Ebola haizuwii mechi Sierra Leone

Wakuu wa kandanda wa Sierra
Leone wanasema mechi ijayo ya duru za mwanzo za Kombe la Afrika, baina
ya Sierra Leone na Ivory Coast, itafanywa ingawa kuna ugonjwa wa ebola
Afrika Magharibi.
Shirika la Kandanda la Sierra Leone limesema itataja timu yao ambayo itakuwa na wachezaji walioko nje ya nchi.Lakini haikutangaza wapi mechi itafanywa na pengine inaweza kupoteza mechi hiyo.
Huku nyuma nchini Nigeria, mjane wa daktari aliyekuwa mtu wa sita kufa kwa sababu ya ebola nchini humo, naye ameonekana ameambukizwa virusi.
Na wagonjwa watatu wa daktari huyo mjini Port Harcourt wamepelekwa katika zahanati maalumu lakini haikuthibitishwa iwapo kweli wana virusi vya ebola.
%2B(1).png)
0 comments: