JAJI AMUHUKUMU KIFO MWANAMKE ALIYEBADILI DINI KUWA MKRISTO NCHINI SUDAN
Mwanamke wa kisudani aitwaye Meriam Yahia Ibrahim Ishag (27) jina ambalo
analitumia baada ya kubadili dini na kuwa mkristo, amehukumiwa
kunyongwa mpaka kifo na mahakama moja nchini huko Khartoum Sudan baada
ya kukataa kata kata kuikana dini yake mpya na kurudi kwenye uislamu.
Mwanamke huyo alikuwa akifahamika kwa jina la Adraf Al-Hadi Mohammed
Abdullah alipewa siku tatu kama nafasi kwake kurudi katika dini yake ya
kiislamu lakini akabaki na msimamo wake kitendo kilichomfanya jaji Abbas
Mohammed Al-Khalifa aliyekuwa akimuita mwanamke huyo kwakutumia jina
lake la zamani la kislamu kwamba amemuhukumu kunyongwa mpaka kifo kwa
kuukataa uislamu na kuwa mkristo ikiwa pamoja na kuchapwa viboko 100 kwa
kosa la uzinzi kutokana na mwanamke huyo kuwa mjamzito.
Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo siku ya leo, mmoja kati ya viongozi wa kiislamu alienda
 |
| Baadhi ya wakristo wakiwa kanisani nchini Sudan. |
kuzungumza na mwanamke huyo kwa dakika 30 akimsisitiza kubadili uamuzi
wake bila mafanikio na kusikika akimwambia jaji Abbas kwamba yeye ni
mkristo na hajawahi kushiriki uislamu na ndipo jaji huyo kutoka katika
wilaya ya Haj Yousef alipoamua kumhukumu kifo huku mwanamke huyo
akionekana kutostushwa na hukumu hiyo.
Baada ya hukumu hiyo watu wapatao 50 waliandamana kupinga hukumu hiyo
wakisema si haki kwakuwa suala la dini ni haki kikatiba huku pia kundi
lingine linalounga mkono hukumu hiyo liliwasili kuonyesha kuunga mkono
jambo hilo huku ikielezwa hakutokea hali ya uvunjifu wa amani.
Mdau wa GK omba kwa ajili ya Meriam na taifa lake kwa ujumla, bila
kusahau wakristo wanaopitia hali ya mateso kwasababu ya imani yao,
lakini pia ombea wanaowatesa kwamba wakakutane na nguvu za Mungu. AMEN
Chanzo
Yahoo
 |
| Mkuu
wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya
Mwakifulefule na Mwenyekiti wa chama cha msaraba mwekundu mkoa wa Mbeya
Ulimboka Mwakilili wakimkabidhi mkuu wa wilaya Kyela Margareth Esther Malenga Msaada waliotoa |
 |
Mkuu wa
Wilaya ya Kyela, Margareth Esther Malenga, akitoa shukrani kwa kampuni
ya Vodacom na Chama cha Msalaba mwekundu kwa msaada walioutoa kwa
wananchi wake.
|
 |
Mkuu wa
Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya
Mwakifulefule, alisema baada ya kupata taarifa za mafuriko wilayani
Kyela Kampuni ilikaa na kujadiliana namna ya kutoa msaada kwa waathirika
hao.
|
 |
| Ziara ya kwenda maeneo yaliokumbwa na mafuriko hali halisi ndiyo hii barabara zimeharibika |
 |
| Jitihada zinaendelea kutengeneza miundo mbinu ya barabara |
 |
| Wanafunzi wa shule ya msingi Kajunjumele wakiwa nje ya darasa lao |
 |
| Mkuu
wa Kitengo cha Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya
Mwakifulefule,akiongea na wanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi
kajunjumele darasa hilo paa halina baadaya ya kukumbwa na kimbunga
kilichoambatana na mafuriko yaliotokea hivi karibuni wilayani Kyela |
 |
| Mwalimu akiwa nje ya darasa akisahihisha masomo ya wanafunzi wake |
 |
| Hii ni nyumba ya mwalimu tope limejaa ndani ya numba hiyo |
 |
| Hali sasa imetulia na maji yanaenda kwa kasi ya kawaida |
 |
KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetoa
msaada kwa Wananchi wa Wilaya ya Kyela kufuatia mafuriko yaliyoikumba Wilaya
hiyo hivi karibuni na kutoa athari kubwa kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada
huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Margareth Ester Malenga, Mkuu wa Kitengo cha
Maafa(Vodacom Foundation)kutoka Vodacom, Yesaya Mwakifulefule, alisema baada ya
kupata taarifa za mafuriko wilayani Kyela Kampuni ilikaa na kujadiliana namna
ya kutoa msaada kwa waathirika hao.
Alisema baada ya kuchangishana na kupata
shilingi Milioni 10, walikubaliana na kitengo cha Msalaba Mwekundu juu ya vitu
vinavyohitajika kwa haraka kwa ajili ya kuwapa msaada waathirika na ndipo
walipowakabidhi fedha hizo.
Alisema Msalaba mwekundu walinunua
Magodoro 500, Vyandarua 500 na mablanketi 500 vyote vyente thamani ya shilingi
Milioni 10 ambavyo viliwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela juzi.
Aidha Mwakifulefule alitoa wito kwa
mashirika mengine kujitolea kwa hali na mali misaada mbali mbali kwa wakazi wa
Wilaya ya Kyela kutokana na kuwa bado na mahitaji muhimu.
Alisema hali badi ni tete na maeneo
mengi yaliyoathirika bado hayajafikiwa hivyo ni vema taasisi zingine
zikajitokeza kusaidia wananchi walioathirika na mafurika hayo.
Kwa upande waku Mkuu wa Wilaya ya Kyela,
Margareth Esther Malenga, akipokea msaada huo kwa niaba ya wananchi alitoa
shukrani kwa kampuni ya Vodacom na Chama cha Msalaba mwekundu kwa msaada
walioutoa wananchi wake.
Alisema Kampuni ya Vodacom inaubia na
Serikali lakini ndani yake imekuwa ikiitumikia jamii na wananchi ambao ndiyo
wateja wao na watumiaji wa bidhaa zao lakini wanaguswa na kutoa misaada mbali
mbali kwa jamii inapokuwa inahitajika.
Mwisho.
|
No comments:
Post a Comment