Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Tuesday, 22 July 2014

CECAFA  imetoa Ratiba ya Mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA KAGAME CUP, ambayo yatachezwa huko Kigali Nchini Rwanda kuanzia Agosti 8 na kumalizika Agosti 24.YANGA_NA_KAGAME
Yanga, ambao walipangwa Kundi A, wataanza kwa kuivaa Rayon Sports ya Rwanda kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali hapo Ijumaa Agosti 8.
KMKM ya Zanzibar, ambao wako Kundi moja na Yanga, wataanza kwa kuivaa Atlabara ya South Sudan Siku hiyohiyo Agosti 8 kwenye Uwanja wa Nyamirambo huko Kigali.

MAKUNDI:
KUNDI A
-Rayon Sports [Rwanda]
-Yanga [Tanzania]
-Coffee [Ethiopia]
­-Atlabara [South Sudan]
-KMKM [Zanzibar]
KUNDI B
-APR FC [Rwanda]
-KCCA [Uganda]
-Flambeau de l'est [Burundi]
-Gor Mahia [Kenya]
-Telecom [Djibouti]
KUNDI C
-Vital'O [Burundi]
-El Merreikh [Sudan]
-Benadir [Somalia]
-Polisi [Rwanda]
+++++++++++++++++++
Mechi zote zitachezwa Mjini Kigali kwenye Viwanja vya Amahoro na Nyamirambo huku Rubavu ikiwa ni Uwanja wa Akiba.
Tangu Mwaka 2002 Mdhamini wake mkuu ni Rais Paul Kagame wa Rwanda ambae amekuwa akitoa Dola 60,000 kila Mwaka.
Mashindano haya yatarushwa moja kwa moja kwenye TV na SuperSport International ambacho hivi karibuni kilisaini Mkataba wa Miaka Minne na CECAFA.
Ratiba kamili itatolewa baadae na CECAFA baada Timu zote kuthibitisha kushiriki.
Mbali ya kutwaa Kombe, Bingwa wa Kagame Cup huzoa Donge la Dola 30,000, Mshindi wa Pili Dola 20,000 na Timu ya Tatu hupata Dola 10,000.
RATIBA KAMILI:
TAREHE
NA
MECHI
KUNDI
UWANJA
Ijumaa Agosti 8
1
Atlabara v KMKM
A
NYAMIRAMBO


2
Rayon v Yanga
A
AMAHORO


3
Gor Mahia v KCCA
B
AMAHORO
Jumamosi Agosti 9
4
Vital ‘O’ v Banadir
C
AMAHORO


5
Police v El Mereikh
C
AMAHORO


6
APR v Flambeau
B
AMAHORO
Jumapili Agosti 10
7
KMKM v Young
A
AMAHORO


8
Telecom Vs KCCA
B
NYAMIRAMBO


9
Coffee v Rayon
A
AMAHORO
Jumatatu Agosti 11
10
Banadir v El Mareikh
C
NYAMIRAMBO


11
Gor Mahia v Flambeau
B
‘’


12
Vital ’O’ v Police
C
‘’
Jumanne Agosti 12
13
KMKM v Coffee
A
‘’


14
Yanga v Atlabara
A
‘’
Jumatano Agosti 13
15
APR  v Telecom
B
‘’


16
KCCA v Flambeau
B
‘’
Alhamisi Agosti 14
17
Coffee v Atlabara
A



18
Rayon  v KMKM
A



19
Police v Banadir
C

Ijumaa Agosti 15
20
Flambeau v Telecom
B



21
APR v Gor mahia
B



22
El Mareikh v Vital ‘O’
C

Jumamosi Agosti 16
23
Coffee v Yanga
A



24
Rayon v Atlabara
A

Jumapili Agosti 17
25
Telecom v Gormahia
B



26
KCC v APR
B


Jumatatu Agosti 18


MAPUMZIKO


Jumanne Agosti 19


ROBO FAINALI




27
C1 v B3

NYAMIRAMBO


28
A1 v B2

‘’
Jumatano Agosti 20
29
A2 v C2

‘’


30
B1 v A3

‘’
Alhamisi Agosti 21


MAPUMZIKO


Ijumaa Agosti 22


NUSU FAINALI




31
32
Mshindi 27 v Mshindi 28
Mshindi 29 v Mshindi 30

AMAHORO
Jumamosi Agosti 23


MAPUMZIKO


Jumapili Agosti 24


MSHINDI WA 3 & FAINALI




33
34
Mfungwa 31 v Mfungwa 32
Mshindi 31 v Mshindi 32

AMAHORO
**MUDA WA KUANZA MECHI UTAAMULIWA KATI YA CECAFA, FERWAFA NA SUPERSPORT KWA AJILI YA MATANGAZO LAIVU YA TV Read More

0 comments:




Kutoka kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Sangu, Mwalimu, Andongwisye Bukuku, Katibu wa Jumuiya ya wazazi, wilaya  ya Mbeya Mjini, Juma Mng'ombe na Mkuu wa shule msaidizi Sophyllin Gwandage.
 Katibu wa Jumuiya ya wazazi, wilaya ya Mbeya mjini, Juma Mng'ombe.
 Mkuu wa shule msaidizi, Sangu sekondari, Sophyllin Gwandage akiwa ofisini kwake.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Sangu, Mwalimu, Andongwisye Bukuku.

 Wanafunzi wa kidato cha tatu mchepuo wa Sayansi 1&2.



WADAU wa Elimu Nchini wameombwa kujitokeza kuchangia maendeleo ya kielimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya kujifunzia, ikiwa ni pamoja na walimu kufundishia.
Katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia, shule ya sekondari SANGU inayomilikiwa na Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), iliyopo Jijini Mbeya, imeandaa harambee kwa ajili ya ujenzi wa maabara kubwa ya kisasa na ununuzi wa usafiri wa basi la wanafunzi. 

Akiungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Andongwisye Bukuku, alisema Maabara hiyo inatarajia kugharimu kiasi cha Tsh.111,000,000/=, wakati basi la shule litagharimu shillingi milioni 50.

Alisema ujenzi wa maabara hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa uwepo wa wanafunzi watakaosoma masomo ya sayansi,  na kuongeza kuwa wanafunzi waliopo kidato cha tano na sita ni wale wenye michepuo ya sanaa (Art) pekee, hivyo upatikanaji wa maabara hiyo utatoa fursa kwa shule hiyo kuanzisha michepuo ya sayansi na wanafunzi kunufaika.

“Harambee hii tunatarajia kuifanya Agost 14, mwaka huu, katika ukumbi wa Mkapa hapa Mbeya, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha, NDG.ADAM KIGOMA MALIMA, ambapo matarajio yetu ni kupata shilingi milioni 161.

Kwa upande wake katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM),wilaya ya Mbeya mjini, Juma Mng’ombe, amewaomba wadau wote kujitokeza kwa wingi siku hiyo, kuunga mkono jitihada hizo hususani wanafunzi wote waliosoma shuleni hapo miaka ya nyuma.

Amewataja baadhi ya watu waliosoma shuleni hapo kuwa ni Rais wa Jamhuri ya watu wa Demokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, Mbunge wa Sindgida mjini, Azam Dewji na mbunge wa jimbo la Songea Mjini Emmanuel Nchimbi.

Aidha,Mng’ombe amewaalika wadau wote wenye mapenzi na elimu kote nchini kuchangia kupitia akaunti namba iliyoanzishwa mahususi kwa ajili ya harambee hiyo…..

CRDB bank Tawi la Mbeya. 01J1065276501
Read More

0 comments:

Tuesday, 8 July 2014

Apostle Jeremiah M A akiwa na menyeji wake mchungaji Mchungaji Mkisi katika ibada ya Jumapili asubuhi
Tumaini Mbembela akiwa katika ibada ya sifa katika ibada nzuri ilyojaa uwepo wa Bwana
Waumini wakifurahia uwepo wa Bwana katika ibada
Mchungaji Mkisi hakubaki nyuma aliamua kuingia katika sifa na hatimaye kuchukua jukumu la kuogoza nyimbo za kusifu na kuabudu ilileta raha mmno katika Bwana
Apostle Jeremiah Mwakanyelenge aliyetunukiwa cheo Cha Postor katika ibada hiyo muhimu na nzuri
Mtumishi wa Mungu akifafanua jambo katika mahubiri yake
Mungu aliamua kuwahudumia watu katika ibada yamaombezi hakika Mungu alimtumia mtumishi wake Apostle Jeremiah

Ibada yenye uwepo wa Mungu watu walibubujika hakuna aliyehangaika na mwenzake kila mmoja kwa Mungu tu Read More

0 comments:

Friday, 4 July 2014

Umati wa watu uliofurika katika viwanja kanisa la EAGT mwaka katika mkutano wa Injili Tunduma


Mtumishi wa Mungu Joseph Lwiza maarufu kwa J J Lwiza Maua akihubiri katika mkutano mkibwa wa Injili Tunduma
Mtume Apostle Jeremiah Mwakanyelenge Pamoja na Mwalimu Joshua Mwakitalima wakifurahia jambo na style ya mtumishi Lwiza alivyokuwa akimwakilisha Mungu

Umoja wa waimbaji mkoa wa Mbeya wanaendesha mkutano mkubwa mno ni mkutano wa kihistoria haijawahi kutokea.
Hatimaye waimbaji wameamka sasa na kuanza kuandaa mikutano ya injili ili kuwaleta watu kwa Yesu na sasa tunaona watu wakioklewa, wakifunguliwa magojwa yao Read More

0 comments:

HOT NEWS: HALI TETE KANISA LA MORAVIANI JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI, SASA WATAKA ASKOFU AJIUZURU. SOMA HAPA KILA KITU


 Askofu Alinikisa Cheyo anayeshinikizwa kujiuzuru.
Mchungaji Edward Chilale, Mwenyekiti wa Baraza la wazee Usharika wa Bethrehemu na mwenyekiti wa kikao kilichotoa tamko
Bonyeza Hapa kwa maelezo zaidi


Read More

0 comments:

Recent News