Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Monday, 1 September 2014

Marekani yaombwa silaha Ukraine


Robert Menendez
Mkuu wa baraza la kamati ya mahusiano ya Marekani ameiomba nchi yake kupeleka silaha Ukraine ili kukabiliana na kinachodaiwa uvamizi unaofanywa na Urusi.
Robert Menendez amesisitiza Umoja wa Ulaya kutoa silaha za kivita kuisaidia Ukraine ili iweze kujihami dhidi ua Urusi.
Wito huo umekuja huku Rais Putin wa Urusi akiita majadiliano ya haraka kuhusiana na mwa Ukraine kama nafasi ya kufanya makubaliano ya kusitisha uhasama wao.
Kauli ya Putin inakuja ikiwa ni siku moja kabla ya mazungumzo yatakayofanyika huko Minsk kati ya Ukraine na Urusi kujadili machafuko hayo.
Read More

0 comments:

Ebola haizuwii mechi Sierra Leone


Timu ya Sierra Leone
Wakuu wa kandanda wa Sierra Leone wanasema mechi ijayo ya duru za mwanzo za Kombe la Afrika, baina ya Sierra Leone na Ivory Coast, itafanywa ingawa kuna ugonjwa wa ebola Afrika Magharibi.
Shirika la Kandanda la Sierra Leone limesema itataja timu yao ambayo itakuwa na wachezaji walioko nje ya nchi.
Ivory Coast imesisitiza kuwa haitaruhusu mechi hiyo kufanywa katika mji mkuu, Abidjan, kwa sababu ya wasiwasi wa kutapakaza virusi vya ebola.
Lakini haikutangaza wapi mechi itafanywa na pengine inaweza kupoteza mechi hiyo.
Huku nyuma nchini Nigeria, mjane wa daktari aliyekuwa mtu wa sita kufa kwa sababu ya ebola nchini humo, naye ameonekana ameambukizwa virusi.
Na wagonjwa watatu wa daktari huyo mjini Port Harcourt wamepelekwa katika zahanati maalumu lakini haikuthibitishwa iwapo kweli wana virusi vya ebola.
Read More

0 comments:

Recent News