Turn off for: Swahili
Mtumishi wa mungu calvin Nyorobi akiwaanaimba wakati wa uzinduzi wa albam yake mjini Tunduma Muimbaji wa nyimbo za injili na mtangazaji wa mtangazaji wa kituo cha radio kiitwacho Ushind Fm Radio, Calvin Nyorobi atikisa mji wa Tunduma mkoani mbeya Jumapili ya tarehe 7-12-2014 wakati alipokuwa akizindua albam yake ya kwanza ijulikanayo kwa jina la USIKATE TAMAA.
Muimbaji huyo aliyefanya tamasha hilo katika ukumbi wa kanisa la Tanzania Asemblies of God(TAG)Tunduma kwa Askofu Kalinga ambapo watu wengi walihudhulia tamasha hilo la aina yake katika mji huo na kumuona mungu kwa namna ya ajabu
Askofu Kalinga wa kanisa la TAG Tunduma akiwa katika tamasha hilo mara baada ya kuzindua rasmi
waimbaji mbalimbali pamoja na kwaya mbalimbali walihudhuli tamasha hilo na kutoa michango kwa ajili ya kumtia moyo muimbaji huyo akiwemo Tumaini Mbembela(mke wake),Sara Mwanginde,Hawa Lusekelo,Peter Mbuba, Gwakisa Mwakilema,Tedy na kwaya mbalimbali zilikuwepo kuhakikisha tamasha linapendeza na kuvutia.
waimbaji mbalimbali pamoja na kwaya mbalimbali walihudhuli tamasha hilo na kutoa michango kwa ajili ya kumtia moyo muimbaji huyo akiwemo Tumaini Mbembela(mke wake),Sara Mwanginde,Hawa Lusekelo,Peter Mbuba, Gwakisa Mwakilema,Tedy na kwaya mbalimbali zilikuwepo kuhakikisha tamasha linapendeza na kuvutia.
Muimbaji huyo ambaye pia amekuwa akija kwa kasi katika tasnia ya habari amedai kuwa kumtumikia mungu kwa nanmna ya uimbaji ni tamaa ya yake siku nyingi kwani anaamini katika kutumika pia ndiko ziko Baraka za mungu "kutumika ndko kunafanya mtu apokee mshahara wake hivyo katika kutumika kuna nguvu ya ajabu ndiyo sababu inayo nifanya niwe natamani kmtumikia mungu siku zote" alisema
wageni waalikwa wote waliweza kuonesha uwezo wao kufanya kila linalowezekana kuhudhulia tamasha hilo pamoja na changamoto za hali ya hewa lakini bado wali weza kuwa na subira ya kumuona mtumishi wa mungu huyo kwani walizoea kumsikia katika radio tu na siyo kuonana naye ana kwa ana na tamasha lijawa n nguvu ya mungu na watu walimuona mungu aliye hai katika mji wa tunduma
%2B(1).png)
0 comments: