-1.jpg)
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Kenya imesema safari zimeanza kama kawaida baada ya mamlaka hiyo kuondoa ndege zote kwenye njia ya kurukia ya Jomo Kenya mapema jana kufuatia tukio la ndege kutua kwa dharura.
Kwenye taarifa yake mamlaka hiyo imesema imemaliza uchunguzi wa njia ya kurukia ndege na sasa imefunguliwa, na safari zote za kuingia na kutoka zimerudi katika hali ya kawaida.
Awali mamlaka hiyo ilisema timu yake imefanikiwa kuiondoa ndege iliyotua kwa dharura kwenye njia ya kurukia, tukio ambalo lilisababisha ndege kutua kwa muda kwenye uwanja wa ndege wa Mombasa. Hadi sasa haijajulikana sababu ya ndege hiyo kutua kwa dharura na hakuna ripoti za watu waliokufa au kujeruhiwa kwenye tukio hilo.
%2B(1).png)
0 comments: