Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Tuesday, 28 October 2014

JE MWAKA 2015 TUTAFIKA?

Unknown / / 0
  Ni miongon mwa maswali waliyo nayo watanzania weng kuhusu uchaguz mkuu mwkan hii ni kutokana na kwepo kwa makundi tofauti yanayokuwa yakipinagana hasa kwa upande wa siasa ndani ya Tanzania, jambo ambalo limechukua sura mpya kwa viongoz na wananchi wa Tanzania ambapo kumezuka makubaliano ya wananchi UKAWA dhidi ya chama tawala CCM

makubaliano ya pamoja, kuking’oa madarakani Chama tawala.
Utiaji huo saini makubaliano ya kukishinda Chama cha Mapinduzi CCM, katika uchaguzi ujao, umefanywa na viongozi wa vyama vinne, huku tukio hilo likishuhudiwa na wafuasi wao.
Katibu Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Dr. Willibrod Slaa ni miongoni mwa viongozi waliotia saini makubaliano hayo na amesema vyama hivyo vitasimamisha wagombea wake kwa pamoja kwenye ngazi zote za uchaguzi kuanzia serikali za mitaa mpaka ngazi ya urais.
Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim seif Sharif Hamad anasema tukio hilo la vyama kusaini makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kuing’oa CCM ni muhimu na la kihistoria.
Viongozi waliotia saini waraka huo wa makubaliano ni Freeman Mbowe Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Profesa Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF, Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye pia ni Makamu wa kwanza rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, James Mbatia Mwenyekiti NCCR Mageuzi, Mosena Nyambabe Katibu Mkuu NCCR Mageuzi, Dr Emmanuel Makaidi Mwenyekiti NLD na Tozzi Matwanga Katibu Mkuu wa NLD.

Unknown


Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit. Ut odio. Nam sed est. Nam a risus et est iaculis adipiscing. Vestibulum ante ipsum faucibus luctus et ultrices.
Follow me @Bloggertheme9

0 comments:

Recent News