Anaitwa Faridah Efesi Ambonisye ni mwimbaji wa nyimbo za injili na nyimbo na anatambulikana kwa jina la nyimbo yake - USIJIINUE na alizaliwa tarehe 31-july 1995 na alizaliwa mkoani Mbeya (chunya mjini-ujenzi) na kwa sasa unaishi mkoa wa mbeya eneo la soweto na ni mwanafunzi lakin pia anajishughulisha na huduma ya uimbaji wa nyimbo za injili.
Farida alianza kuimba kwaya akiwa na msukumo wa huduma ya uimbaji ndani yake, kwaya mbalimbali ameweza kuimba nazo kama vile vijana “A” Chunya,isanga,Ruanda katika makanisa ya Moravian Tanzania; lakini hali ilibadilika mnamo mwezi wa 12 mwaka jana alipo sikia wito wa kuhudumu binafsi kwani watu wengi walimshauri kuaza huduma hii na pili ni huduma aipendayo kwa siku nyingi.
Katika kila kitu kizuri hapawezi kosa changamoto na kwa Farida changamoto anzo zipitia katika huduma ya uimbaji ni kuvunjwa moyo na baadhi ya watu walio mtangulia kihuduma kwani wao hujiona kuwa wamefika na kuwadharau waimbaji wanao anza huduma hii ya uimbaji wa nyimbo za injili lakini pia kukosa wadhamini wa huduma hiyo kwani anatamani kufanya huduma mahali pengi na kwa wakati muafaka lakini tatizo kubwa ni upatikanaji wa pesa za kurekodia nyimbo zengine ili kukamilisha albam yake
“kiu ya kufika mahali ndiyo itakayo kuwezesha kufanikiwa katika kila kitu unacho kitamani kufanya”
Ushauri wake kwa waimbaji wale wanaohitaji kuanza kuhudumu kwa namna ya uimbaji wasikate tamaa hata kama hali yao kifedha ,maisha na hata vita vya huduma wawe roho ya kusahau yale wanayo yaona bali kutazama mungu anasema nini kwako,na kuongeza kuwa huduma ya uimbaji waithamini kama huduma zingine pia kutofanya kama sehemu ya kupatia kipato.
Amependa kuwaarika watu kusikiliza kazi zake alizoanza nazo sasa kwani zina ujumbe mzuri kwa ajili ya watu wote “naipenda huduma yangu na naithamini lakini pia napenda kuwa mfano mzuri katika huduma,kitabia,kusema lakini pia hata kutembea kwangu”alisema Farida…

%2B(1).png)
0 comments: