Kundi
la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, wameteka mabasi saba ya abiria
yanayofanya safari zake kati ya Jiji la Arusha na Nairobi, Kenya na
kupora mali na fedha ambavyo thamani yake haijafahamika.
Tukio
hilo ambalo limethibitishwa na Jeshi la polisi, mkoani Arusha llitokea
usiku wa kuamkia jana katika eneo la Mbuga Nyeupe, wilayani Longido Mkoa
wa Arusha baada ya watu hao kuweka mawe barabarani na kuwamuru abiria
wote kutemka mmoja baada ya mwingine, kulala chini na kuwapekua kila
kitu walichokuwa nacho.
DEREVA ALIYETEKWA ASIMULIA
Akisimulia mkasa huo, dereva wa basi la Perfect Trans, Joseph John,
alisema kuwa watu hao waliokuwa na silaha za jadi yakiwamo mashoka,
mapanga na sime, waliteka mabasi hayo majira ya saa 8 usiku.
“Hao jamaa walikuwa kama 50 hivi kwani waliteka magari yetu ambayo
yalikuwa yamefuatana, wametuvua hadi viatu, saa yaani walipekua hadi
wanawake waliamriwa kuvua nguo na kuporwa urembo wenye nakshi ya madini
ya vito,” alisema John.
Alisema yeye alikuwa dereva wa kwanza kufika na basi katika eneo hilo
na kuwa alipoona mawe yamepangwa kati kati ya barabara, aliamua
kusimama na alipokuwa akijaribu kuyakwepa, alipigwa jiwe usoni hali
iliyomfanya ashindwe kukimbia.
“Hata wengine walikuwa hawajafunika nyuso zao, tukio lilidumu kwa
dakika zaidi ya shirini, kila walipomaliza kupekua watu wa basi moja
waliwaamuru warudi ndani ya gari,” alisimulia.
Dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jabir Athumani, alisema
baadhi ya majambazi hayo yalikuwa yakiita majina ya baadhi ya watu na
kuwaamuru kutoa fedha walizokuwa nazo.
“Tunaomba vyombo ulinzi na usalama vifuatilie tukio hili kwa umakini
wa hali ya juu ili kuwanasa wahusika wa tukio hili,” alisema Jabir.
Aidha, alililitaka Jeshi la Polisi lirudishe magari ya doria katika
barabara ya Arusha–Namanga ambayo yaliondolewa Aprili mwaka jana.
POLISI: TUTAZUNGUMZA LEO
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi leo.
“Hapa nipo katika majukumu mengine, sipo ofisini nitawapa taarifa za
tukio lote Jumatatu (leo) mchana, naomba subiri nitafanya mkutano na
vyombo vya habari na nitawapa maelezo ya tukio lote,” alisema Sabas.
mbunge wa mbeya mjinimh Joseph Mbilinyi anusurika katika ajali iliyotokea mkoani iringa wilaya ya kilolo eneo la mlima kitonga tarehe 10, inaelezwa kuwa chanzo cha ajali ni kufeli kwa break iliyopelekea kuanguka kwa gari miguu juu kichwa chini. Gari aina ya Toyota rand cruser ambalo lilikuwa likiendeshwa na muheshimiwa huyo na ndani ya gari kulikuwa nawatu wanne na wote walitoka kwa usalama isipokuwa mh: sugu. Gari ya sugu baada ya kupata ajali mkoani iringa
muonekano wa gari baada ya ajali mlima kitonga mkoani iringa
mbunge wa jimbo la mbeya akiwa hospitali kutibiwa majeraha
Read More
0
comments:
Gari yenye
namba za usajili T349CPQ aina ya Kenta likiwa limepata ajali maeneo Mbala
Chalinze baada ya kupasuka taili la nyuma na kupoteza muelekeo.Dereva wa gari
hiloambaye hakutambuluka jna lake aliumia na kukimbizwa Hospitali Chalinze.
Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda LRA.
AFP
Mtu anayedai kuwa mmoja wa makamanda wa juu wa kundi la waasi la LRA kutoka nchini Uganda, anazuiliwa na wanajeshi wa Marekani.
Mtu huyo anayejiita Dominic Ongwen alijisalimisha kwa wanajeshi
wa Marekani, kwa mujibu wa ripoti za Wizara ya ulinzi ya Marekani.
Ongwen anatakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC kwa makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Joseph Kony akiwa Sudani Kusini mwaka 2008.
REUTERS/Africa24 Media
Ongwen
amekuwa akielezwa kuwa naibu wa kiongozi wa LRA, Joseph Kony,
anayetafutwa na wanajeshi wa Marekani na wale wa Umoja wa Afrika. Serikali ya Marekani imeendelea kuthibitisha taarifa hiyo ya kujisalimisha kwa mmoja wa makamanda wa juu wa kundi la waasi wa Uganda la Lords Resistance Army LRA.
Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani, Jane
Psaki, Dominic Ongwen anayedai kuwa ni mmoja wa watu wa karibu wa
kiongozi wa kundi la LRA linaloongozwa na Joseph Kony, amejisalimisha
kwa wanajeshi wa Marekani.
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa iwapo itathibitika kuwa mtuhumiwa
huyu ni mtu wa karibu wa Kony, itakuwa pigo kwa kundi hili ambalo
linaendesha harakati zake kwenye misitu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa
Kenya imesema safari zimeanza kama kawaida baada ya mamlaka hiyo kuondoa
ndege zote kwenye njia ya kurukia ya Jomo Kenya mapema jana kufuatia
tukio la ndege kutua kwa dharura.
Kwenye taarifa yake mamlaka hiyo imesema imemaliza uchunguzi wa
njia ya kurukia ndege na sasa imefunguliwa, na safari zote za kuingia na
kutoka zimerudi katika hali ya kawaida.
Awali mamlaka hiyo ilisema timu yake imefanikiwa kuiondoa ndege
iliyotua kwa dharura kwenye njia ya kurukia, tukio ambalo lilisababisha
ndege kutua kwa muda kwenye uwanja wa ndege wa Mombasa. Hadi sasa
haijajulikana sababu ya ndege hiyo kutua kwa dharura na hakuna ripoti za
watu waliokufa au kujeruhiwa kwenye tukio hilo.
Watu 90 wameuawa katika mapigano
yaliyojiri kati ya askari wa Burundi na waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo katika mkoa wa Cibitoke, kaskazini magharibi mwa Bujumbura.
Msemaji mmoja wa jeshi la Burundi aliyefahamika kwa jina moja la
'Anatoli' amewaambia waandishi wa habari kwamba, mapigano hayo
yaliyoanza tangu siku ya Jumatatu na kuendelea hadi jana, yaliibuka
wakati waasi wanaokadiriwa kufikia 200 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo walipojaribu kuingia nchini Burundi. Kwa mujibu wa afisa huyo wa
jeshi la Burundi, askari wasiopungua 20 wamepoteza maisha huku zaidi ya
waasi 70 wakiuawa. Kwa mujibu wa duru za jeshi la nchi hiyo, hadi sasa
hakujatolewa ripoti kamili juu ya hasara iliyotokana na mapigano hayo.
Inaelezwa kuwa waasi hao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walikuwa
wamekusudia kuteka ardhi na kupora maliasili za eneo la Kibira nchini
Burundi.
0 comments: