Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Monday, 23 June 2014

MAZISHI YA DEBORA KUFANYIKA LEO, WAIMBAJI WAFIKA KUTOA FARAJA

Joyce Ombeni pamoja na Christina Matai wakiimba msibani hapo jana.
Mazishi ya aliyekuwa mwimbaji wa muziki wa injili nchini Debora John Said ambaye pia alikuwa mama mchungaji, yanatarajiwa kufanyika majira ya saa nane mchana wa leo katika makaburi ya Makuburi jeshini jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo GK imezipata, ni kwamba ibada ya mazishi inatarajiwa kuanza majira ya saa nne asubuhi nyumbani kwa marehemu kisha msafara wa kuelekea kwenye kuupumzisha mwili unatarajiwa kuwa majira ya saa saba mchana. Toka kutokea kwa msiba huo, waimbaji mbalimbali wamefika msibani hapo kutoa faraja kwa nyimbo na wengine kufikia hatua ya kuzimia kutokana na huzuni ya kuondokewa na mwimbaji mwenzao.

Kati ya waimbaji walioimba siku ya jana ni pamoja na mwanamama Christina Matai, Victor Aron,
Marehemu Debora John Saidi.
Sarah Mvungi, Sifa John ambaye alizimia wakati akiimba kutokana na majonzi, wengine ni Joyce Ombeni, Mc Joshua Makondeko ambaye alikuwa karibu na marehemu hata wakati anaumwa kwa kumtembelea hospitalini pamoja na nyumbani akiongozana na waimbaji wenzake, lakini pia wanakwaya kutoka kanisa alilokuwa akiabudu marehemu wengi wao walizimia wakati wakiimba wimbo maalumu kwa mama mchungaji wao ambaye hawatamuona tena. 
Chini ni moja ya uhuhuda kutoka kwa mwimbaji Rungu la Yesu kama alivyouandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kumuelezea marehemu jinsi alivyofanyika baraka katika maisha yake ya huduma.


NAKUMBUKA MARA YA MWISHO ALINIPIGIA SIMU NIENDE KWENYE HUDUMA YAO AMBAYO NI BRANCH YA MAISHA YA USHINDI VINGUNGUTI KWAMNYAMANI PALE SOKONI,NIKAMSTUA BASHANDO TUKAENDA KUWASHA MOTO,NASIKITIKA KWASABABU MARA NYINGI AMEKUWA MAMA ALIYEKUWA AKINITIA MOYO SANA NA KUNIAMBIA MWANANGU RUNGU SONGA MBELE,TUMPATE WAPI MAMA KAMA HUYU TENA MAMA ANAYEJUA KUWALEA WATU KANISANI KWAKE KILA MUIMBAJI ANAKARIBISHWA BILA KUJALI UNAJULIKANA KIASI GANI,SIUMII KWASABABU AMEKUFA MAANA BIBLIA INASEMA HERI WAFU WAFAO KTK BWANA,HILA NAUMIA KWASABABU ALIKUWA MAMA MWENYE UPENDO NA KUMJALI KILA MTU HIVI TUTAMPATA WAPI MAMA KAMA HUYU TENA? NAHISI MOYO WANGU UMEKUFA GANZI NA KUFIKA MBALI ZAIDI KWA NINI MUNGU ASINGE MWACHA KIDOGO LKN BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE,MIAKA SITA ILIYOPITA MAMAYETU DEBORA JOHN SAIDI NA NA MCHUNGAJI JOHN SAIDI WALITUOMBEA MAOMBI MAZITO SANA PALE KANISANI KWAKE VINGUNGUTI BAADA YA KUFANYA TAMASHA LA GOSPEL HIP HOP,MAOMBI YALIKUWA HIVI"UWAINUE,UWAPE KIBARI WAFANIKISHE KIRO NA KIMWILI,WAPE MAGARI YAO WAPE NYUMBA ZAO NA WAPE HATA VIWANJA VYA KUJENGA" BAADA YA MAOMBI HAYO TUKIWA TUNAMTUMIKIA MUNGU MILANGO IKAANZA KUFUNGUKA WENGINE KWELI WAKAPATA MAGARI,WENGINE SASA WAMEJENGA,WENGINE SASA WANAVIWANJA NA MASHAMBA WENGINE SASA NI WATU WA KUBWA SANA...NIISHIE HAPO SINA CHA KUSEMA TUZIDI KUMWOMBEA BABA YETU MCHUNGAJI JOHN SAIDI NA FAMILIA NZIMA MUNGU AWATIE NGUVU KWENYE KIPINDI KIGUMU HIKI...JUMATATU SAA NNE ASUBUHI KATIKA KANISA LA USHINDI LILOPO MABIBO EXTENAL TUTAKUWA NAIBADA YA MWISHO YA ALIYEKUWA MPENDWA WETU,LKN MSIMBA UNAENDELEA PALE NYUMBANI KWAO MABIBO HOSTEL UKIFIKA TU PALE UWEZI KUPOTEA...TIMU NZIMA YA YESU OKOA MITAA TUTAKUWA PALE NA WEWE POPOTE ULIPO SOGEA PALE...YESU OKOA MITAA- KILA KONA YA MTAA....YOM.
 

BAADHI YA PICHA KUTOKA MSIBANI WAIMBAJI WAKIIMBA HAPO JANA
Joyce pamoja na Christina Matai wakiwa msibani kutoa faraja.
Sifa John akimsifu Mungu msibani hapo.
Sifa John akimsifu Mungu.
Makondeko, Matai, Mvungi pamoja na Ombeni wakiwa pamoja.



Mwinjilisti Sarah Mvungi akimtukuza Mungu.
Sifa John akiwa amezimia msibani hapo.
Victor Aron akiimba huku Addo November na waimbaji wengine wakiwa sambamba naye.
Joshua Makondeko akimsifu Mungu msibani hapo.
Mc Joshua Makondeko akimsifu Mungu.
Christina na Joyce Ombeni wakiimba.
Christina Matai akimsifu Mungu.

Read More

0 comments:

Friday, 20 June 2014

YALE YALE: WAZIRI MAGUFULI ANAPOTAFUTWA UBAYA....

Semi-Trela likiwa limebeba kontena likiwa limeanguka baada ya kulielemea  kwa uzito na kulivunja daraja la chuma katika barabara ya Banana-Kinyerezi maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam jana jioni. Haikuweza kufahamika mara moja lilikuwa limebeba mzigo gani na kama dereva alikuwa anajua daraja hilo ni kwa magari yenye uzito wa wastani  wa tani 7 tu au ni kiburi tu.  Hakika Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli  na jeshi lake wana kazi ya ziada kuhakikisha uzembe kama huu hautokei na haujirudii.…
Semi-Trela likiwa limebeba kontena likiwa limeanguka baada ya kulielemea  kwa uzito na kulivunja daraja la chuma katika barabara ya Banana-Kinyerezi maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam jana jioni. Haikuweza kufahamika mara moja lilikuwa limebeba mzigo gani na kama dereva alikuwa anajua daraja hilo ni kwa magari yenye uzito wa wastani  wa tani 7 tu au ni kiburi tu.  Hakika Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli  na jeshi lake wana kazi ya ziada kuhakikisha uzembe kama huu hautokei na haujirudii.


Read More

0 comments:

Friday, 13 June 2014

Waimbaji wakimsifu na kumtukuza Mungu katika mkutano wa Neno la Mungu unaoendelea katika viwanja vya EAGT-Kisima cha baraka Uyole.
Baadhi ya watu waliowahi kufika kwenye unaoendelea hadi tarehe 15 Jumapili ya wiki hii katika viwanja vya kanisa la EAGT-Kisima cha Baraka Uyole-Mbeya.
Apostle Jeremiah Anyelwisye Mwakanyelenge akizungumza na mwimbaji wa nyimbo za Injili Bony Mwaitege katika viwanja vya mkutano. Read More

0 comments:

Monday, 9 June 2014

Hiki ni kituo cha daladala cha Kabwe ambacho ni kituo kikubwa cha daladala kwa jiji la Mbeya kikiwa hakina msogamano wa magari baada ya daladala za Uyole - Sokomatola/ Stend kuuu/ Majengo kugoma
Kituo kikiwa cheupe hakina daladala yoyote ya kuelekea Uyole huku abiria hawamini macho yao
Abiria wakiwa kstika nyuso za huzuni kwa kutokuwa na usafiri wa uhakika kuwapeleka katika majukumu ya kila siku huku Bajaji zikiokoa jahazi ama ndo vile tena kuvunjika kwa pakacha nafuu ya mchukuzi
Hatimaye kufa kufana kila aina ya gari lenye uwezo na nafasi ya kubeba ilibeba abiria ikiwa inashusha na kupakia abiria katika kituo cha kabwe
Bajaji zikiwa kazini huku waendesha bajaji wakiomba hali hii iendelee hata kwa wiki baada ya kunufaika na mgomo huo

Mwenye Noah, Canter, Fuso, Pikipiki kaingiza barabara kuokoa JAHAZI baada wenye Hiace kuibip serikali

Bora kufika haijarishi uko katika usafiri wa aina gani
 Kituo cha Mwanjelwa chenye pilikapilika nyingi leo kikiwa cheupe kabisa
Watu wakikimbilia Canter ndo usafiri wa siku ya leo
Wamama wakihangaika wenye nyuso za huzuni katika vituo
Leo 9/6/2014 imekuwa ni asubuhi yenye mchanganyiko wa huzuni na furaha manung'uniko na pongezi kati ya makundi kadha wa kadha baada ya daladala kugoma kutoa huduma ya usafiri kutoka Uyole kuelekea Sokomatola, Stend kuu na Majengo kugoma kutoa huduma kwa siku ya leo

Madai yao makubwa ni kupinga njia zilizoongezwa ya kuzunguka Moondust Uhai Batist na kutokea Soweto stendi kwa gari zinazo tokea mjini kuelekea Uyole wakati zile za kutokea Uyole zinakunja kutokea Soweto kupitia njia ya Chuo kikuu cha Teku Block T na hatimaye kutokea Kabwe.

Wanadai kuwa hizo njioa zifutwe ili wapite njia kuu kusiwepo na mchepuko ama nauli ipandishwe hadi 500/= waameona hii ni njia ya kuishinikiza SUMATRA kubadilisha mfumo uliopo wa kutoa huduma hizo za usafiri

Jambo la msingi tunasaha kuwa kukua kwa jiji lazima kutalazika kuongezeka kwa njia ili kuendana na ongezeko la idadi ya magari kupanuka kwa mji si vema kuishi kwa mazoea tukubali kubadilika

Lakini ndo hivo tena wengine wananufaika na mgomo huo kwa kujiongezea kipato kama vile Bajaji Picup kubeba abiria kama unavoona kwenya picha hapo juu

Lakini hebu tuone katika sakata hili serkali itasema nini na je hawa watoa huduma watalegeza msimamo wao ama wataendelea na msimamo huo huo tutajua mwisho wake
Tutaendelea kukupa kinacho jili
 By M Eliezer
Read More

0 comments:

Wednesday, 4 June 2014

Mchungaji na mwimbaji Daniel Mwasumbi aachiwa huru baada ya kushinda rufaa kutokana na kesi tata iliyokuwa ikimkabiri
Mtoto wa Mchungaji Mwasumbi, Elizabet Daniel Mwasumbi akilia kwa furaha na kumshukuru Mungu
kwa Muujiza aliyo watendea baada ya tamko la kuachiwa huru kwa baba yake kipenzi
Apostle Jeremiah Mwakanyelenge akisalimiana na wakili Benjamini Mwakagamba ni miongoni
mwa watumishi waliohidhuria kusikiliza kesi ya mtumishi mwenzao
Mtoto wa Mwasumbi na mashuhuda wengine waliokuwa wakifuatilia kwa makini kesi hiyo

Wakili Benjamini Mwakagamba akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habri mara tu baada ya kushinda kesi

Mdogo wake na Daniel Mwasumbi mwenye shati la mistari akifuatiwa na katibu mkuu wa kanisa la Uinjilisti Mwakasole mwenye miuani wakisikiliza jambo toka kwa wakili



Hatimaye yametimia
Jaji Atuganile Ngwala aliyetumia muda wa saa 1:15 kusoma hukumu ya kesi iliyokuwwa ikimkabili Mchungaji na Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injiri hapa Nchini Mchungaji Daniel Mwasumbi

Hukumu hii ilitokana na upande wa mtuhumiwa kukata rufaa baada ya hukumu ya awali iliyomtia hatiani mtumishi wa Mungu huyo kwa kuamriwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela. Pamoja na kuchapwa viboko 12 na pia kuawajibika kulipa faini ya Tsh 20,000,000/= pindi amalizapo kutumikia kifungo hicho

Hukumu ya awali iliyopelekea Mchungaji Daniel Mwasumbi (57) kufungwa jele ilitolewa siku ya jumanne ya 2/7/2013 na mahakama ya Wilaya ya Mbeya chini ya Hakimu Gilbert Ndeuruo na serikali kusimamiwa na wakili Achiles Mulisa ambapo mahakama ilimtia hatiani kwa kosa la kukiuka sheria ya nchi kifungu cha 130 (2) e na 131 (1) sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002

Wakili wa kujitegemea aliyekuwa akimtetea Mchungaji Daniel Mwasumbi ambaye alikuwa anakabiriwa na mashitaka makubwa mawili Kubaka na Kumpa mimba mwanafunzi
ilisadikiwa kuwa Mchungaji alitenda kosa hilo kati ya mwaka 2008 hadi 2011 ambapo katika kipindi hicho alimpa mimba binti huyo Neema Ben (19) mwanafunzi wa shule ya Sekondari Itende na kubahatika kupata watoto wawili kati ya 2008 na 2011. Kilichopelekea Mtumishi wa Mungu Mwasumbi anayetamba na nyimbo kama Dhambi ni mbaya na nyingine nyingi kufungwa jela

Lakini baada ya hukumu hiyo upande wa mtuhumiwa haukuridhika na mwendo wa kesi pamoja na hukumu hiyo. Waliamua kukata rufaa 26/7/2013 na shauri lake kusomwa mahakamani 3/11/2013 chini ya wakili wa kujitegemea Benjamini Mwakagamba kutoka Dar es Salaam, wakati upandea wa Serikali ikiwa chini ya wakili Prosister Paul
Upande wa utetezi ukiwa na hoja kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa kisheria katika hukumu hiyo

Jaji Atuganile Ngwala akisoma hukumu hiyo alisema utoaji hukumu hiyo haukuzingatia vipengele muhimu vya kisheria vilivyotumika kumtia hatiani Mchungaji Mwasumbi
Katika rufaa hiyo kuna mambo kadha wa kadha ambayo yalonekana kukiukwa katika kutoa hukumu hiyo kama alivyoweza kubainisha wakili wa utetezi hivyo jaji kasema nakubaliana na wakili wa upande utetezi Mwakagamba kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kisheria katika hukumu hiyo

Kama ilivyoelezwa na wakili msomi na mwenye weredi katika kazi hiyo ya kisheria Bwana Mwakagamba kuwa muda lilipotokea tukio na liliporpotiwa kwenye vyombo vya usalama unaonekana kuchelewa na kukinzana na zaidi sana ushahidi uliotolewa mahakamani na mhanga wa tukio hilo ulionekana kujichanganya na kuonesha wazi kuwa mtuhumiwa hakutenda kosa hilo

Lakini jaji Ngwala alitoa kali yenye kuaktisha tamaa kwa upande wa mtuhumiwa pale aliposema kuwa mtu kama huyu ni mende na mtu hatari katika jamii, hivyo anastahili kudhalilishwa na kuadhibiwa. Kitu kilichifanya wote wliohudhuria kusikiliza kesi hiyo kwa upande wa Mchungaji kukata tamaa na kuinamisha nyuso zao chini

Jaji aliendelea kusoma hukumu kuwa kutokana na mwendo wa kesi husika kujikanganya kwa ushahidi na zaidi sana shahidi namba 1 mhanga mwenyewe
jaji karejea kauli yake kusema mende hafai ni hatari katika jamii na hakustahiri katika jamii kama ingethibitika na ushahidi kuthibitisha, lakini kwa kuwa  ushahidi umeshindwa kuthibitisha hilo hivyo basi mtuhumiwa ana haki kisheria ya kuachiwa huru.

Jaji Atuganile Ngwala akahitimisha kwa kusema upande wa Jamhuri chini ya wakili makini katika kazi yake Prosisteer Paul kuwa una haki ya kukata rufaa na kesi kuanza upya endapo haujaridhika na hukumu hiyo

Wakili aliyekuwa akimtetea Mchungaji Mwasumbi alisema kuwa katika rufaa ya mteja wake aliwasilisha sababu saba za kupinga hukumu hiyo ambapo alidai kuwa  hakimu wakati wa kutoa hukumu hiyo alikosea kisheria na haki muda wa kuripotiwa kwa shauri hilo kwa vyombo vya usalama na lilipotokea ulikinzana na kwamba aliegemea kwa ushahidi wa Mhanga tu.
Sababu zingine alidai kuwa hakimu aliegemea katika ushahidi  au vidhibiti ambavyo awali alivikata mwenyewe, pia alidai kuwa hakimu hakuangalia uhalisia kosa lenyewe na badala yake alionekana kutoa maoni yake binafsi.
Lakini sababu nyingine wakili Mwakagamba alisema kuwa hakimu huyo, aliegemea ushahidi ambao ulijichanganya, wendesha mashtaka  walishindwa kuwapeleka mahakamani hapo  mashahidi wa msingi katika kesi hiyo, hakimu aliegemea upande wa vyeti vya watoto wawil waliodaiwa ni wa Mchungaji Mwasumbi ambapo vyeti vilidurufiwa (photocopy) na si vyeti halisi na  mwisho hakimu huyo alitoa hukumu ambayo haikufuata mtiririko uliosahihi wa mashahidi husika.
Akizungumza na waandishi wa habari, mtoto wa Mchungaji Mwasumbi,  Elizabeth Mwasumbi alisema anamshukuru Mola kwa kumwezesha Jaji Ngwala kwa kutenda haki katika rufaa ya baba yake.
Alisema; ’Mimi na wenzangu tulikuwa na wakati mgumu sana pindi baba yetu akiwa ndani, kwani mimi niliathirika sana kiafya na kiuchumi nilishindwa kufanya shughuli yoyote kutokana na mawazo lakini namshukumuru Mungu kwa kutenda haki’.
Hata hivyo nje ya Mahakama ndugu na jamaa waliofurika kusikiliza hatma ya Rufaa hiyo waliokuwa na hamu ya kumlaki kwa furaha Mchungaji Mwasumbi ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kushindwa kutokana na Maafisa wa Magereza kumpeleka Gereza la Ruanda kukamilisha taratibu za Magereza

         Na Eliezer Masoud
             Apostle blog Read More

1 comments:

Tuesday, 3 June 2014


WANAKUALIKA KUSHIRIKA KATIKA MKUTANO MKUBWA UTAKAOFANYIKA KATIKA VIWANJA
   VYA KANISA LA EAGT KISIMA CHA BARAKA UYOLE NI KUANZIA 11-15/06/2014
       UTAKUWA NI MKUTANO WA BARAKA USIKOSE MWALIKE NA JIRANI YAKO
NJOONI TUJUMUIKE PAMOJA KATIKA NYAKATI HIZI ZA MWISHO KUMHUBIRI KRISTO KWA NGUVU  ZOTE
NA MUNGU AKUBARIKI SANA Read More

0 comments:

Monday, 2 June 2014

Rais mpya wa TEKUSO Ndugu Selemani Izack akila kiapo cha utii mbele mwanasheria wa Chuo Hon Martha Gwalema na kusaini hati ya kiapo
Makamu wa Rais Ndugu Benjamini Nehemia akiapishwa kiapo cha utii kwa nafasi hiyo ya umakamu wa raisi kwa serkali ya wanafunzi TEKUSO mbele ya Advocate  Martha Gwalema

Tunawatakia utumishi uliotukuka  Read More

0 comments:

Askofu mteule Conrad Nguvumali wa Jimbo la Rukwa
Askofu Mteule C. Nguvumali pamoja na mke wake wakati wa sherehe ya kumpongeza
Askofu Alinikisa Cheyo Askofu kiongozi wa kanisa la Moravian Tanzania ni 
miongono mwa wageni wa rasmi katika ibada hiyo

 Mch C. Mwaitebele Mwenyekiti wa jimbo la Kusini Rungwe ndiye aliyeongoza ibada
maa;lumu ya kumpongeza Askofu mteule wa Jimbo la Rukwa
Dr Tully Kassimoto makamu mkuu wa chuo Kikuu Teofilo kisanji ni miongoni mwawaheshimiwa
waliohudhuria ibada hiyo


Ni baadhi wa Wachungaji pamoja na wakristo waliohudhuria katika ibada hiyo ya kumpongeza
Askofu mteule C . Nguvumali
Apostle Jeremiah Mwakanyelenge ndiye aliyekkuwa mshereheshaji MC katika sherehe hiyo
ni mwimnaji mhubiri na ni Mc



Hii ni zawadi ya Gari ambayo alizawadiwa Askofu Mteule Nguvumali T 120 CTE Cruser
 Askofu mteule Conrad Nguvumali akipokea zawadi ya gari T 120 CTE Cruser
Askofu Mteule C. Nguvumali akiwa ndani ya gari yake akiwashukuru kwa zawadi aliyopewa
anamshukuru Mungu na anashangaa muujiza huo

Askofu mteule wa Jimbo la Rukwa Mchungaji Conrad Nguvumali ambaye ni katibu Mkuu wa kanisa la Moravian Tanzania na kwa sasa amechaguliwa kuwa Askofu Mteule katika Sinodi ya uchaguzi wa Jimbo hilo ambao ulifanyika mapema mwaka huu na kuchaguliwa kushika nafasi hiyo. Baada ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo Mch Kasitu kusataafu wadhifa huo.
Ibada hiyo maalumu ya kumpongeza Askofu huyo Mteule iliyofanyika katika Ushirika wa Chuo Kikuu Teofilo Kisanji. Ibada hiyo ilihudhuriwa na wachungaji wengi pamoja na Wakristo, ibada hiyo iliongozwa na Mchungaji  Clement Mwaitebele Mwenyekiti wa Jimbo la Kusini.

Mchungaji C. Nguvumali ambaye ameriki kwa nguvu zake zote katika kukiimarisha Chuo Kikuu cha kwanza cha Kimoravian Read More

0 comments:

Recent News