Total Pageviews

Recent news

About Us

Powered by Blogger.

Pages

Saturday, 3 January 2015

WATU 90 WAUWAWA KATIKA MAPIGANO BURUNDI

Unknown / / 0
Image result for WATU WAUAWA BURUNDI

Watu 90 wameuawa katika mapigano yaliyojiri kati ya askari wa Burundi na waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mkoa wa Cibitoke, kaskazini magharibi mwa Bujumbura. Msemaji mmoja wa jeshi la Burundi aliyefahamika kwa jina moja la 'Anatoli' amewaambia waandishi wa habari kwamba, mapigano hayo yaliyoanza tangu siku ya Jumatatu na kuendelea hadi jana, yaliibuka wakati waasi wanaokadiriwa kufikia 200 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walipojaribu kuingia nchini Burundi. Kwa mujibu wa afisa huyo wa jeshi la Burundi, askari wasiopungua 20 wamepoteza maisha huku zaidi ya waasi 70 wakiuawa. Kwa mujibu wa duru za jeshi la nchi hiyo, hadi sasa hakujatolewa ripoti kamili juu ya hasara iliyotokana na mapigano hayo. Inaelezwa kuwa waasi hao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walikuwa wamekusudia kuteka ardhi na kupora maliasili za eneo la Kibira nchini Burundi.

Unknown


Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit. Ut odio. Nam sed est. Nam a risus et est iaculis adipiscing. Vestibulum ante ipsum faucibus luctus et ultrices.
Follow me @Bloggertheme9

0 comments:

Recent News