Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Saturday, 31 May 2014

MUNGU AKIKUPA KAZI YAKE,ATAKUPA NA MAELEKEZO SAHIHI.

Mtumishi Gasper Madumla.
Imeandikwa;
" Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.
Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami.
Hivi ndivyo utakavyoifanya; mikono mia tatu urefu wa safina, mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake. " Mwanzo 6:13-15

Haleluya....

Nuhu anatumwa kazi na BWANA Mungu,akipewa maelekezo sahihi kabisa.
Kazi hii haikuwa rahisi hata kidogo maana ilihitajika usikivu wa hali ya juu. Usikivu wa neno la Mungu ni IMANI,Hivyo kwa lugha nyingine kazi hii anayotumwa Nuhu ilimuhitaji Nuhu awe na imani ya hali ya juu,
Sababu kile alichokuwa akiambiwa,kilikuwa ni hakika ya mambo yatarajiwayo,ni bayana na mambo yasioonekana.

" Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. "Waebrania 11:1

Ninakuambia kwamba Nuhu alihitajika awe na IMANI sababu yale mambo aliyokuwa akiambiwa yalikuwa hayaonekani kwa macho haya ya damu na nyama,tazama ;
Safina aliyoambiwa aitengeneze ilikuwa kwa ajili ya kujiokoa na mvua kubwa,lakini kipindi kile hapakuwa na mvua wala dalili ya mvua. Hivyo ni kama vile Nuhu alionekana kana kwamba ni mtu asiye na akili,maana kipindi ambacho ni ukame yeye ndio anatengeneza Safina.

Yaani mfano wa haraka haraka,chukulia kwamba mpo kundi la watu fulani hivi katika maombi ya kuombea mvua inyeshe,kisha muongozaji maombi aseme kesho kutakuwa na mvua kubwa wakati nyakati hizo ni nyakati za ukame kweli kweli. Kisha mmoja wenu aje na mwamvuli siku ya kesho,maana aliamini neno la kiongozi wa maombi.
Ukweli ni kwamba wengine hawatakuja na miamvuli,na yamkini watamshangaa yule aliyekuja na mwamvuli.
Sasa,
Aliyekuja na mwamvuli wakati wa kiangazi ndie mwenye IMANI.
Mazingira ya mtu huyu,yanataka kufanana na Nuhu.

Haleluya...

Leo tunasoma kwamba Nuhu anapewa kazi ya kutengeneza safina,lakini Mungu anahakikisha anampa maelekezo yakinifu juu ya safina.
Mungu angeliweza kumwambia Nuhu atengeneze safina pasipo maelekezo yoyote,lakini Bwana Mungu hakufanya hivyo sababu ulikuwa sio mpango wake. Bwana Mungu anampa Nuhu maelekezo yote ya jinsi safina itakavyokuwa.

Kwa lugha nyingine ni kwamba safina ile,Bwana Mungu alishaiona,na kuijua kabla hata ya kutengenezwa, ndipo anampa maelekezo yote Nuhu aifanye jinsi ipasavyo.
Laiti kama Nuhu asingepewa vipimo na mahitaji yote,yamkini angetengeneza lakini isingelifanana na safina ile ya Mungu. Ona katika hilo andiko hapo juu,BWANA Mungu anampa na vipimo sahihi vya hilo safina.

Haleluya....
Bwana Yesu asifiwe sanaa...

• Mungu hawezi kukutuma kazi pasipo kukuelekeza kwa usahihi juu ya kazi hiyo.
• Maelekezo na vipimo vya kazi hiyo vipo tayari kwa yule aliyetumwa kuifanya kazi ya Mungu.

Hata tunapomuangalia Musa,tutagundua kwamba maisha yake ya utumishi yote yalikuwa yanaongozwa na maelekezo sahihi kwa kila kazi aliyopewa na Mungu,kuanzia kuitwa kwake katika utumishi hadi kuwaendea ndugu zake huko Misri.

Tazama tu hata pale alipowaendea ndugu zake huko Misri,BWANA Mungu hakumuacha aende peke yake,na ndio maana alihitaji USO WA BWANA uende pamoja naye,tena alizidi kuumpa maelekezo sahihi,
Napapenda pale alipoambiwa aitumie ile fimbo kugawanya bahari,nao wana wa Israeli wapite,
Tunasoma;

" Nawe inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya bahari, na kuigawanya; nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu. " Kutoka 14:16

Haya nayo yalikuwa ni maelekezo makubwa sana.

Nasi tunahitaji sana kuyasikia maelekezo ya Roho mtakatifu kwa kazi ya Bwana tuzifanyazo,sababu wenyewe hatuwezi kufanya kwa akili zetu,maana si kazi yetu,bali ni kazi ya Bwana.
• Kama tukishindwa kuyasikia maelekezo ya Mungu kwa usahihi wake,basi kazi tuzifanyazo ni bure.

Unafikirije?
Kama Musa,Nuhu wasingeisikiza kwa makini sauti ya Bwana Mungu wangefaulu?

*Wengi tunafeli kwa kushindwa kuisikiza sauti ya Mungu.

Mfano mdogo tu ni huu;
Chukulia liwapo kundi la wanamaombi sehemu fulani,na kama vile ujuavyo kuwa maombi ni silaha katika ulimwengu wa roho na wa mwili pia,sasa watu hawa wanapoongozwa na kiongozi wa maombi waombee ombi fulani,mfano kiongozi anaweza sema " tuombee kwa kumsukuru Bwana Mungu tu "
Sasa hapo ndipo kazi inaanza:
Utakuta kila mmoja ameelekeza silaha yake juu,wengine kweli wataanza kushukuru kama kiongozi alivyosema,na wengine wataanza maombi ya kuvunja,kuteketeza na kuharibu kinyume na neno la kiongozi.

Watu hawa kama ukiwaona katika ulimwengu wa kiroho,utaona risasi zikipigwa bila mpangilio,maana nyingine zitapigwa juu,nyingine chini,nyingine zitapigwa pembeni, Yaani hawakuweza kulenga sehemu moja sababu ya KUTOKUISIKIZA KWA BIDII SAUTI YA BWANA n.k

Siku zote Bwana Mungu husema nasi kwa njia tofauti tofauti,akitutuma kazi na kutupa maelekezo sahihi.

• Kama ukifanya kazi ya Mungu pasipo maelekezo,kazi hiyo itakuwa ngumu.
• Ukiona huna maelekezo yoyote ujiulize,kwamba hiyo ni kazi ya Mungu aliyokutuma ? Au ni kazi yako mwenyewe uliyotumwa?

Ngoja tuangalie katika ujio wa Yesu Kristo akiwa Bwana na mwokozi wetu.
Mitume wote hawakufanya kazi yake Bwana,pasipo kuelekezwa namna ya kufanya, tazama hapa;

" Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. " Matendo 1:4&8

Mitume wanaambiwa wasikwende mahali popote pale wakifanya huduma,mpaka wapokee ahadi ya Roho mtakatifu. Haya ni maelekezo sahihii kabisa kabla ya kufanya hiduma.

Huduma ya kina Petro ilikuwa ni huduma yenye nguvu sana,udhihirisho wa kazi ya Roho mtakatifu ulionekana sababu,si wao walifanya bali Roho alikuwa kazini,kwanza kwa maelekezo sahihi.

• Leo hii,ipo shida katika huduma tuzifanyazo.
• Wengi tunapenda huduma pasipo kupenda kusikiza sauti ya maelekezo ya Roho mtakatifu.
• Mungu atusaidie sana, ndio maana huduma inakuwa ngumu sana,kiasi kwamba mpaka unajiuliza kwamba " hii ni kazi ya Mungu kweli?"
• Tunahitaji kusikia zaidi,kabla ya kufanya.

Read More

0 comments:

Thursday, 29 May 2014

UHARIBIFU WA MAGHUBA CHANZO CHA TAKA MBEYA

Baadhi ya wananchi wakiwa wanaendelea kutoa takataka nje ya Ghuba na kuziweka katika sehemu husika ukiwemo na Mzoga wa Mbwa .



MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Mussa Zungiza, amesema tatizo la uchafu uliopo katika maeneo mbalimbali Jijini umetokana na kuharibika kwa maghuba kumi ya kuzolea taka.
Zungiza alisema chanzo cha kuharibika kwa maghuba hayo kumetokana na watumiaji wa maghuba hayo kuchoma taka ndani ya maghuba hayo ali inayopelekea kupasuka na kuvujisha taka.
Alisema kutokana na kuharibika kwa maghuba hayo maeneo mbalimbali yameathirika na kusababisha wananchi kutupa taka chini na kwamba magari yaliyopo kwa ajili ya kuzoa taka ni machache hivyo kuleta mrundikano wa taka kwa muda mrefu na kuwa kero kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kutupa taka.
Mkurugenzi alisema tangu amefika Jijini Mbeya ameweza kukarabati maghuba sita yaliyokuwa yameharibika na sasa maghuba kumi yameharibika hivyo wako mbioni kukatabati pindi utaratibu wa serikali katika manunuzi kukamilika.
Alisema  kutokana na uzalishaji mkubwa wa taka unaotokana na ungezeko la wakazi na viwanda wameagiza maghuba mengine 84 yatkayoondoa kero ya muda mrefu ya mrundikano wa taka Jijini Mbeya.
Aidha alisema hivi sasa wanajitahidi kuzoa kwa kutumia magari yaliyopo ingawa yanalemewa na uwingi wa taka katika Kata 36 za Jiji ni magari matatu tu yanayofanya kazi kila siku hivyo baadhi ya maeneo ya masoko kutopitiwa mara kwa mara na magari hayo.
Aliongeza pia mkakati wa Serikali ni kuongeza magari mengine ya kuzolea taka sambamba na marekebisho ya magari ya kisasa ya kuzolea taka ambapo mazungumzo ya awali baina ya Jiji na Wahisani kutoka China yanaendelea vizuri.
Kwa upande wake Afisa Usafishaji Jiji la Mbeya Samwel Bubegwa alisema kuwa mbali ya mikakati hiyo Halmashauri ya Jiji inakusudia kubinafsisha shughuli za usafi kwa vikundi vya vijana vitakavyokuwa na jukumu la usafi katika kila Kata hivyo kuongeza ajira kwa vijana katika kila Kata.
Bubegwa alisema utafiti uliofanywa katika Kata ya Iyunga umeonesha mafanikio makubwa hivyo mbali ya kutoa ajira utaboresha usafi katika maeneo yote kutokana na vikundi hivyo kuwa karibu ya wananchi.
Afisa huyo alisema hivi sasa vijana katika kila Kata wajiunge ili kuanzisha vikundi hivyo kwani Jiji litatoa tenda kwa vikundi na si mtu binafsi ili vijana waondokane na tatizo la ukosefu wa ajira.
Mkurugenzi Mussa Zungiza amemaliza kwa kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jiji la Mbeya kwa kufuata taratibu za usafi ikiwa ni pamoja na kuacha kutupa samadi katika maghuba na mizoga hali inayohatarisha afya za wakazi wanaoishi karibu na maghuba kuwa hatarini na magonjwa yanayotokana na hewa.
Read More

0 comments:

MAYA ANGELOU, AFARIKI DUNIA

 
Mwandishi wa vitabu na mwanaharakati mashuhuri wa Marekani,Maya Angelou enzi za uhai wake.
Akiwa mmoja wa waandishi maarufu zaidi kwa miaka 50, Angelou anajulikana zaidi kwa kitabu chake cha mwaka 1969, I Know Why the Caged Bird Sings. Kilikuwa ni kitabu cha kwanza kati ya saba ya vitabu kuhusu maisha yake kuanzia mateso aliyopata miaka ya 1930s.
I Know Why the Caged Bird Sings, kilichoandika kuhusu ubaguzi wa rangi na mateso ya familia wakati akikua kilikaa miaka miwili kwenye orodha ya vitabu vilivyouza zaidi. Vitabu vyake vingine ni pamoja na Just Give Me a Cool Drink of Water ‘fore I Diiie (1971), And Still I Rise (1978), Now Sheba Sings the Song (1987), na I Shall…
Mwandishi wa vitabu na mwanaharakati mashuhuri wa Marekani,Maya Angelou enzi za uhai wake.
Akiwa mmoja wa waandishi maarufu zaidi kwa miaka 50, Angelou anajulikana zaidi kwa kitabu chake cha mwaka 1969, I Know Why the Caged Bird Sings. Kilikuwa ni kitabu cha kwanza kati ya saba ya vitabu kuhusu maisha yake kuanzia mateso aliyopata miaka ya 1930s.
I Know Why the Caged Bird Sings, kilichoandika kuhusu ubaguzi wa rangi na mateso ya familia wakati akikua kilikaa miaka miwili kwenye orodha ya vitabu vilivyouza zaidi. Vitabu vyake vingine ni pamoja na Just Give Me a Cool Drink of Water ‘fore I Diiie (1971), And Still I Rise (1978), Now Sheba Sings the Song (1987), na I Shall Not Be Moved (1990).
Shairi lake ‘On the Pulse of the Morning’ lililoandikwa kwaajili ya sherehe ya kuapishwa kwa Rais Bill Clinton liliwagusa wengi na kuuza kopi zaidi ya milioni moja Marekani. Alipewa pia kazi ya kuandika mashairi kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Mataifa mwaka 1995 na alimkumbuka Nelson Mandela kwenye shairi kwaajili ya ikulu la Marekani mwaka jana.
Angelou pia aliongoza filamu Down in the Delta, iliyoshinda tuzo tatu za Grammy kwa album ya maneno ya kuongea.
Read More

0 comments:

Wednesday, 28 May 2014

MREMBO ANASWA NA NGUO ZA KUAMBIANA

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
AMA kweli duniani kuna sarakasi! Takribani siku kumi tangu alipofariki dunia aliyekuwa ‘kichwa’ kwenye filamu za Kibongo, Adam Phillip Kuambiana (38), mrembo aliyejitambulisha kwa jina Mary Njombe amenaswa na nguo za staa huyo wakati mali za marehemu hazijagawanywa.
Mary Njombe aliyenaswa akiwa amevaa nguo za marehemu Adam Phillip Kuambiana.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Mary ambaye ni mkazi wa Magomeni Hospitali, Dar amekuwa akipigilia pamba za marehemu hasa baada ya jamaa huyo kutangulia mbele ya haki.
“Jamani njooni huku Magomeni Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga nguo za marehemu Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walifanya msako eneo hilo hadi wakamnasa Mary.
Katika mahojiano na gazeti hili, Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa Kuambiana na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara ya mwisho amfulie (zinaonekana pichani).
Mary alisema kuwa yeye na Kuambiana walifahamiana tangu mwaka 2006 ambapo alikuwa akimbembeleza kuwa naye.
“Mwaka 2008 ndiyo tulianza rasmi uhusiano kwani mimi nilikuwa sina mwanaume na yeye hakuwa na mtu hivyo tulikubaliana na alikuwa akijulikana nyumbani kwetu,” alifunguka Mary.
Mwanadada huyo alisema kuwa yeye na Kuambiana walikuwa wakikutana kwenye Hoteli ya Grand iliyopo Magomeni, Dar na mara nyingi alikuwa akimpikia chakula na kumpelekea ‘lokesheni’.
“Nimeumia sana na sijielewi, Kuambiana ameniachia donda kubwa, nakumbuka neno la mwisho aliniambia nimpende sana kwani ipo siku nitamkubuka,” alisema Mary huku akiangua kilio.
Adam Phillip Kuambiana enzi za uhai wake akiwa amevaa shati alilonaswa nalo mrembo.
Alipoulizwa kama kweli nguo hizo ni za marehemu Kuambiana, alizama ndani akatoka akiwa amevaa pensi na shati la ‘drafti’ alilokuwa anapendelea kulivaa staa huyo ambalo ni maarufu sana.
Kuambiana alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 17, mwaka huu baada ya kuanguka chooni kutokana na kusumbuliwa vidonda vya tumbo.
Chanzo cha Habari: www.globalpublishers.info

 

BABA AMUUA KWA MAWE BINTIYE MJAMZITO KWA KOSA LA KUOLEWA NA ASIYEMTAKA

Mwili wa marehemu Farzana ukiwa chini pembeni yakiwa matofali yaliyotumika kumshambulia.

Wakati Meriam anasubiri kutekelezwa kwa adhabu yake kifungoni huko nchini Sudan, habari nyingine kutoka nchini Pakistan zinasema polisi nchini humo wamemkamata baba mmoja kwa kosa la kumuua binti yake wa kumzaa kwa mawe akishirikiana na familia nzima yenye jumla ya watu takribani 20 kwa kosa la binti yake kuolewa na mwanaume asiyetakiwa na familia.

Marehemu ametambulika kwa jina la Farzana Parveen (25) inadaiwa alikuwa mjamzito wa miezi mitatu wakati ambao kaka zake, baba yake na ndugu wengine walipowashambulia kwa mawe yeye na mumewe aitwaye Mohammad Iqbal (45) majira ya mchana mbele ya mahakama kuu ya mjini Lahore nchini humo.

Kwa mujibu wa mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu mkazi wa Pakistani aitwaye Zia Awan amesema hajawahi kusikia aina ya kesi kama ya Farzana kupigwa mawe hadi kifo, mbaya zaidi tukio hilo limefanyika mbele ya mahakama amesema Zia akizungumza na The Associated Press. Naye kwa upande wa baba mzazi wa marehemu Mohammad Azeem ambaye amemfungulia kesi mwanaume aliyefunga ndoa na binti yake bila ridhaa yake licha ya kwamba walikuwa wachumba kwa miaka kadhaa, ameonyesha kutojutia kitendo alichokifanya "Nimemuua binti yangu kwakuwa ameidhalilisha familia nzima kwakuolewa na mwanaume ambaye hakuwa na ridhaa yetu, sijutii kitendo nilichokifanya" amesema mzee Azeem.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa shirika la habari la AP linasema kumekuwa na vitendo vya adhabu za
Mume wa marehemu akiwa na mwili wa mkewe kwenye gari la wagonjwa.
kupigwa mawe katika taifa hilo la kiislamu la Pakistan kwasehemu kubwa kutokana na wanawake kutaka kuolewa kutokana na upendo ama mapenzi kwa ampendaye bali kwa kuchaguliwa mtu wa kuolewa naye jambo ambalo baadhi ya wanawake hawalitaki na kujikuta wakipoteza maisha namna hiyo.
Na katika kuonyesha kwamba vitendo hivyo haviwezi kuisha ni kutokana na adhabu nyepesi wanazopewa watu wanaokamatwa kwa kosa la kuua wenzao kwa kuwarushia mawe. Aidha Awan amesema linapotokea jambo kama hilo polisi hawafanyi uchunguzi kwa makini na kusababisha mahakama kutoa adhabu nyepesi kwa watuhumiwa.

Mapema mwezi wa April, wanandoa wa Kikristo nchini humo walihukumiwa kifo kwakosa la kuukashifu uislamu kwakupitia ujumbe wa simu za mkononi. Licha ya mwanasheria aliyekuwa akiwatetea wanandoa hao kwamba ujumbe huo haukutoka kwao kwakuwa hawajui kusoma wala kuandika lakini utetezi wake haukusikilizwa. Wakristo huishi katika matatizo mazito nchini Pakistani kwakufuatiliwa na polisi, kupelekwa vifungoni na wengine kuhukumiwa kifo.

 

MWANAMKE ALIYEHUKUMIWA KIFO SUDAN AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE GEREZANI

Meriam na mumewe Daniel siku ya ndoa yao.

Habari kutoka Khartoum nchini Sudan zinasema mwanadada Meriam Ibrahimu ambaye amehukumiwa kuchapwa bakora 100 na adhabu ya kifo kwa kosa la kubadili dini na kuwa Mkristo, amejifungua mtoto wa kike jana asubuhi, akiwa jela anakosubiria kutekelezwa kwa adhabu yake.

Meriam ambaye pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye miaka takribani miwili, wako pamoja jela toka mwezi february mwaka huu toka amekamatwa akidaiwa kuikana imani yake ya kiislamu na kuwa Mkristo, jambo ambalo Meriam analipinga kwakuwa licha ya baba yake kuwa mwislamu lakini amelelewa katika mazingira ya Kikristo toka akiwa mdogo na kwamba hakubadili dini alipoolewa na Dkt Daniel bali alikuwa Mkristo toka udogoni.

Licha ya utetezi wake huo, mahakama nchini humo imemtia hatiani mwanadada huyo mwenye miaka 27 kwakuwa ndoa yake haitambuliki kwa mujibu wa sheria za kiislamu na kwamba ameshiriki uzinzi katika kupata watoto wake hao. Meriam alipewa mda wa kujifikiria na kurudi kuwa mwislamu ili kuondolewa adhabu ya kifo, lakini hakufanya hivyo na kushikilia msimamo wake wa kuwa Mkristo, jambo ambalo lilipelekea hakimu Abbas kumuhukumu kifo na bakora 100, adhabu ambazo atazitumikia mara baada ya kujifungua.

Kwa mujibu wa mumewa dkt Daniel amesema mkewe amefungwa kwa mnyororo miguuni na hali yake imedhoofika huko gerezani. Hata hivyo tayari mashirika na mataifa mbalimbali wameitaka Sudan kumwachilia mwanamke huyo na kuwapa watu uhuru wa kuabudu wanachokipenda. Endelea kumuombea Meriam.
Bonyeza hapa kuona taarifa ya habari ikielezea tukio hilo Read More

0 comments:

Tuesday, 27 May 2014

  Bonyeza hapa kusikiliza JP Radio FM...Nyote mnakaribishwa

KING KIKI: KILA SIKU NASALI BABU SEYA AACHIWE


MWANAMUZIKI mkongwe katika muziki wa dansi nchini, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ amesema huwa anasali kila siku kumuombea mwanamuziki mahiri nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Pakii Kocha’ waachiwe kutoka gerezani.
Mkongwe katika muziki wa dansi nchini, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ akisisitiza jambo katika ofisi za Global Publishers.
Nguza na mwanaye wapo kwenye Gereza Kuu la Ukonga jijini Dar es Salaam wakitumikia kifungo cha maisha kufuatia kupatikana na hatia ya kulawiti watoto 10 katika hukumu iliyotolewa Juni 25, 2004,  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Katika mahojiano na Live Chumba cha Habari Alhamisi iliyopita, King Kiki alisema anamuombea Babu Seya kwa Mungu kwa sababu bila yeye asingekuwa Tanzania na kuimbia Bendi ya Marquis Du Zaire.
Kiki alisema wakati anatunga mtindo wa Kamanyola Bila Jasho, Babu Seya ndiye alikuwa akikung’uta gitaa la solo na akajipatia umaarufu mkubwa hadi kupewa cheo cha kijeshi cha Field Marshal wa solo. Baadhi ya mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwandishi: Kwa maoni yako unadhani Nguza au Babu Seya walifanya makosa waliyohukumiwa nayo?
Kiki: Binafsi kwa jinsi ninavyomjua Babu Seya, naamini hakufanya, alionewa na ipo siku yanaweza kutokea maajabu akaachiwa huru.
Mwandishi: Unaamini katika miujiza?
Kiki: Naamini miujiza ipo na huwa inatokea sana duniani.
Mwandishi: Ulitunga mtindo wa Kamanyola ukiwa na Bendi ya Marquis Du Zaire, nini maana ya mtindo huo?
Kiki: Kamanyola ni mji kule DRC Kongo, sasa mimi niliongeza Bila Jasho kwa maana kuwa mchezaji wa muziki huo atacheza taratibu kwa raha zake. Nilitunga mtindo huo baada ya kujiunga na bendi hiyo mwaka 1977.
Mwandishi: Ulianza kuimba muziki wa dansi mwaka gani? Halafu tupe historia yako kwa ufupi.
Kiki: Kwanza kabisa, nilizaliwa mwaka 1947. Nilianza kuimba mwaka 1962 baada ya kuacha masomo nikiwa sekondari kwa sababu muziki uliniingia katika damu.
“Nilijiunga na Bendi ya Fouvette kabla ya kubadilishwa jina na kuitwa Safari Nkoi. Tuliingia Tanzania na bendi hiyo chini ya Fred Ndala Kasheba miaka ya 1970.
“Baadaye tulirudi nyumbani Lubumbashi (DRC) lakini mwaka 1977 nilikuja tena Tanzania na kujiunga na Bendi ya Marquis kabla ya kuiacha na kujiunga na Orchestra Safari Sound, nikaanzisha mtindo wa Masantula Ngoma ya Mpwita.
“Hata hivyo, mwaka 1983 nilianzisha bendi yangu ya King Kiki Double O na mtindo wa Embalasasa Shika Breki.
“Bendi hiyo ilikufa kutokana na uchakavu wa vyombo, nikaongoza kwa muda Bendi ya Sambuluma na Nguza lakini mwaka 1994 nikiwa na marehemu Ndala Kasheba tukaanzisha Bendi ya Zaita Musica.
“Mwaka 2003 nikiwa na Ndala huyohuyo tukaanzisha Bendi ya Wazee Sugu La Capital. Bahati mbaya mwenzangu Kasheba akafariki dunia mwaka mmoja baadaye, yaani 2004, lakini mpaka sasa nina bendi mbili, moja ipo Mwanza.”
Mwandishi: Una historia ndefu. Je, unaweza kutueleza mafanikio yako katika muziki?
Kiki: Namshukuru Mungu nina mafanikio ya kawaida, nina nyumba Temeke Wailes (Dar), nina watoto saba, walikuwa tisa wawili  walishafariki dunia.
“Nina mke Mtanzania na bendi hizo mbili. Niliwahi kwenda Uingereza tulipata mwaliko na mwaka 2011 tulienda Marekani tulialikwa katika sherehe ya miaka hamsini ya uhuru wetu na nashukuru Bendi ya Wazee Sugu. Mimi kwa sasa ni Mtanzania nilipata hati hiyo mwaka 1997.
Mwandishi: Kwa nini uliamua kuishia Tanzania?
Kiki: Ni ukarimu wa Watanzania. Nilipofika hapa mara ya kwanza mwaka 1970, niliona watu ni wakarimu sana, nikaamua kurudi mwaka 1977 na nikaamua kuishi hapa.
Mwandishi: Mpaka sasa umetunga nyimbo ngapi?
‘King Kiki’ akikumbushia waandishi wa Global Publishers wimbo wa kitambaa cheupe.
Kiki: Nimeshatunga nyimbo nyingi, hamsini kwenye Bendi ya Marquis na ishirini Safari Sound. Kuna wakati nilikuwa na uwezo ndani ya wiki mbili kutunga nyimbo ishirini.
“Baadhi ya nyimbo zilizotikisa ni Kyembe, Safari Yetu Mbeya, Nasema Sina Ndugu, Msimamo wa Nyerere, Noele (Krismas), Haruna Kaka na kadhalika.
Mwandishi: Kuna tetesi kwamba ulikuwa na mpango wa kumuoa mwanamuziki Ngalula enzi hizo. Je, kuna ukweli?
Kiki: Hapana. Ngalula alikuwa mcheza shoo wa Marquis na mwenzake Frida. Alikuwa na uhusiano na mpiga solo wetu Bizo Matuka na ndiye aliyemuoa, ni mke na mume hadi leo.
Mwandishi: Miaka yote nakuona unaimba. Je, kupiga ala za muziki huwezi? Na kati ya watoto wako kuna aliyefuata nyayo zako?
Kiki: Naweza kupiga magitaa yote lakini huwa napendelea kuimba kwani hata waswahili walisema kila ndege na mti wake. Katika watoto wangu, Veronica Kikumbi amefuata nyayo zangu, huwa naimba naye, hata ule wimbo wa Fungua Njia nimerekodi naye.
Mwandishi: Nini kifanyike ili kuinua muziki wa dansi unaoonesha kuporomoka nchini?
Kiki: Kama angepatikana mdhamini, tukarekodi upya nyimbo zilizovuma na zikatangazwa, kukafanyika onesho, maajabu makubwa yataonekana.
Mkongwe katika muziki wa dansi nchini, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ akiwa na wahariri wa Global Publishers.
Siku hizi tunatunga nyimbo nzuri lakini hazipigwi kwenye vituo vya redio na tv, hivyo watu hawajui kinachoendelea na muziki unaporomoka.
Mwandishi: Kuna mwanamuziki kijana anaitwa Diamond anafanya vizuri, unamshauri nini?
Kiki: Ni kweli kijana huyu ana nyota ya muziki na anakubalika. Namshauri asilewe sifa, afuate miiko ya muziki, atapaa zaidi.
Mwandishi: Upo tayari kufanya kazi na mwanamuziki yeyote wa kizazi kipya?
Kiki: Huwa nafanya nao kama vile Joh Makini na nduguye, nilifanya naye muziki na hata MwanaFA. Wote nawakaribisha, nipo tayari kuwasaidia uzoefu wangu.
Mwandishi: Katika muziki, nini unakikumbuka?
Kiki: Ni safari yetu ya Tanga miaka ya 1980, Bendi ya Atomic ilitupokea vizuri sana lakini pia siku hiyo tulizindua OSS na mtindo wetu wa Masantula pale Safari Resort, watu walijaa sana na walinishangilia sana. Sizisahau siku hizo kwani Ibrahim Sembreno mwenyeji wetu alitupokea vizuri.
Mwandishi: Kwa sasa watu wakitaka kuona shoo yako unapatikana wapi hapa Dar?
Kiki: Tunapiga Whips Bar kila Ijumaa, Jumamosi tunakuwa La Prima, Victoria na Jumapili Shekina Bar, Mbezi Beach.
Chanzo Cha Habari : www.globalpublishers.info  Read More

0 comments:

Monday, 26 May 2014

 

Bonyeza hapa kusikiliza JP Radio FM...Nyote mnakaribishwa

 HOJA YA UCHAWI KANISANI; ONGEZEKO LA IMANI ZA UCHAWI MAKANISANI TANZANIA


Nafasi ya Tanzania katika uchawi kimataifa

Askofu Sylvester Gamanywa
Tafiti zilizofanywa na vyombo vya kimataifa vya habari na utafiti zimeipandisha daraja Tanzania na kushika nafasi ya kwanza kwa umahiri wa kuamini katika uchawi kimataifa. Mojawapo ya taasisi zilizoitangaza Tanzania kwamba imekithiri kwa mambo ya uchawi ni Pew Research lenye makao yake Washington DC nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa zake inasadikiwa kwamba miongoni mwa nchi 19 za Kusini mwa Jangwa la Sahara ya Afrika zilizofanyiwa utafiti, Tanzania imeongozwa kwa kuwa idadi ya watanzania 93% wanaoamini katika uchawi. Nchi ya pili inayoifuatia Tanzania ni Cameroon ambayo idadi ya washirikina wake ni 78%. Wakati huo huo nchi jirani ya ikiwemo Uganda yenyewe ina 29%, ikifuatiwa na Kenya yenye 27%
Vitendo vya uchawi vinavyoongoza kwenye uchawi ni pepo wachafu, juju, matamko ya laana za kichawi, na ufundi wa kutoa dawa za kinga dhidi ya kulongwa na kuthamini sana utoaji wa kafara kwa mizimu.
Chombo kingine ambacho kilifanya utafiti wake ni CNN kwa kufanya mahojiano mbali mbali kutangaza kwamba, 60% ya watanzania waliohojiwa wanaamini katika utoaji wa kafara kwa mizimu au pepo wachafu kwa imani ya kujikinga kutoka na vitisho vya kulogwa, na ikaongeza kusema kwamba waumini wengi wa dini za Kikristo na Kiislamu, pamoja na kuhudhuria kwa wingi kwenye majengo ya ibada; bado wengi wao wameshkilia imani za kienyeji za kiafrika.
Salum Khalfani Bar'wani ndiye mbunge wa kwanza kuchaguliwa kutoka jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi ©CNN
Chombo kingine ambacho kilifanya utafiti wake ni CNN kwa kufanya mahojiano mbali mbali kutangaza kwamba, 60% ya watanzania waliohojiwa wanaamini katika utoaji wa kafara kwa mizimu au pepo wachafu kwa imani ya kujikinga kutoka na vitisho vya kulogwa, na ikaongeza kusema kwamba waumini wengi wa dini za Kikristo na Kiislamu, pamoja na kuhudhuria kwa wingi kwenye majengo ya ibada; bado wengi wao wameshkilia imani za kienyeji za kiafrika

Madhumuni ya makala

Kutokana na matukio yanayoendelea katika jamii kwa jumla; na wakati huo huo nikiangalia upande wa huduma za kikanisa; nimeshawishika kuamini kwamba, jamii inapovamiwa na wimbi au janga fulani, maana yake hata kanisa nalo huathiriwa kwa njia moja au nyingine. Takwimu zimeonesha kwamba 93% ya watanzania wote wanaamini katika uchawi! Tena ikasisitizwa kwamba “idadi kubwa ya wafuasi wa dini za Kikristo na Kiislamu wanaishi katika maisha ya ushirika na uchawi!
Pamoja na kwamba, taarifa hizi zilikwisha kusambazwa hapa nchini katika miaka ya hivi karibuni, bado sina hakika kama kweli watanzania walio wengi wameshafikiwa na habari hizi! Tena mashaka yangu makubwa yako kwa upande wa waumini wa madhehebu ya Kikristo; hususan yale ya mlengo wa kipentekoste na uamsho wa karimatiki pamoja na wafuasi wa vuguvugu la itikadi za mitume na manabii; sijui kama wanazo taarifa hizi. Na kama zimewafikia bado sioni juhudi za makusudi katika kutafuta ufumbuzi wa kweli wa kulinusuru taifa la Tanzania na “janga hili na imani za uchawi”. Badala yake ninaona kinyume chake tu! Naliona kanisa ambalo linalotegemewa na jamii ya wasioamini kuonesha njia ya kutokea kupitia mamlaka ya Kristo; badala yake lenyewe ndio linapoteza mwelekeo wa kiimani na kimafundisho ya kweli ya kibiblia.
Nasema haya kwa sababu kwa uchunguzi wangu; mpaka hivi sasa ninapoandika makala haya, ziko dalili za waziwazi kwa baadhi ya makanisa kupoteza ujasiri wa kiroho na kuruhusu ushirikina kujikita kanisa. Baadhi ya dalili zenyewe ni pamoja na kuongezeka kwa: i) Hali ya kutukuzwa utendaji wa nguvu za Ibilisi kwa waumini badala ya ujazo wa nguvu za Roho Mtakatifu; ii) Hali ya waumini kujengewa mtazamo potofu wa madai kwamba wachawi ndio wanaofanikiwa kiuchumi!
Pengine hujanielewa ninachosema. Nikupe mfano mdogo. Hivi sasa, bila shaka utakuwa umeshasikia kwamba, baadhi ya watu wanaoonekana katika jamii wamefanikiwa kiuchumi na huku wakiwa ni waamini wacha-Mungu; hawa wanatafsiriwa kuwa ati wamefanikiwa kiuchumi na ndumba za “freemason”! Kana kwamba hii haitoshi, kila kiongozi au mtumishi wa Mungu ambaye anafanya huduma na anapata wafuasi wengi, naye pia anatafsiriwa kuwa mafanikio yake ni matunda ya “freemason”! Huu ndio mtazamo ndani ya baadhi ya makanisa! Hii imani ndiyo imani inayopandikizwa na kutukuzwa kwenye majengo ya ibada! Kwa bahati mbaya, pengine wahusika bila kujua athari zake, wanapoendelea kutukuza habari za freemason kupita kiasi matokeo yake ni kama ifuatavyo:
  1. Washirika wanapojengewa imani potofu kwamba mcha Mungu “hawezi kufanikiwa kiuchumi” isipokuwa mafanikio hayo yanatolewa na “freemason”;! Tayari hii “injili ya freemason” inapata ushawishi ndani ya kanisa tena kwa waamini wachanga, na dhaifu wa imani, ambao huamua kuisaka hiyo “freemason” ili wafanikiwe kiuchumi!
  1. Imani hii potofu inajenga na kufuga tabia ya uvivu makanisani ambapo washirika wanaacha kufanya kazi kwa bidii ili wajikwamue kiuchumi; badala yake wanabaki kuwa “tegemezi wa maombezi” tu, huku wakuzunguka zunguka kwenye vituo vya maombezi ili kuvunja “laana za umaskini”! Wakati ukweli wa mambo, kwa maisha yao wenyewe; wameufungulia mlango umaskini kwa uvivu wao wenyewe!
Kwa kusema haya, sina maana kwamba, ninakataa kuwepo kwa uchawi na wachawi. Na wala sipingani na dhana nzima ya kukemea pepo wachafu kuwaachia watu huru ikiwa ni pamoja na mizimu ya uchawi. Ninatambua na kutekeleza agizo kuu la Yesu Kristo aliposema “kwa jina langu watatoa pepo”!
Madhumuni ya makala haya, ni kuelimisha, kutahadharisha na kuonya kwa upendo na upole, kanisa halisi lirudi kwenye wito wake na lionesha mamlaka ya Kristo aliyoliachia; na sio kutangaza sifa na nguvu za uchawi kuwa ndizo zina uwezo wa kufanya mambo makubwa na mazuri!

Tafsiri ya misamiati ya uchawi

Katika mwanzo wa kuelimisha kwangu hebu kwanza tuanze na uchambuzi wa misamiati ya maneno yatakayotumika sana kupitia makala haya.Baadhi ya manenp yafuatayo yatatumika sana ambayo ni i) mchawi ii) uchawi iii) mwaguzi iv) uaguzi v) mnajimu vi) unajimu. Vii) mshirikina viii) ushirikina. Ni imani yangu tukijua tafsiri ya maneno haya tutalielewa vema somo hili na kupata ufumbuzi wa matatizo yatokanayo na matumizi ya maneno haya.
Kwa mujibu wa tafsiri ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu, neno ‘mchawi’ limetafsiriwa kuwa ni mtu anayesadikiwa kuwa anaweza kuwadhuhuru watu kwa kuwaroga; mlozi, kahini. Halafu tafsiri ya neno ‘uchawi’ limefafanuliwa katika sehemu kuu mbili zifuatazo: Kwanza ni ‘ufundi wa kutumia dawa au vitabu maalum vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe; au juju. Pili ni ‘vifaa vinavyotumika katika shughuli za kurogea’.
Kutokana na tafsiri za maneno haya mawili ya ‘mchawi’ na ‘uchawi’ tunapata picha kwamba utamaduni wa lugha ya kiswahili unatambua na kukubali kuwepo kwa hali, vitendo na imani za kichawi.
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu neno ‘Mwaguzi’ limetafsiriwa kuwa ni ‘mtu anayemtibu mgonjwa na kumponya’; au ‘mtu mwenye ujuzi wa kufasiri ndoto au kubashiri mambo yatakayokuja’. Kisha tukichuguza neno ‘uaguzi’ tunakuta limetafsiriwa kuwa ni i) Namna ya kubashiri mambo yatakayokuja au kutafsiri ndoto au ishara ii) Namna ya utoaji huduma agh ya dawa iii) Namna ya kutegua au kugangua uchawi
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu neno ‘mnajimu’ limetafsiriwa kuwa ni i)Mtu mwenye elimu ya mienendo ya nyota; ii) Mtu mwenye elimu ya kutabiri utokeaji wa matukio kulingana na elimu ya nyota. Halafu neno ‘unajimu’ limetafsiriwa kuwa ni i) Elimu ya nyota au ii) Kazi ya najimu; falaki
Neno la mwisho ni ‘mshirikina’ ambalo limetafsiriwa kuwa ni mtu mwenye kuamini na kupenda mambo ya uchawi na mazingaombwe; na neno ‘ushirikina’ limetafsiriwa kuwa ni ‘tabia ya kuamini mabo ya mambo ya uchawi, mizimu nk.
Hitimisho la tafsiri:
Tumegundua kwamba kiswahili kinatambua kuwepo kwa maneno ya uchawi, na wachawi, uaguzi na waaguzi na wanajimu, ushirikina na washirikina. Lakini pia baadhi ya tafsiri tulizozipitia zinatupa picha ya hisia walizokuwa nazo wataalamu wa lugha ya kiswahili.
Kwa mfano tafsiri isemayo: ‘mchawi ni mtu anayesadikiwa kuwa anaweza kuwadhuhuru watu kwa kuwaroga’. Usemi huu unatoa picha tofauti na uzito wa neno lenyewe. Kule tu kusema kwamba mchawi ni ‘mtu anayesadikiwa;’’ tayari kunaashiria kutokuwa na hakika kama kweli huyu ‘mchawi anaweza kuwadhuru watu kwa kuwaroga’!
Itaendelea toleo lijalo
Read More

0 comments:

Wednesday, 21 May 2014

  Bonyeza hapa kusikiliza JP Radio FM...Nyote mnakaribishwa

  HATIMAYE ZOEZI LA KUMSAKA CHATU JIJINI MBEYA LAANZA KUFANIKIWA BAADA YA KUKAMATWA KWA CHATU MDOGO!

SIKU chache baada ya wakazi wa Jiji la Mbeya kupewa tahadhari  juu ya uwepo wa nyoka mkubwa aina ya Chatu katika maeneo ya Rift Valley pembezoni mwa mto Meta uliopo jijini hapa juhudi za kumsaka zaanza kuzaa matunda.
 Juhudi za kumsaka Chatu huyo zilianza juzi kwa ushirikiano wa Wataalamu wa Wanyamapori pamoja na waganga wa jadi ambao walikuwa wakimsaka pembezoni mwa mtu huo.
 Hata hivyo jitihada za klumsaka Nyoka huyo zilianza kuzaa matunda baada ya jana asubuhi Waganga hao kufanikiwa kumnasa Chatu mdogo pembezoni mwa Mto Meta karibu na Hoteli ya Rift Valley.
 Kwa mujibu wa Mganga huyo, Mazoea Hamis(39) mkazi wa Chalinze mkoani Pwani alisema siku ya kwanza ya zoezi hilo walifanikiwa kugundua njia alimokuwa amepita lakini hawakufanikiwa kumpata.
 Alisema jioni yake baada ya kupumzika waliona waweke dawa za kienyeji ambazo zingiweza kumtoa mafichoni na kusogea karibu ambapo asubuhi waliwahi kuendelea kumtafuta.
Alisema baada ya muda kidogo wakati akiendelea kufyeka vichaka lakini kwa bahati nzuri alimkanyaga chatu huyo na yeye kukurupuka ndipo alipofanikiwa kumkamata.
Kwa mujibu wa mganga huyo ambaye anasaidiwa na Athman Keneth(30) mkazi wa Chunya mkoani hapa, alisema Chatu huyo ni mdogo na juhudi za kuendelea kumtafuta mkubwa zitaendelea kama kweli yupo.
Alisema mara nyingi Chatu mdogo anapoonekana Mkubwa anakuwa amehama ili kuwapisha wadogo kuendelea na maisha yao ama huyo mdogo alisombwa na maji kipindi cha mvua kutoka kwenye hifadhi na wenzie.
Hata hivyo taarifa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji zinadai kuwa baada ya kukamatwa kwa Chatu huyo atahifadhiwa na kutunzwa katika Hifadhi ya Wanyama ya Ifisi ambako kuna wanyamapori wengine wa maonesho.
Read More

0 comments:

Tuesday, 20 May 2014

  Bonyeza hapa kusikiliza JP Radio FM...Nyote mnakaribishwa

 MTOTO ALIYEIBIWA APATIKANA NA KUKABIDHIWA KWA WAZAZI WAKE

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi akimkabidhi mtoto Yosia Jerome kwa mama yake Orester Shabani 


Mume na mke baada ya kukabidhiwa mtoto wao wakitoka katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya


Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limemtia nguvuni mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Esther Amos(23) mkazi wa Nzovwe Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga  jinsi ya kiume mwenye umri wa miezi miwili.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema mtoto huyo Yosia Jerome aliibwa Mei 14 mwaka huu alipokuwa na mama yake aitwaye Orester Shaban(24) aliyekuwa akiuza mbogamboga katika soko la Ikuti Kata ya Iyunga Jijini Mbeya majira ya saa tatu asubuhi.

Mbinu aliyoitumia Esther ni kumrubuni mama wa mtoto kwenda kununua samaki huku akimkabidhi shilingi elfu kumi kuwa mbali ya njegere alizonunua kwa Orester pia angehitaji kupata samaki hivyo kumwachia mtoto ndipo alipotokomea naye kusiko julikana.

Kamanda ameongeza kuwa mama wa mtoto alitoa taarifa Polisi kituo cha Iyunga na Kati ambapo juhudi za kumtafuta mwanamke huyo zilianza na kufanikiwa kumpata Kijiji cha Mahenje Wilaya ya Mbozi nyumbani kwa Dada yake Esther.

Baada ya wasamaria wema kusikia taarifa za kuibiwa kwa mtoto wakazi wa Nzovwe walianza kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi walianza kufuatilia taarifa za Esther aliyedaiwa kujifungua na yupo kwenye mapumziko ya uzazi kwa Dada yake wilayani Mbozi.

Askari walifuatilia mwenendo wa Esther na kufanikiwa kumkamata Mei 18 mwaka huu majira ya saa saba akiwa na mtoto na alipotakiwa kutoa maelezo alionekana kujikanyaga na hata alipotakiwa kumnyonyesha alishindwa kufanya hivyo badala yake alitoa chupa ya maziwa kwa ajili ya kumnyonyesha.

Baada ya Askari kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa waliitwa wazazi wa mtoto kwa ajili ya utambuzi wa mtoto na baada ya kumtambua Orester alizirai kutokana na kutoamini kile kilichotokea machoni pake kupatikana mwanae akiwa hai.

Mtuhumiwa alisafirishwa hadi Jijini Mbeya kwa mahojiano zaidi na Esther ambapo uchunguzi umebaini kuwa katika maisha yake kabla ya kuolewa amejaliwa kupata mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa na alipoolewa hakujaliwa kupata mtoto ndipo alipodanganya mume wake kuwa ana ujauzito ambapo amekwenda kwa Dada yake kujitazamia.

Mtoto Yosia alifikishwa Hospitali ya Wazazi ya Meta na kwamba Afya yake inaendelea vema.

Kamanda wa Polisi alimkabidhi mtoto kwa wazazi wake Ofisini kwake mbele ya Waandishi wa Habari na Maafisa wa Polisi ambapo alitoa wito kwa wazazi kuwa makini na watoto wao na kutowakabidhi watu wasiowafahamu pia waendelee kushirikiana na Polisi ili kukomesha uhalifu Mkoani Mbeya na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Kwa upande wake Baba wa Mtoto Jerome Nzowa amelishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano mkubwa hata kufanikisha kupatikana kwa mwanae akiwa hai na salama.

 

HATIMAE MTOTO ALIYEFUNGIWA NDANI MIEZI TISA KWA ULEMAVU WA MDOMO SUNGURA ATIBIWA NA KUREJEA SALAMA CHUNYA

Mtoto Selemani Kolineli Mushi(Miezi kumi)kutoka Kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Baada ya kufanyiwa upasuaji wa mdomo sungura

Mtoto Selemani Kolineli Mushi(Miezi kumi) Kabla ya kufanyiwa upasuaji

Yohana Kolineli  mama mzazi wa mtoto huyo akiongea na mwandishi wetu ambae hayupo pichani

Baba mzazi Kolinel Mushin kushoto akimsikiliza mkewe kwa makini baada ya mama huyo kufika kijijini kwao



Mtoto Selemani Kolineli Mushin(Miezi kumi)kutoka Kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya amerejea salama Kijijini baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na kuzaliwa na matatizo ya mdomo sungura.

Mtoto huyo alifichwa ndani baada ya kuzaliwa na kutakiwa kurudi Hospitali ya Wilaya ya Chunya miezi sita baadaye lakini Baba Mzazi wa mtoto huyo aitwae Kolineli Mushin akikataa kumpeleka Hospitali akidai huo ni mpango wa Mungu.

Mwanzoni mwa mwezi Mei baada ya mtoto huyo kukutwa na mwandishi wa Mbeya yetu na kuwashauri wazazi wa mtoto ndipo walipokubali kumpeleka Hospitali ambapo dhamana hiyo ilichukuliwa na Afisa Ustawi wa jamii Anna Geleta la kusafirishwa hadi Hospitali ya CCBRT.

Selemani baada ya kupokelewa katika Hospitali ya CCBRT alifanyiwa upasuaji na kurekebishwa mdomo ambao ulikuwa ukimpa shida wakati wa kula na kupumua kwa shida na aliruhusiwa kutoka Hospitali Mei 15 Mwaka huu na kurejea Mbeya Mei 17 ambapo gharama za safari ya kwenda na kurudi na matibabu kugharamiwa na CCBRT.

Kwa upande wake Baba mzazi Kolinel Mushin na Mkewe Yohana Kolineli wameishukuru Mbeya yetu blog,  Serikali na Asasi ya CCBRT kwa kufanikisha matibabu ya mtoto wao ambapo wao walidhani kuwa ugonjwa huo usingetibika.

Aidha walimshukuru msamaria mwema Osward Mwailomo aliyetoa taarifa kwa mwanahabari na Mwenyekiti wa Kijiji cha Igundu kwa ushirikiano wake hata kufanikisha upasuaji wa mtoto na hali yake inaendelea vema.

Selemani atafanyiwa upasuaji wa pili mwezi Mei mwakani katika Hospitali hiyo ya CCBRT ambapo gharama zote hutolewa na Hospitali hiyo.

Read More

0 comments:

Monday, 19 May 2014

JAJI AMUHUKUMU KIFO MWANAMKE ALIYEBADILI DINI KUWA MKRISTO NCHINI SUDAN


Mwanamke wa kisudani aitwaye Meriam Yahia Ibrahim Ishag (27) jina ambalo analitumia baada ya kubadili dini na kuwa mkristo, amehukumiwa kunyongwa mpaka kifo na mahakama moja nchini huko Khartoum Sudan baada ya kukataa kata kata kuikana dini yake mpya na kurudi kwenye uislamu.

Mwanamke huyo alikuwa akifahamika kwa jina la Adraf Al-Hadi Mohammed Abdullah alipewa siku tatu kama nafasi kwake kurudi katika dini yake ya kiislamu lakini akabaki na msimamo wake kitendo kilichomfanya jaji Abbas Mohammed Al-Khalifa aliyekuwa akimuita mwanamke huyo kwakutumia jina lake la zamani la kislamu kwamba amemuhukumu kunyongwa mpaka kifo kwa kuukataa uislamu na kuwa mkristo ikiwa pamoja na kuchapwa viboko 100 kwa kosa la uzinzi kutokana na mwanamke huyo kuwa mjamzito.

Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo siku ya leo, mmoja kati ya viongozi wa kiislamu alienda
Baadhi ya wakristo wakiwa kanisani nchini Sudan.
kuzungumza na mwanamke huyo kwa dakika 30 akimsisitiza kubadili uamuzi wake bila mafanikio na kusikika akimwambia jaji Abbas kwamba yeye ni mkristo na hajawahi kushiriki uislamu na ndipo jaji huyo kutoka katika wilaya ya Haj Yousef alipoamua kumhukumu kifo huku mwanamke huyo akionekana kutostushwa na hukumu hiyo.

Baada ya hukumu hiyo watu wapatao 50 waliandamana kupinga hukumu hiyo wakisema si haki kwakuwa suala la dini ni haki kikatiba huku pia kundi lingine linalounga mkono hukumu hiyo liliwasili kuonyesha kuunga mkono jambo hilo huku ikielezwa hakutokea hali ya uvunjifu wa amani.

Mdau wa GK omba kwa ajili ya Meriam na taifa lake kwa ujumla, bila kusahau wakristo wanaopitia hali ya mateso kwasababu ya imani yao, lakini pia ombea wanaowatesa kwamba wakakutane na nguvu za Mungu. AMEN

Chanzo Yahoo

  Bonyeza hapa kusikiliza JP Radio FM...Nyote mnakaribishwa

VODACOM YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KYELA.

Mkuu wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule na Mwenyekiti wa chama cha msaraba mwekundu mkoa wa Mbeya Ulimboka Mwakilili wakimkabidhi mkuu wa wilaya Kyela Margareth Esther Malenga  Msaada waliotoa



Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Margareth Esther Malenga, akitoa shukrani kwa kampuni ya Vodacom na Chama cha Msalaba mwekundu kwa msaada walioutoa  kwa wananchi wake.

Mkuu wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule, alisema baada ya kupata taarifa za mafuriko wilayani Kyela Kampuni ilikaa na kujadiliana namna ya kutoa msaada kwa waathirika hao.



Ziara ya kwenda maeneo yaliokumbwa na mafuriko hali halisi ndiyo hii barabara zimeharibika

Jitihada zinaendelea kutengeneza miundo mbinu ya barabara



Wanafunzi wa shule ya msingi Kajunjumele wakiwa nje ya darasa lao

Mkuu wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule,akiongea na wanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi kajunjumele darasa hilo paa halina baadaya ya kukumbwa na kimbunga kilichoambatana na mafuriko yaliotokea hivi karibuni wilayani Kyela


Mwalimu akiwa nje ya darasa akisahihisha masomo ya wanafunzi wake 

Hii ni nyumba ya mwalimu tope limejaa ndani ya numba hiyo


Hali sasa imetulia na maji yanaenda kwa kasi ya kawaida



KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetoa msaada kwa Wananchi wa Wilaya ya Kyela kufuatia mafuriko yaliyoikumba Wilaya hiyo hivi karibuni na kutoa athari kubwa kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Margareth Ester Malenga, Mkuu wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule, alisema baada ya kupata taarifa za mafuriko wilayani Kyela Kampuni ilikaa na kujadiliana namna ya kutoa msaada kwa waathirika hao.
Alisema baada ya kuchangishana na kupata shilingi Milioni 10, walikubaliana na kitengo cha Msalaba Mwekundu juu ya vitu vinavyohitajika kwa haraka kwa ajili ya kuwapa msaada waathirika na ndipo walipowakabidhi fedha hizo.
Alisema Msalaba mwekundu walinunua Magodoro 500, Vyandarua 500 na mablanketi 500 vyote vyente thamani ya shilingi Milioni 10 ambavyo viliwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela juzi.
Aidha Mwakifulefule alitoa wito kwa mashirika mengine kujitolea kwa hali na mali misaada mbali mbali kwa wakazi wa Wilaya ya Kyela kutokana na kuwa bado na mahitaji muhimu.
Alisema hali badi ni tete na maeneo mengi yaliyoathirika bado hayajafikiwa hivyo ni vema taasisi zingine zikajitokeza kusaidia wananchi walioathirika na mafurika hayo.
Kwa upande waku Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Margareth Esther Malenga, akipokea msaada huo kwa niaba ya wananchi alitoa shukrani kwa kampuni ya Vodacom na Chama cha Msalaba mwekundu kwa msaada walioutoa wananchi wake.
Alisema Kampuni ya Vodacom inaubia na Serikali lakini ndani yake imekuwa ikiitumikia jamii na wananchi ambao ndiyo wateja wao na watumiaji wa bidhaa zao lakini wanaguswa na kutoa misaada mbali mbali kwa jamii inapokuwa inahitajika.
Mwisho.

 

  Read More

0 comments:

Recent News