
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Sangu, Mwalimu, Andongwisye Bukuku, Katibu wa Jumuiya ya wazazi, wilaya ya Mbeya Mjini, Juma Mng'ombe na Mkuu wa shule msaidizi Sophyllin Gwandage.

Mkuu wa shule msaidizi, Sangu sekondari, Sophyllin Gwandage akiwa ofisini kwake.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Sangu, Mwalimu, Andongwisye Bukuku.
Wanafunzi wa kidato cha tatu mchepuo wa Sayansi 1&2.
WADAU wa Elimu Nchini wameombwa
kujitokeza kuchangia maendeleo ya kielimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata
mazingira mazuri ya kujifunzia, ikiwa ni pamoja na walimu kufundishia.
Katika kuhakikisha wanafunzi
wanapata mazingira bora ya kujifunzia, shule ya sekondari SANGU inayomilikiwa na
Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), iliyopo Jijini Mbeya, imeandaa
harambee kwa ajili ya ujenzi wa maabara kubwa ya kisasa na ununuzi wa usafiri
wa basi la wanafunzi.
Akiungumza na
waandishi wa habari jana, Mkuu wa shule
hiyo, Mwalimu Andongwisye Bukuku, alisema Maabara hiyo inatarajia
kugharimu kiasi cha Tsh.111,000,000/=, wakati basi la shule litagharimu
shillingi milioni 50.
Alisema ujenzi
wa maabara hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa uwepo wa wanafunzi watakaosoma
masomo ya sayansi, na kuongeza kuwa wanafunzi
waliopo kidato cha tano na sita ni wale wenye michepuo ya sanaa (Art) pekee, hivyo
upatikanaji wa maabara hiyo utatoa fursa kwa shule hiyo kuanzisha michepuo ya
sayansi na wanafunzi kunufaika.
“Harambee hii tunatarajia
kuifanya Agost 14, mwaka huu, katika ukumbi wa Mkapa hapa Mbeya, ambapo mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha, NDG.ADAM KIGOMA MALIMA, ambapo matarajio yetu ni kupata
shilingi milioni 161.
Kwa upande wake katibu wa
Jumuiya ya Wazazi (CCM),wilaya ya Mbeya mjini, Juma Mng’ombe, amewaomba wadau wote
kujitokeza kwa wingi siku hiyo, kuunga mkono jitihada hizo hususani wanafunzi
wote waliosoma shuleni hapo miaka ya nyuma.
Amewataja baadhi ya watu
waliosoma shuleni hapo kuwa ni Rais wa Jamhuri ya watu wa Demokrasia ya
Kongo, Joseph Kabila, Mbunge wa Sindgida mjini, Azam Dewji na mbunge wa jimbo
la Songea Mjini Emmanuel Nchimbi.
Aidha,Mng’ombe amewaalika
wadau wote wenye mapenzi na elimu kote nchini kuchangia kupitia akaunti namba
iliyoanzishwa mahususi kwa ajili ya harambee hiyo…..
CRDB bank Tawi la Mbeya.
01J1065276501






%2B(1).png)
0 comments: