-1.jpg)
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa
Kenya imesema safari zimeanza kama kawaida baada ya mamlaka hiyo kuondoa
ndege zote kwenye njia ya kurukia ya Jomo Kenya mapema jana kufuatia
tukio la ndege kutua kwa dharura.
Kwenye taarifa yake mamlaka hiyo imesema imemaliza uchunguzi wa
njia ya kurukia ndege na sasa imefunguliwa, na safari zote za kuingia na
kutoka zimerudi katika hali ya kawaida.
Awali mamlaka hiyo ilisema timu yake imefanikiwa kuiondoa ndege
iliyotua kwa dharura kwenye njia ya kurukia, tukio ambalo lilisababisha
ndege kutua kwa muda kwenye uwanja wa ndege wa Mombasa. Hadi sasa
haijajulikana sababu ya ndege hiyo kutua kwa dharura na hakuna ripoti za
watu waliokufa au kujeruhiwa kwenye tukio hilo.