inayomwabudu Shetani, ikiwa wazi kwamba imekuwa ikiwaingiza Watanzania katika mtandao wake.
Kupitia mtandao huo ambao kwa hekima Gazeti hili linauhifadhi, dini hiyo imetoa tangazo lenye mvuto wa aina yake ikijinadi kwamba ina uwezo wa kumpatia mtu atakayetimiza masharti ya kujiunga nayo kiasi cha shilingi milioni 50.

“You can join and get sh.50 Milion”, sehemu ya tangazo la dini hiyo linaeleza kwa lugha ya Kiingereza, likimaanisha kwamba atakayefanikiwa kujiunga atapatiwa shilingi milioni 50 za Kenya.
Tangazo la dini hiyo likiwa na nembo yake yenye umbo la duara na alama ya nyota katikati linaeleza jinsi dini hiyo iliyojisheheneza nchini Kenya na kufanikiwa kuwapata wafuasi kutoka Tanzania kuanzia Februari 23 tangu mwaka 2013.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, nchi ya Kenya yenyewe iliwahi kushangazwa na jinsi ambavyo dini hiyo imepenya na nchini humo na kupata mafanikio.

“…took the country by storm which raised the question of how well organized the secret societies associated with devil worshipping are in Africa”, linaeleza tangazo hilo kwa Kiingereza likimaanisha jinsi ambavyo dini hiyo ya siri inayojihusisha na ibada za kishetani barani Afrika ilivyowahi kuifanya Kenya namna ilivyoweza kujiendesha nchi humo. 

Gazeti moja la kila siku linalochapishwa nchini humo, likizungumzia dini hiyo katika moja ya makala zake lilieleza kuwa jumuiya za siri za Waabudu Shetani nchini Kenya huundwa na Wakenya wanaopendelea jambo hilo.

Aidha ililiweka wazi kuwepo kwa mtandao unaotoa mahubiri na pia kuonesha ibada za kishetani huku pia zikijitangazia watu wajiunga na dini hiyo.

Gazeti hilo liloandika kwamba kwamba mtandao huo huwataka watu wanaotaka kujiunga wanapaswa kuuza nafsi zao.

Gazeti hilo linalochapishwa kila siku Jijini Nairibi nchini Kenya, lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa watu waliojiunga na dini hiyo aliyekataa kutaja jina lake,ambapo alibainisha kwamba ni kweli kiasi kikubwa cha fedha hutolewa kwa mtu anayejiunga nao.

Alisema mtu huyo hupatiwa kiasi hicho cha fedha baada ya kutumiza masharti muhimu na kukubaliwa uanawachama kwa vigezo maalumu ambayo sio kila mtu anaweza kuvitimiza.

Fomu maalumu ya kwa mtu anayejiunga na dini hiyo, inamtaka akubali kuuza nafsi yake kwanza.
Pamoja mambo mengine mengi, fomu hiyo inaeleza kwamba mtu anayeuza nafsi yake ni lazima akubali kujitoa kikamilifu na kuitumikia dini hiyo kwa milile hata katika kifo.

Aidha fomu hiyo inamtaka mtu anayejiunga kujaza fomu kwa hiyari yake na kuwa na uelewa wa anachokifanya anachokifanya, ikiwemo mambo yatakayomtokea ikiwa itaachana na dini hiyo.

Uwepo watu wanaodaiwa kumwabudu shetani sio jambo geni kusikia nchini Kenya na Tanzania, ukiacha mataifa ya Marekani na Ulaya ambayo ni kitu cha kawaida, lakini suala la dini hiyo kujitangaza na kuelekeza nguvu zake nchini Tanzania ni suala linalopaswa kuchukuliwa tahadhari.

Akizungumza na Gazeti hili kuhusu suala hilo, mmoja wa wachungaji waandamizi anayechunga kanisa moja kubwa Jijini Dar es Salaam, alisema tangu zama za kale wafuasi wa Shetani walikuwepo na watu hivyo kinachotakiwa ni kwa wachaMungu kulitambua hivyo na kushika nafasi zao katika kuhubiri Injili na kuwavuta watu kwa Yesu ili waepuke hila za shetani katika kuwateka na hatimaye kuwaangamiza.

Kwa sharti la kutatajwa jina lake Gazetini, alisema kuwa waabudu shetani wako wengi ulimwenguni, wakitumia hata huduma na imani tata zinazojitangaza kuwa za Kikristo.

Alisema ndio maana katika mataifa ya barani Ulaya na Marekani ni jambo la kawaida kukuta mtu anasoma Biblia ya Kishetani (tazama picha ukurasa wa kwanza) akiamini kwamba ndiye mungu wake anayepaswa kumwabudu.

“Jambo hilo linamaanisha kwamba waabudu Shetani wapo na ndio maana hata wamechapisha Biblia zao.Kwa kweli dunia ipo katika nyakati za mwisho zilizotabiriwa katika Biblia, hivyo umakini unahitajika sana”, alisema Mchungaji huyo.

“Nawapongeza sana Gazeti Msemakweli kwani mmekuwa mkiandika sana kuhusu imani potofu ili kuwatahadharisha watu na kulifanya Kanisa halisi la Kristo kuwa macho. Ni wajibu wa Kanisa kuhubiri Injili ya kweli ili kuokoa roho za watu zinazongamizwa kwa kutofikiwa na Injili”, alisistiza Mchungaji huyo.

Gazeti Msemakweli limeanika.


Read More

0 comments:

Tuesday, 26 August 2014

DKT. SHEIN AWAAPISHA MAWAZIRI WAPYA IKULU ZANZIBAR SIKU YA JANA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dk.Sira Ubwa Mamboya kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla Dk.Sira alikuwa Naibu Waziri wa Afya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Juma Duni Haji kuwa…
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dk.Sira Ubwa Mamboya kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla Dk.Sira alikuwa Naibu Waziri wa Afya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Juma Duni Haji kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa Waziri wa Afya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Afya,awali alikuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano hafla ya kiapo imefanyika katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar siku ya jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mahmoud Thabit Kombo kuwa Naibu Waziri wa Afya, hafla ya kiapo imefanyika katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Meja mstaafu Juma Kassim Tindwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Omar Khamis Othman kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mwanajuma Majid Abdulla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar  ,kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Ayoub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya Magharibi siku ya jana katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,awali alikua Afisa Tawala katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Hanuna Masoud Ibrahim kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Pemba  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
(Picha na Ramadhan Othman Ikulu.)
Read More

0 comments:

Friday, 22 August 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Wabunge Mhe Abdul Mketeme (kushoto) na Mhe Getrude Rwakatale (kulia) wakifunua pazia kwa pamoja kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua wodi mpya ya  kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa maeneo mbali mbali ya kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini baada ya kukifungua Agosti 22, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wazazi baada ya kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa  kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014. Read More

0 comments:


Abdimalik Yusuph na Mohamed Bashir mwandishi wa habari wakiwa mahakamani
Meneja wa redio Shabelle, inayomilikiwa kibinafsi, iliyoko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, amearifu BBC kuwa yuko mafichoni baada ya utawala nchini humo kuifunga stesheni yake.
Mohamed Musa amesema wanajeshi walishambulia ofisi za stesheni hiyo siku ya Ijumaa, na kutia watu 20 nguvuni, watatu kati yao wakiwa wamezuiliwa hadi sasa bila ya kufunguliwa mashtaka.
Redio hiyo ilirejea kupeperusha matangazo yake siku ya Jumanne, lakini ilivamiwa tena na vifaa vyote vya utangazaji kutolewa.
Musa amekana madai kuwa redio hiyo ilikuwa inaeneza habari zinazochochea chuki.
Serikali, inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, ilitoa habari inayosema kuwa stesheni hiyo haikufuata sera za taaluma ya utangazaji kwa kueneza ujumbe unaochochea vurugu kati ya jamii za Mogadishu.
‘Jambo la kutisha’
HALI IKOJE MOGADISHU?
Kumekuwepo na wasiwasi mjini Mogadishu kufuatia operesheni ya serikali ya kupokonya raia silaha zisizo halali, ambapo wanamgambo katika vitongoji kadhaa wamepokonywa silaha.
Bwana Musa amesema Shabelle haikupeperusha habari zozote za kuegemea upande mmoja, zinazounga mkono au dhidi ya operesheni hiyo ya serikali.
"Hatuegemei upande wa serikali, hatuegemei upande wa wapinzani, sisi hupasha wanachi yaliyo ya kweli,” aliarifu BBC Focus katika kipindi cha redio cha Afrika.
Mwanahabari wa BBC Mohammed Moalimu aliye Mogadishu amesema mashirika ya watangazaji yamekashifu kukamatwa kwa watangazaji hao na kuelezea kushtushwa kwao na mkondo unaochukuliwa na serikali katika operesheni zake.
Kumekuwepo na miito ya wanahabari waliokamatwa kufunguliwa mashtaka kulingana na katiba, kwani katiba inaelekeza kuwa waliozuiliwa hufaa kufikishwa mahakamani kwa kipindi cha masaa 24.
UHUSIANO WA SERIAKALI NA KITUO HICHO UKOJE?
Bwana Musa alikiri kuwa kulikuwepo na uhusiano wa kiuhasama kati ya Shabelle na serikali, mwaka uliopita redio hiyo ilikuwa mpangaji katika jumba la serikali, na serikali iliwafukuza kutoka humo.
Musa alisema aliamini kuwa amri ya kukamatwa kwake ilikuwa imetolewa na alihofia kuwa huenda wanahabari wenzake waliotiwa nguvuni wakatendewa unyama.
"Niko mafichoni Mogadishu.... Nahamahama, ni jambo la kutisha mno."
Wababe wa vita vya kiukoo, wanasiasa hasimu, na wanamgambo wa kiislamu wamekuwa wakipigania uthibiti wa Somalia tangu Siad Barre kuondolewa mamlakani 1991 baada ya kuongoza kwa muda mrefu.
Chini ya mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, serikali mpya ilibuniwa mwaka 2012 inayojaribu kuchukua uthibiti wa maeneo yaliyochukuliwa na wanamgambo wa Al-Shabaab walio na mtandao na al-Qaeda, ili kurejesha utulivu nchini humo wakisaidiwa na Umoja wa Afrika.
Read More

0 comments:


Boko Haram wazidi kumlaza macho Raisi Jonathan Moyo
Kundi la wapiganaji la kiislam la Boko Haram,wamevamia shule moja ya mafunzo ya kipolisi.kituo hicho cha mafunzo kilichoko kwenye kitongoji cha Gwoza kiko karibu na mpaka wa nchi ya Cameroon ambacho hufundisha maofisa wa Polisi nchini Nigeria.
Kikundi hicha Boko Haram pia kinasemekana kuudhibiti mji wa jirani na Gwoza uitwao Buni Yadi.
Nalo shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch wametoa takwimu ya vifo vilivyosababishwa na kundi hilo kua watu zaidi ya elfu kumi mpaka sasa tangu walipoanzisha harakati za kutaka upande wa kaskazini mwa Nigeria uwe chini ya utawala wa Kiislam.
Read More

0 comments:


Raisi Barak Obama aahidi ulinzi kwa wamarekani
Kitengo cha sheria nchini ya Marekani kimeanza kufanya uchunguzi wa jinai dhidi ya kifo chamwandishi wa habari mwenye asili ya Marekani ,James Foley aliyeuawa na wapiganaji wa kiislamu wenye msimamo mkali.
Mwanasheria mkuu wa kitengo hicho,Eric Holder ameweka wazi kuwa wote waliohusika na mauaji ya mwandishi huo watawatia mkononi muda si mrefu.
Maofisa wa serikali ya Marekani wandai kwamba askari hao wauaji walidai kiasi kikubwa cha pesa zipatazo dola za kimarekani zaidi ya milioni mia moja na thelathini kama fidia ya kumuachilia James Foley.
Marekani imekwisha anza harakati za kuwasaka na hatimaye kuwakamata waliohusika na mauaji ya mwandishi huyo kwa kurusha ndege zake takriban sita katika anga inayomilikiwa na waislamu kaskazini mwa Iraq.
pamoja na kwamba waislam hao kutishia kumuua mmarekani mwingine wanayemshikilia kama ulipizaji wa kisasi endapo mashambulio yataelemea upande wao.
Read More

0 comments:

BONGO MUVI WACHAFUKA!

Na: Gladness Mallya na Imelda Mtema

JAMBO limezua jambo! Baada ya hivi karibuni wasanii wa Bongo Muvi (Movie) kufanya dua kwa ajili ya wenzao waliofariki dunia, baadhi ya ndugu wa marehemu wamecharuka na kudai kuwa waandaaji wa kisomo hicho walifanya kwa manufaa yao binafsi.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baadhi ya ndugu wa marehemu wanalalamika kuwa dua hiyo iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,…
Na: Gladness Mallya na Imelda Mtema
JAMBO limezua jambo! Baada ya hivi karibuni wasanii wa Bongo Muvi (Movie) kufanya dua kwa ajili ya wenzao waliofariki dunia, baadhi ya ndugu wa marehemu wamecharuka na kudai kuwa waandaaji wa kisomo hicho walifanya kwa manufaa yao binafsi.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baadhi ya ndugu wa marehemu wanalalamika kuwa dua hiyo iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar, ilikuwa ni kwa ajili ya kujipatia fedha yeye ndiyo maana hakuona haja ya kuwashirikisha.
“Dua ilifanyika lakini baadhi ya ndugu wa marehemu hawakuambiwa na wanalalamikia sana kitendo hicho kwani si cha kiungwana, kimsingi mamilioni waliyopewa na mdhamini wa shughuli yametumika vibaya,” kilidai chanzo hicho bila kueleza fedha hizo zimepatikana wapi.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba akizungumza jambo.
Baada ya malalamiko hayo kutua mezani, mapaparazi wetu waliwatafuta ndugu wa marehemu ambao hawakuonekana kwenye dua hiyo ambapo walifunguka kwa nyakati tofauti:
MKE WA MZEE SMALL
Bi. Fatuma Said ambaye ni mke wa aliyekuwa mkongwe wa maigizo nchini, marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’ alisema kwamba hawakupewa taarifa wao kama familia jambo ambalo limemsikitisha sana.
Aliyekuwa mke wa muongozaji wa filamu Bongo(George Otieno Tyson) Beatrice Shayo.
“Imeniuma kwa kweli kwani sisi wajane tunatengwa sana, yaani wasanii wakishazika hakuna anayerudi nyuma tena, kitendo cha kutokututaarifu kuhusu dua kimeniumiza sana jamani tungepewa tu taarifa,” alisema Fatuma.
BEATRICE SHAYO ‘MKE WA TYSON’
Huyu ni mwanadada aliyekuwa mke wa marehemu, George Otieno ‘Tyson’ ambaye naye alikiri kwamba hakuwepo kwenye dua kwa sababu hakuwa na taarifa.
Aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, marehemu Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ enzi za uhai wake.
“Sikujisikia vizuri na imeniuma sana kwani sikujua inafanyika wapi na imeandaliwa na nani, ukweli walioandaa hawakufanya vizuri kwani walipaswa kutushirikisha sisi wahusika ili tuwe kitu kimoja, sasa nashangaa walifanyaje dua wakati ndugu na jamaa wa marehemu hawana taarifa?” alisema Beatrice.
MAMA SHARO
Mama wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ ambaye alisema kwamba hakuwa na taarifa yoyote kuhusu dua na ndiyo alisikia kutoka kwa mwandishi.
“Ndiyo nasikia kwako, ukweli nimeumia kutokupewa taarifa kwani ningejumuika na mimi kwa ajili ya kumuombea mwanangu, naona wamenitupa na kunisahau kabisa, wasanii msiwe mnanitenga hivyo jamani!” alisema Mama Sharo.
Aliyekuwa mkongwe wa maigizo nchini, marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’ enzi za uhai wake.
SETH BOSCO
Ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba ambaye alitafutwa baada ya simu ya mama Kanumba kuita bila kupokelewa ambapo alisema wao kama familia hawakupewa taarifa ndiyo maana hawakuonekana kwenye dua hiyo jambo ambalo limewahuzunisha.
“Aliyeandaa dua hiyo hakufanya jambo la kiungwana, tumejisikia vibaya sana kwani suala kama hilo walitakiwa kuwafuata wahusika na kuwaalika tena ikiwezekana washirikiane kwa pamoja lakini walifanya kwa ajili ya kujipatia fedha tu hakuna chochote,” alisema Seth.
Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
MSIKILIZE RAIS
Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba alilaani vikali kitendo hicho na kusema waandaaji hawakufuata utaratibu.
“Walitakiwa kuwashirikisha wahusika na mazingira haya tata ndiyo maana maswali yanakuwa mengi vinywani mwa watu kwamba hakikuwa kitu chema na cha uungwana,” alisema.
NYERERE SASA!
Akizungumza muandaaji mkuu wa shughuli hiyo, Steve Nyerere alisema wahusika wote walipewa taarifa japokuwa aligawana majukumu na watu wengine kwani asingeweza kuwafikia wote.
“Sisi tuligawana majukumu na nilituma watu kwa wahusika sasa kama hawakuwa na taarifa siyo kosa langu ni la kwao hao niliowapa hilo jukumu, hatukufanya shughuli ile kwa masilahi binafsi zaidi ya kuwakumbuka ndugu zetu,” alisema Steve pasipo kufafanua zaidi.
Read More

0 comments:

Thursday, 21 August 2014

DEREVA BODABODA MBARONI KWA KUMNG’ATA MWENZAKE MDOMO NA KUONDOKA NAO

Richard Konga, Arusha

DEREVA wa bodaboda, Adinan Adam, mkazi wa Kata ya Olorieni, mkoani Arusha ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumng’ata mdomo Shabani Temba na kuondoka nao.
Kijana Shabani Temba aliyepigwa na kung'twa na dereva wa bodaboda, Adinan Adam.
Akizungumza kwa uchungu wakati akitoa maelezo katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Olorieni, Shabani alisema ameshangazwa kujikuta anapigwa kisha kung’atwa mdomo na kutolewa nyama ya mdomo pasipokuwa na kosa…
Richard Konga, Arusha
DEREVA wa bodaboda, Adinan Adam, mkazi wa Kata ya Olorieni, mkoani Arusha ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumng’ata mdomo Shabani Temba na kuondoka nao.
Kijana Shabani Temba aliyepigwa na kung'twa na dereva wa bodaboda, Adinan Adam.
Akizungumza kwa uchungu wakati akitoa maelezo katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Olorieni, Shabani alisema ameshangazwa kujikuta anapigwa kisha kung’atwa mdomo na kutolewa nyama ya mdomo pasipokuwa na kosa lolote.
Temba alisema, Alhamisi iliyopita, majira ya saa 12 jioni alifika katika kijiwe cha vyuma chakavu katika kata ya Olorieni akiwa amechoka kutokana na mizunguko yake, ndipo alipoona akae juu ya bodaboda iliyokuwa imeegeshwa kijiweni hapo huku watu wengine wakiwa pembeni yake.
“Nilipokuta pikipiki (bodaboda) hiyo ikiwa imeegeshwa katika kijiwe hicho kutokana na hali yangu ya kuchoka, niliamua kuikalia ndipo ghafla mtuhumiwa alipotokea na kuanza kunishambulia kisha kuning’ata hadi kuondoa nyama yote ya mdomo wangu,” alisema mlalamikaji huyo.
Mtuhumuiwa ambaye ni dereva wa bodaboda, Adinan Adam(aliyesimama) akiwa Kituo Kidogo cha Polisi cha Olorieni, mkoani  Arusha.
Alisema baada ya kutendewa tukio hilo, alipiga kelele hali iliyosababisha wasamaria wema waliokuwa katika eneo hilo kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha katika kituo cha polisi ili kujibu tuhuma zinazo mkabili.
Kwa upande wake mtumuniwa huyo alipohojiwa sababu ya kutenda kosa hilo alisema ilikuwa ni hasira za kishetani kwa kuwa alifikiri kitendo cha mlalamikaji kukaa kwenye bodaboda yake kungesababisha kuibiwa.
Mtuhumiwa huyo aliomba asamehewe akidai kuwa alifanya tukio hilo kwa sababu ya hasira ambapo amebaini ni kosa baada ya kutiwa mbaroni na jeshi la polisi.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wamelaani kitendo hicho na kudai kuwa kinaweza kuhusishwa na viashirio vya mazingira ya vitendo vya kishirikina.
“Kitendo alichofanyiwa Shabani siyo bure kitakuwa na mambo ya kishirikina, inabidi ahangaike kujua undani wake,” alisema kijana mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
Jeshi la polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari limeshamkamata mtuhumiwa ambaye amefunguliwa jalada la kesi ya jinai Namba AR/RB/10937/2014 KUJERUHI.
Read More

0 comments:

Wednesday, 20 August 2014

Kushoto ni Padri Kassase akiwa na mkuu  wa chuo cha Mlimani School of Professional Students, Hassani Ngoma katika makabidhiano ya hati ya udhamini wa  wanafunzi .
Viongozi na wawakilishi wa dini ya Kikristo na Kislamu wakiwa katika majadiliano kabla ya mkutano kuanza.
Mkuu wa chuo cha Mlimani Hassani Ngoma akisikiliza maswali kutoka kwa viongozi wa dini (hawapo pichani).
Mkuu wa chuo cha Mlimani School of Profession Students, Hassan Ngoma akikabidhi hati ya udhamini kwa wanafunzi  20 kutoka taasisi za dini ya Kiislam na Kikristo.
Viongozi na wawakilishi wa dini ya Kiislam wakiwa na bahasha zenye fomu ya udhamini walizopewa na chuo cha mlimani School of Profession Students.
Wanafunzi wakiwa wanajisomea eneo la chuo.
Wawakilishi wa dini ya Kikristo na Kiislam zinazozunguka chuo cha Mlimani School of Profession Students, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo hicho.
Baadhi ya waumini na viongozi wa dini ya Kiislamu wakibadilishana mawazo nje ya jengo la chuo cha Mlimani, Mbezi kwa Msuguri.
Kibao cha chuo cha Mlimani School of Profession Students.
CHUO cha Mlimani School of Profession Students cha Mbezi kwa Msuguri, jijini Dar es Salaam, kimetoa hati za udhamini kwa wanafunzi wasiojiweza wapatao 20, kutoka taasisi za kidini za Kiislam na Kikristo kwa makanisa ya kata tano zinazozunguka chuo hicho.
Kata hizo ni Msigani, Kimara, Saranga, Mbezi na Kwembe zilizopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wetu mkuu wa chuo Hassan Ngoma, ameitaka jamii kujitokeza ili kutumia fursa waliyotoa kwa watu waliofeli na wale wenye kipato kidogo kuweza kuwasomesha watoto wao kwa kulipa kiwango kidogo cha fedha kulingana na uwezo wa wazazi ama mlezi wao.
‘’Tumejikita katika kutoa huduma kwa jamii kwa kutoa udhamini wa wanafunzi 20 wasiojiweza, lengo likiwa ni kurudisha fadhila za chuo chetu kuwepo eneo la Mbezi kwa miaka 5,” alisema mkuu wa Chuo hicho.
Read More

0 comments:

MWANDISHI WA MAREKANI AKATWA KICHWA

Mwandishi wa habari wa Marekani aliyekatwa kichwa, James Wright Foley (kushoto), akiwa amevishwa kanzu maalum.
Kabla ya kuuawa kwake, Foley, aliwataka marafiki, wanafamilia wake na wapenzi wake wote kupambana na “wauaji wangu wa kweli” ambao ni serikali ya Marekani.…
Mwandishi wa habari wa Marekani aliyekatwa kichwa, James Wright Foley (kushoto), akiwa amevishwa kanzu maalum.
Kabla ya kuuawa kwake, Foley, aliwataka marafiki, wanafamilia wake na wapenzi wake wote kupambana na “wauaji wangu wa kweli” ambao ni serikali ya Marekani.
Foley akiwa na muuaji wake ambaye alisema kitendo cha kumwadhibu mwandishi huyo ni kulipiza kisasi mashambulizi ya ndege za Marekani nchini Iraq.
Muuaji wa Foley akijitayarisha kumkata kichwa.
Foley enzi za uhai wake hadi alipopotea Novemba 2012, baada ya kutekwa huko Taftanaz, kaskazini mwa Syria.
Mama yake Foley, Diana, na baba yake John, wakiwa katika mkesha kanisani kuwataka wapiganaji wa ISIS kuwaachia mateka wao.
Kikosi cha Kiislam cha kijeshi chenye msimamo mkali kimeachilia video inayoonyesha mauaji ya mwandishi wa habari mwenye asili ya Marekani, James Foley, aliyepotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria miaka miwili iliyopita na sasa ameuawa.
Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo, serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwa nini James Foley auawe.
CHANZO CHA HABARI www.globalpublishers.info
Read More

0 comments:

Recent News