Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Wednesday, 30 April 2014

Wafanyakazi New Habari (2006) wapinga ubaguzi

Wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari (2006), jana walijumuika na baadhi ya mastaa duniani kula ndizi kama ishara ya kupinga vitendo vya kibaguzi kama alivyofanyiwa mchezaji Daniel Alves wa Barcelona

Read More

0 comments:

Tuesday, 29 April 2014

                                   SAFARI YA MWISHO YA MWISHO YA MAMA BENJA
Leo ni siku ya mwisho ya mama Benja .Mamia ya watu kutoka mikoa mbalimbali ndani ya Tanzania pamoja na wachungaji wamehudhuria katika sherehe hii ya mwisho ya kumuaga shujaa huyu wa imani Mama Benja. Mpaka kifo kinamkuta alikuwa Mkurugenzi mkuu wa WWI Taifa( Chama Cha Wamama wa EAGT ). Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali yaliyo tukio katika sherehe hiyo.
                             Baaadhi ya watu waliohudhuria sherehe hii wakimuaga mama Benja
  
Read More

0 comments:

Saturday, 26 April 2014

MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU. 

                     Brian Deacon akiigiza kama Yesu ndani ya filamu ya JESUS.

JEM Gospel Ministry imeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.

 
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.

               Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.
Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

    
watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani  amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.

 

 

Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi
Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.

Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel.
habari kwa msaada wa mtandao.

 

Read More

0 comments:

Friday, 25 April 2014

 

BREAKING NEWS: MKURUGENZI WA WANAWAKE WA INJILI EAGT AFARIKI DUNIA

Taarifa za kusikitisha ambazo zimetufikia hivi punde ni kwamba mkurugenzi taifa wa wanawake wa injili wa kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania anayefahamika kwa jina la Mama Benja, amefariki dunia.

Kwa mujibu wa familia, hadi mauti yanamkuta Mama Benja, presha ilikuwa chini kiasi cha kulazwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa maazishi yatafanyika siku ya Jumanne mkoani Mbeya.

Miaka ya 1974 huko Bugando mjini Mwanza ndipo historia ya Mama huyu imetambuliwa kuanzia, ambapo alikuwa mmoja wa viongozi wa WWK enzi hizo kanisa la Bugando (alikoanzia marehemu Askofu Moses Kulola) likiwa chini ya TAG, wakati huo pia mume wake akiwa mzee wa kanisa. Miaka 6 iliyopita alikuwa makamu wa WWI EAGT na hatimaye 2011 kuwa Mkurugenzi kamili.

Licha ya kuwa muinjilisti wa muda mrefu zaidi, shujaa huyu wa injili kwa zaidi ya miaka 30 amekuwa pia kiongozi wa wamama kwa kipindi kirefu akishika  nyadhifa mbalimbali.

Tutaendelea kukufahamisha zaidi kwa kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia, kaa na GK. BWANA ametoa, na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe

Marehemu mama Benja kwenye maazishi ya aliyekuwa makamu mkurugenzi wa Wanawake wa Injili taifa, Mama Nyanda.Chanzo:Gospel Kitaa

MAMA WANNE APELEKWA KATIKA KITUO MAALUMU NA WATOTO WAKE WAWILI WALIOBAKI KWA AJILI YA UANGALIZI.

 
Meneja wa Kituo cha Nuru, Amanda Fihavango alisema alikubali jukumu la kuwapokea watoto hao pamoja na mama yao kutokana na kuguswa na hali iliyowakuta ya kupotea kwa watoto wawili kati ya wanne.
 


UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kupitia kitengo cha Ustawi wa jamii  umemtafutia kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru Ophans Centre Mama aliyejifungua mapacha wanne na kubakia wawili baada ya kuugua Nimonia kwa ajili ya uangalizi wa karibu.
Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa Hospitali hiyo kumfuata mama mwenye watoto hao Aida Nakawala(25) pamoja na mapacha wake waliobaki kutoka kijijini kwao Chiwanda Wilaya ya Momba mkoani hapa na kuwalaza hospitalini hapo kwa uangalizi wa karibu kwa muda wa zaidi ya wiki moja.
Aidha baada ya afya za watoto hao  kuimarika kwa kiwango kikubwa pia Uongozi wa Hospitali hiyo imemtafutia hifadhi katika kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole jijini Mbeya kwa ajili ya uangalizi wa karibu kutoka kwa wauguzi na maafisa wa ustawi wa Jamii kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwakabidhi watoto hao pamoja na mama yao kwenye uongozi wa kituo cha Nuru Orphans centre, Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Aisha Mtanda, alisema wameguswa na mazingira anayoishi mama huyo na kuamua kumpa uangalizi kwa miezi sita zaidi.
Alisema jukumu hilo halipaswi kufanywa na Hospitali kwa kuwa tayari  walikuwa wamemaliza jukumu lao la kumhudumia alipokuwa ana matatizo lakini wamelazimika kubeba jukumu hilo baada ya kuguswa na mazingira na hali ya makazi ya familia hiyo.
Alisema Hospitali imekubaliana na uongozi wa Kituo cha Nuru kwamba apewe hifadhi mama huyo na watoto wake ili apate uangalizi wa karibu ikiwa na lengo la kunusuru maisha ya watoto waliobaki kutokana na wengine kupoteza maisha kiuzembe kwa ugonjwa wa Nimonia.
Aliongeza kuwa Hali ya hewa ya Mkoa wa Mbeya kwa siku zijazo kunakuwa na baridi kali sana hivyo watoto wasipokuwa kwenye uangalizi wa karibu wanaweza kupatwa na ugonjwa wa Nimonia tena kwa kukosa matunzo kama ya awali.
Kwa upande wake, Meneja wa Kituo cha Nuru, Amanda Fihavango alisema alikubali jukumu la kuwapokea watoto hao pamoja na mama yao kutokana na kuguswa na hali iliyowakuta ya kupotea kwa watoto wawili kati ya wanne.
Aliongeza kuwa ingawa anakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kiuchumi atajitahidi kwahudumia kadri ya uwezo wake na kuomba wasamaria wema watakaoguswa na jambo hilo kujitolea kwa hali na mali kufanikisha kuokoa uhai wa watoto hao pamoja na wengine anaowalea.
Alisema kituo chake hupokea watoto waliookotwa baada ya kutupwa na wazazi wao au mama zao kufariki mara baada ya kutoka kujifungua ambao hupelekwa na Serikali kupitia Ustawi wa Jamii ingawa haichangii fedha zozote baada ya kuwapeleka.
Mtu yoyote mwenye kuguswa anaweza kuwasilisha mchango wake kituoni hapo au kuwasiliana na Meneja wa Kituo cha Nuru kupitia namba za Simu  0754 043004 kwa ajili ya kusaidia watoto hao pamoja na mama yao kuishi hapo kwa muda wa miezi sita.
Mwisho.

 

Read More

0 comments:

Sunday, 20 April 2014

SIKU YA MWISHO YA SEMINA YENYE KICHWA "KUFIKA KILELE CHA MAFANIKIO KWA UAMINIFU"
Apostle Jeremia Mwakanyelenge alifundisha  yafuatayo kabla ya kuingia kwenye maombi
LUKA 4:18-19
ISAYA 61:1
Maandiko yanaposema roho wa Bwana yu juu yangu maana yake ufalme wa Mungu uko juu yako na kwa maana hiyo una nguvu za kumshinda Shetani, haijalishi ni mateso aina gani ulikuwa nayo huko nyuma roho wa Bwana akiwa ndani yako mateso na mahangaiko yote yanapotea.
Waumini mbalimbali waliohudhuria semina wakifuatilia kwa makini mafundisho ya neno la Mungu kupitia kwa Apostle Jeremiah Mwakanyelenge
Mama huyu baada ya kufanyiwa oparesheni, alisumbuliwa na maumivu  kwa miaka  6, lakini baada ya mtumishi  wa Mungu kumuombea kupitia jina la Yesu alifunguliwa papo hapo.
Read More

0 comments:

Mwimbaji wa nyimbo za injili Tumaini Mbembela akimwimbia Mungu wakati ibada ya sifa katika semina ya neno la Mungu ndani ya kanisa la Moravian Isanga inayoongozwa na Apostle Jeremiah Mwakanyelenge..


      Fundi mitambo Jimmy Mwankemwa akihakikisha mambo yanakuwa sawa wakati wa semina. Read More

0 comments:

                   IBADA YA PASAKA KATIKA KANISA LA MORAVIAN ISANGA
         Waimbaji wa kwaya kuu usharika wa Moravian Isanga katika ibada ya Pasaka.
 Apostle Jeremiah Mwakanyelenge kulia akiwa ameketi akifuatilia ibada ya PASAKA ndani ya kanisa la Moravian Isanga.

                   Waumini wa kanisa la Moravian Isanga wakiwa katika ibada ya PASAKA

                Waumini wa kanisa la Moravian Isanga wakiwa katika ibada ya PASAKA Read More

0 comments:

Saturday, 19 April 2014

Mtumishi wa Mungu Jeremiah Mwakanyelenge akifanya huduma ya maombi wakati semina ya neno la Mungu inayoendelea katika kanisa la Moravian Isanga
    Apostle Jeremiah akiendelea kufanya huduma ya maombi wakati wa semina.
   Mmoja wa watu waliokuwa wakianguka baada ya maombi ya Apostle Jeremiah Mwakanyelenge Read More

0 comments:

AINA YA MAOMBI  YATAKAYOKUFANYA UFIKE KILELENI(UFANIKIWE)
  1. Maombi ya kumbariki Mungu(Waebrania 1:3, Wafilipi 2:10, Ufunuo 5:13, Kutoka 20:1-26, 1Timotheo 2:5,1Yohana 3:16,Mathayo 22:37, Matendo 4:12)
  2. Maombi ya toba (Yakobo 5:16, Mwanzo 18:23, Mwanzo 20:17, 1Samweli 12:17, Yeremia 42:2, Marko 1:5, Yohana 9:31, 1Petro 2:24, Hesabu 11:2)
  3. Kumpa shukrani Mungu(Maombi ya shukrani) (Zaburi 28:7, Marko 6:41-43, Kolosai 3:17, 2Thelasonike 1:3, 2Korintho 4:14-16))
  4. Maombi ya uhitaji(Wafilipi 4:6, Mathayo 6:9-13, Waefeso 15:16, Luka 18:1, Warumi 5:8, Zaburi 2:7)
  5. Hayo yote yanabebwa na upendo
UAMINIFU
Uaminifu ni kufuata sheria au kufuata matakwa ya mmiliki wa eneo unaloishi.
  1. Ni lazima uwe na tunda la roho(Wagalatia 5:22-23)
  2. Elewa mpango wa Mungu kwako.(Yohana 10:10, Yohana 3:16)
  3. Usitengane na Mungu/ukimkosea Mungu kumbuka kumuomba msamaha(Warumi 3:3, Isaya 59:10, 1Petro 3:18)
  4. Elewa Yesu yu hai/Uwe mwaminifu hata kama havionekani(1Petro 3:18, 1Korntho15:3)
  5. Ni lazima umkubali(umpokee) Yesu maishani mwako(Yohana 1:12, Waebrania 13:8, Waefeso 2:8-9, Waebrania 10:25)
Read More

0 comments:

Friday, 18 April 2014

     MAFANIKIO
Mafanikio ni kufika katika kile unachokihitaji, kiwe kibaya au kizuri.
2Samweli 21:1-13

MAMBO MUHIMU YATAKAYOFANYA UFIKE KILELENI(KWENYE MAFANIKIO) KWA UAMINIFU

  1. Muogope Mungu kwa njia inayofaa (Mithali 9:10, Zaburi 119:105)
  2. Chagua marafiki wenye hekima(Mithali 13:20)
  3. Epuka kula au kunywa kupita kiasi(Luka 19:41, Mithali 23:1,20,21, Yeremia 29:11)
  4. Usilipize kisasi(Usiwe mtu wa kisasi)(Warumi 12:1, Wafilipi 1:6)
  5. Fanya kazi kwa bidii na uwe mtu wa kubadilika kutaka maendeleo(2Thelasonike2:3-10, Yohana14:12)
  6. Ufuate kanuni ya Mungu(Mathayo 7:12, Torati 4:40, Yoshua 1:7, Luka 17:6)
  7. Dhibiti ulimi wako(1Petro 3:10, 1Falme 10:7, Warumi 12:2)
  8. Uwe mtu wa maombi(1Thelasonike 5:16)


Read More

0 comments:




             Mwimbaji wa nyimbo za injili Scolastica akimsifu na kumtukuza Mungu wakati wa sifa     


        Mwimbaji wa nyimbo za injili Festina Mwandwanga akiongoza ibada ya kusifu na kuabudu
Wanakwaya wa kwaya kuu katika ushirika wa Moravian Isanga wakimwimbia Mungu wakati wa semina
       Mtumishi wa Mungu Baraka akipiga kinanda wakati wa kusifu na kuabudu katika semina


          Mrs Jeremia Mwakanyelenge akimsifu na kumchezea Mungu wakati wa ibada ya sifa. Read More

0 comments:



 Mwimbaji wa nyimbo za injili Alex Mahenge akimtukuza Mungu katika ibada ya Ijumaa kuu wakati wa kusifu.
        Mwimbaji wa nyimbo za injili Festina Mwandwanga akimsifu Mungu wakati wa ibada.

MTUMISHI ELIEZER MWAKIHABA AKISEMA NENO KATIKA IBADA YA IJUMAA KUU KATIKA KANISA LA MORAVIAN ISANGA.
Mtumishi wa Mungu akisema neno  juu ya damu. Mtumishi alisema damu ni uhai.
Kutoka 12:2
Mwanzo 4:10
Torati 12:13
Ebrania 12:24
Ufunuo 9:2,11
Mwanzo 26:14









                     Mtumishi wa Mungu akiendelea kusema neno ndani ya ibada ya Ijumaa kuu.
          Mtumishi wa Mungu Eliezer Mwakihaba akiomba Mungu baada ya kumaliza kufundisha.
Dada huyu alianguka baada ya nguvu ya Mungu kupita ndani yake wakati mtumishi wa Mungu akiomba.       Read More

0 comments:

Thursday, 17 April 2014

NAMNA YA KUJITAMBUA KIBIBLIA YA KWAMBA UMEFIKA KWENYE KUSUDI LAKO AMBALO MUNGU AMELIWEKA.
Mungu anapotaka kutenda jambo kwako haangalii watu wanasema nini juu yako bali huangalia wewe unataka nini kwake.
  1. Mimi mwenyewe nitaanza kutambulika(waamuzi 14:1-21)
  2. Utakuwa mtu mwenye kuhangaika/Mtu mwenye uhitaji mwingi(Mwanzo 30:1 )
  3. Utakuwa ni mtu unayeshuka na kuomba toba(2Nyakati 7:10)
  4. Utakuwa mtu wa vita dhidi ya uovu wa ibilisi(Hesabu 10:9, Yoeli 2:1)
  5. Utakuwa ni mtu wa kusubiri jibu kutoka kwa Mungu(Yoeli 2:21-26)

MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA KUYAFUATA ILI UFIKE KILELENI
  1. Kuwa makini na maisha yako ya rohoni na mwilini(Zaburi 1:1, Mhubiri 9:13-16)
  2. Usimpe ibilisi nafasi (Efeso 4:27)
  3. Kuwa na bidii katika kazi zako(Mithali 22:29, Mhubiri 9:10, Wafilipi 4:13)
  4. Lazima uwe na hekima(Mhubiri 7:12)
Read More

0 comments:

Wednesday, 16 April 2014

SABABU SABA(7) ZINAZO SABABISHA TUSIFIKE MAHALI AMBAPO TUMEKUSUDIA By Apostle Jeremia Mwakanyelenge

  1. Kutokuwaheshimu wazazi wako . (Waefeso 6:1-3)
  2. Kukosa maono .(Habakuki 2:1, Mithali 10:7)
  3. Kutokumcha Mungu(Mithali 10:27. )
  4. Kumwekea Mungu mipaka ya kufanikiwa(Zaburi 78:41, Hesabu 13:41)
  5. Kutomtumikia Mungu kwa kipawa alichokupa(Kutoka 23:25-26, Mithali 3:1-2, Yohana 14:21)
  6. Maisha ya dhambi(Warumi 6:23)
  7. Kukosa bidii katika kumpenda Mungu(Zaburi 91:14-16, Mithali 3:1-6)
Read More

0 comments:

IF YOU YOU WANT TO GO FAST WALK ALONE, IF YOU WANT TO GO FAR WALK WITH OTHERS  By Apostle Jeremiah Mwakanyelenge

Baadhi ya waimbaji wakimtukuza Mungu wakati wa ibada ya kusifu na kuabudu katika semina hiyo. Read More

0 comments:

Tuesday, 15 April 2014


Mtumishi wa Mungu Apostle Jeremia Mwakanyelenge akifundisha katika semina inayoendelea ndani ya kanisa la Moravian Isanga. Semina hiyo inaendelea hadi tarehe 20/04/2014 wote mnakaribishwa.
   
Mtumishi wa Mungu Apostle Jeremia Mwakanyelenge akiombea watu wenye magonjwa.
Mtumishi wa Mungu akiendelea kufundisha katika semina
Somo: Tamani kufika kilele cha mafanikio kwa uaminifu
Baadhi ya waimbaji wakisifu wakati wa kipindi cha kusifu na kuabudu.
Mtumishi wa Mungu Festina Mwandwanga akiongoza ibada ya kusifu na kuabudu,

Wapiga vyombo wakiendelea kumsifu Mungu ndani ya Ibada ya kusifu na kuabudu katika semina
Read More

0 comments:

Recent News