
Shughuli ya kutafuta ndege AirAsia ambayo iliyopotea juzi usiku wa kuamkia imeendelea leo tena baada ya zoezi baada ya zoezi hilo kusitishwa kwa muda, ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Bornea ambapo ndege hiyo ilipotea
Ndege ya indonesia imepotea ikiwa na abiria 162 ikitokea Surabaya nchini humo na kwenda singapore, habari za kupotea ndege hiyo QZ8501 zilianza kutolewa na mitandao mbalimbali ya kijamii mara baada ya kupata taarifa kutoka katika akaunti ya facebook ya Air indonesia.
Kampuni ya kutengeneza ndege ya Airbus ya ufaransa ilisema ndege hiyo ilikabidhiwa kwa kampuni ya AirAsia ikiwa miongoni mwa ndege zilizozalishwa mwaka 2008 na hadi jumapili shirika hilo limedai kuwa ndege ilikuwa imesafiri safari 13,000 ambayo ni sawa na masaa 23,000
Tarifa zilozo patikana katika vyanzo mbalimbali vya habari za kimataifa zinasema marubani waliomba kuchepuka njia kutokana na hali ya hewa mbaya iliyokuwepo kwa wakati huo ni kwa mujibu wa shirika la usafirishaji wa anga la indonesia (CAA).
Uongozi wa kampuni hiyo ulithibitisha kupotea kwa ndege aina ya Airbus320-200 yenye namba za usajili PK-AXC iliondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Surabaya saa 11:35(7:35 usiku) na kupoteza mawasiliano nawaongozaji wake saa 1:24(9:24usiku)
Ndani ya ndege kulikuwa na abilia 155 ambao kati yao watu wazima walikuwa 138 na watoto 16 pamoja na mtoto mchanaga mmoja, pia walikuwamo marubani wawili,wahudumu wanne na muhandisi mmoja ambapo mingoni mwao kulikuwa na raia wa nchi mbalimbali wakiwemo raia 156 wa indonesia,wakorea watatu, na raia mmoja wa ufaransa,malaysia na singapore
Hadi sasa juhudi za kuisaka ndege hiyo zinaendelea kwa kushirikiana na shirika husika la CAA AirAsia
%2B(1).png)
0 comments: