IS waachia maeneo muhimu Kobane
Wapiganaji
wa Islamic State wamelazimika kurudi nyuma katika maeneo muhimu ya mji
wa Kobane ulioko
kaskazini mwa Syria kufuatia mashambulio ya anga ya
Marekani, amesema afisa mmoja wa Kikurd.Idriss Nassan ameiambia BBC kuwa IS imepoteza udhibiti kwa zaidi ya asilimia 20% ya mji huo ulio mpakani na Uturuki katika siku za karibuni.
Wanaharakati wanasema zaidi ya watu 600 wameuawa tangu kundi hilo la jihad kuanzisha mashambulio mwezi mmoja uliopita.
Jumatano, viongozi wa Marekani na Ulaya wamekubaliana kuhusu umuhimu wa hatua zaidi kuzuia wapiganaji wa IS kusonga mbele katika nchi za Iraq na Syria.
Katika mkutano wa video, Rais wa Marekani Barack Obama na viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italia wamesema wataongeza msaada pamoja na "njia ya kisiasa" nchini Iraq na kutoa mafunzo kwa majeshi ya nchi hiyo.
'Oparesheni Safisha'
"Labda katika siku chache zilizopita Islamic State walikuwa wakidhibiti asilimia kiasi cha 40% ya mji wa Kobane, lakini sasa ...Ni chini ya asilimia 20% IS wanadhibiti mji huo," amesema. "Jumatano, YPG ilianza operesheni safisha mashariki na kusini-mashariki mwa mji wa Kobane."
Marekani imesema Kobane bado uko katika hatari ya kuanguka kwa sababu ya kuonghezeka kwa idadi ya wapiganaji wa jihad wanaowasili katika mji huo.
Zaidi ya Wasyria160,000 wamekimbia mji huo na kuvuka kuingia Uturuki na wanaishi katika makambi.


%2B(1).png)
0 comments: